Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Hadi kufikia leo zimepita siku kadhaa wizara ya afya ipo kimya, tangu ilipo tangaza idadi ya wagonjwa wa covid 19 kuongezeka hadi 299 na vifo 10 nchini Tanzania.

mbaya zaidi ndani ya kipindi hicho cha ukimya tanzia zinaongezeka zikiwemo za viongozi.

Hii inaleta mstuko mkubwa sababu huku kwetu elimu ya covid 19 ni ndogo sana,wengi wanaamini kunawa mikono na sabuni pamoja na kuvaa barakoa ndo suruhisho lakuthibiti korona.

Hii ina maanisha usafiri,biashara,mikusanyiko kwenye ibada (ramadhani) vipo kama kawaida,hivyo ni vema taarifa zikatolewa kila siku hata kama hakuna ongezeko zitoke hata za maendeleo ya wagonjwa tu.

Hata kama hali ni mbaya ni vema taarifa zikatoka hivyo hivyo,hii itasaidia wanachi hasa wanao ishi maeneo ya vijiji kuchukua tahadhali zaidi.
Mungu ibariki Tanzania,mungu ibariki Afrika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kukaa kimya ndo inaongeza taharuki wangekuwa wanatoa daily updates watu tujue kinachoendelea....Mbona majirani wameweza.
 
Hadi kufikia leo zimepita siku kadhaa wizara ya afya ipo kimya, tangu ilipo tangaza idadi ya wagonjwa wa covid 19 kuongezeka hadi 299 na vifo 10 nchini Tanzania.

mbaya zaidi ndani ya kipindi hicho cha ukimya tanzia zinaongezeka zikiwemo za viongozi.

Hii inaleta mstuko mkubwa sababu huku kwetu elimu ya covid 19 ni ndogo sana,wengi wanaamini kunawa mikono na sabuni pamoja na kuvaa barakoa ndo suruhisho lakuthibidi korona.

Hii ina maanisha usafiri,biashara,mikusanyiko kwenye ibada (ramadhani) vipo kama kawaida,hivyo ni vema taarifa zikatolewa kila siku hata kama hakuna ongezeko zitoke hata za maendeleo ya wagonjwa tu.

Hata kama hali ni mbaya ni vema taarifa zikatoka hivyo hivyo,hii itasaidia wanachi hasa wanao ishi maeneo ya vijiji kuchukua tahadhali zaidi.
Mungu ibariki Tanzania,mungu ibariki Afrika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waziri anaogopa kutimuliwa, inabidi amridhishe Mfalme kwa taarifa anazopenda kusikia na sio za idadi ya vifo.

Mwache Dada alinde ajira yake na aendelee vema na mfungo wa Ramadhan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wananzengo

Jamani sina mengi sana ya kuandika ila ninauliza tu Ugonjwa wa Corona umeisha hapa nchini kwetu Tanzania??

Maana nina muda sasa sijapata update ya wagonjwa wapya,waliokufa na waliopona nahisi kama umetoweka hivi

Tangu Magufuli ahutubie wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pale Chato ghafla sijapata taarifa mpya ya Ugonjwa

Au Yale maombi ya siku 3 yakiongozwa na Magufuli yameondosha Ugonjwa?

Manake kimya kabisa ,je Ugonjwa umeisha?

Mi naishi bush bush ndani huku Bukombe.
IMG_20200428_072026.jpg
 
Wasalaam wananzengo

Jamani sina mengi sana ya kuandika ila ninauliza tu Ugonjwa wa Corona umeisha hapa nchini kwetu Tanzania??

Maana nina muda sasa sijapata update ya wagonjwa wapya,waliokufa na waliopona nahisi kama umetoweka hivi

Tangu Magufuli ahutubie wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pale Chato ghafla sijapata taarifa mpya ya Ugonjwa

Au Yale maombi ya siku 3 yakiongozwa na Magufuli yameondosha Ugonjwa?

Manake kimya kabisa ,je Ugonjwa umeisha?

Mi naishi bush bush ndani huku Bukombe.View attachment 1433046
Watanzania chapeni kazi haka ni kahoma tu msitishwe....
 
Corona ipo sana inatuchora tu.

Tuendelee kuzika wapendwa wetu kwa idadi ya watu isiyozidi 10
 
naona kwenye picha mheshimiwa alikua live kwenye TV kubwa africa mashariki na kati.
 
Back
Top Bottom