Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Kwa sababu ni lazima wapate kibali cha kutamgaza kutoka chato......
Sasa wkt mwingine mkuu hua hajibu haraka akiwa na stress zake so mpaka aamue idadi ya kutangaza so ndio maana inachukua muda labda.....
Zanzibar ni nchi ndio maana angalau wanajitahidi
 
Wakuu,
Nchi nyingi duniani zilizo katika VITA dhidi ya ugonjwa Covid 19 zimekuwa zikitoa update za hali ya ugonjwa almost kila siku, hii inasaidia wananchi mmoja mmoja kujua ukubwa wa tatizo mkoa kwa mkoa hivyo kuchukua hatua stahiki.

Kumekuwa na tabia inaendelea kujengeka kwa serikali kutotoa taarifa za maambukizi kwa siku nyingi then wanakuja kutoa.

Mfano mara ya mwisho walikaa siku 5 bila kutoa taarifa then wakatoa ikaonyesha kuna maambukizi mapya 196!!! Hii ni mbaya inachafua sifa ya nchi kimataifa, duniani sehemu kubwa wamechukulia kwamba tuna new cases 196 in 24 hours ambapo sio kweli!

Hii kitu ktafanya nchi iogopwe hata baada ya huu ugonjwa kupita.
Serikali ibadilike kwenye hili, taarifa zitolewe kila siku.
 
Pamoja na kuwa tunatakiwa kutii mamlaka, na tunatii kwelikweli, lakini ukweli unatabia ya kupenyapenya kama maji yanayovuja.

Raia tuna jamaa mikoa mbalimbali, kila unayesalimiana nae anakwambia hali ni mbaya.

Sasa hata kama mamlaka haitasema hali ni mbaya, itafika mahali raia wote watakubaliana kuwa kuna ukweli usiosemwa.

Ni hatari wakichukua maamuzi ya kiwenda wazimu. Maana hakuna atakaejali chochote.

Naamini katika hili kiongozi wetu mkuu anatumia kila rasilimali mtu iliyopo kutafuta namna bora ya kukabiliana na janga hili na adha zake zote.

Wataalamu wa kimataifa wanatujuza kuwa ugonjwa huu ukishambulia jamii una kawaida ya kuanza kama mvua yaani vimanyunyu, upepo na ubaridi, mvumo, mvua kubwa labda na mawe. Yanaweza kutokea hadi mafuriko na mvua haija kata.

Swali ni sisi tupo hatua gani, maandalizi na hatua tuchukuazo binafsi na kama nchi hakuna cha kuboresha?

Mvua itakapo kata tutakuwa na hali gani?

Bado naamini kuna maamuzi magumu yanatakiwa kuchukuliwa katika ngazi mbalimbali kupunguza usambaaji wa mdudu corona.

Ni yapi hayo? Wataalamu wahusishwe kimkakati kupata mbinu bora za kupunguza maambukizi ya kasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni swali chokonozi and it is a matter of curiosity. Takribani wiki sasa tangu tutangaziwe maambukizi na vifo vya COVID19. Hata hivyo tangazo hilo lilikuja baada ya kelele kuzidi huku.

Baada ya idadi mpya kutangazwa Mh.Rais alikuja na tuhuma mpya ya kuhisi ama vifaa vya kupima vina matatizo au kuna hujuma inayosababisha idadi kuwa kubwa.

Sambamba na hilo mbunge aliyekuwa akipigania idadi ya wagonjwa isitangazwe alipandishwa cheo.

Baada ya hapo idadi ya maambukizi mapya haijatangazwa tena.

Naomba kujua kwa hiyo baada ya kuonekana vipimo vinachakachua ndio idadi ya maambukizi haitangazwi tena mpaka itakapoamuliwa?

Idadi ya vifo je nayo imesimamishwa
 
Siyo na ndiyo kwa wakati mmoja. Utatoaje takwimu kwa vipimo visivyoaminika??
 
Wewe ukishapata idadi, wewe na mama yako ndio mnakuwa mmepata dawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusubili uchunguzi ukamilike nadhani ni baada ya miezi 6 tuvumilie
Tuwe makini na shughuli zetu za kila siku
 
Ni swali chokonozi and it is a matter of curiosity. Takribani wiki sasa tangu tutangaziwe maambukizi na vifo vya COVID19. Hata hivyo tangazo hilo lilikuja baada ya kelele kuzidi huku.

Baada ya idadi mpya kutangazwa Mh.Rais alikuja na tuhuma mpya ya kuhisi ama vifaa vya kupima vina matatizo au kuna hujuma inayosababisha idadi kuwa kubwa.

Sambamba na hilo mbunge aliyekuwa akipigania idadi ya wagonjwa isitangazwe alipandishwa cheo.

Baada ya hapo idadi ya maambukizi mapya haijatangazwa tena.

Naomba kujua kwa hiyo baada ya kuonekana vipimo vinachakachua ndio idadi ya maambukizi haitangazwi tena mpaka itakapoamuliwa?

Idadi ya vifo je nayo imesimamishwa
Kuuliza si ujinga, siku ile Mkiti alitoa hotuba moja nzuri na moja ya agizo ilikuwa ni kukusanya idadi binafsi ya waathirika wa Covid 19. Je, maendeleo yakoje?

Au ngurumo ya Simba wa Burigi imewakumba kama ilivyoikumba wizara ya Afya Zanzibar na Tanganyika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo na ndiyo kwa wakati mmoja. Utatoaje takwimu kwa vipimo visivyoaminika??
Hivi kati ya nchi zilizokumbwa na covid-19 kuna nchi zingine zaidi ya sisi zenye tatizo kama la kwetu la kutoa majibu ya vipimo yasiyoaminika au ni sisi tu ndiyo tumeonewa na hao mabeberu?
 
Hivi kati ya nchi zilizokumbwa na covid-19 kuna nchi zingine zaidi ya sisi zenye tatizo kama la kwetu la kutoa majibu ya vipimo yasiyoaminika au ni sisi tu ndiyo tumeonewa na hao mabeberu?
Kwanza ni lazima aina ya hicho kipimo itajwe ili mjadala uanzie hapo.
 
Back
Top Bottom