Kwanini tukarabati kivuko kwa Tsh. bil 7.5 wakati kipya ni bil 8.5?

IKO NAMNA, BASI S BORA KINUNULIWE KIPYA?
Mkuu hupo sahihi,kwanza huyo waziri nadhani hajui uhalisia, Mungu anisamehe.
1.Kazi za ukarabati kwenye karakana ya African Marine ni kichekesho,Sio Ile African Marine ya enzi zile.
2.Muda wa kukarabati kama kuikarabati kisawasawa utakuwa muda mwingi kuliko hizo commitments zao.Waziri asiigizwe kwa wapigaji,itamtokea puani,amini usiamini.
3.Hata kama zitaletwa Machine mpya LAKINI hakuna uhakika wa kufanya perfect installation hilo nina uhakika nalo.
4.Lets go to plan B.either kununua bland new,au ikarabatiwe hapa hapa nyumbani kwenye karakana zetu yaani TPA Drydock,au Navy hata karakana za muda as long as tunampata capable contractor mwenye weledi and appropriate, manpower na vifaa vyakutoshereza, thabiti vya kufanyoa kazi.
 
IKO NAMNA, BASI S BORA KINUNULIWE KIPYA?
Nakubaliana na wewe. Hicho chakavu kizamishwe kwenye bahari ya kina kirefu yawe mazalia ya samaki.
Hakuna mtu mwenye chembe ya akili anayeweza kukarabati gari bovu ambalo sio Classic kwa gharama ya kununua jipya. Hapa kuna nia mbaya. Mbona MaV8 ya zamani hayakarabatiwi, tunanunua mapya kila mwaka!!
 
Well analyzed,
Naibu waziri wa Afya juzi ametoka kusema kuwa washauri wengi wa mama ni wajinga, nadhani alimaanisha ujinga wa kutojia mambo lkn pia ujinga wa kudhani watanzania ni wale wale wa kuwadanganya siku zote.

By the way bado nakiona kivuko pale usikute wamekuja shituka kuwa wanapigwa ndo wameamua kukisubirisha!!
 
Serikali ya awamu ya sita imeshikiliwa na mafisadi wa awamu ya nne upigaji katika manunuzi haiepukiki. CCM ni chama kilichojaa wezi, mtu safi hawezi kupatikana humo.
 
Wanaangalia upepo ukitulia tu kinang'oa nanga kwenda ...hawa watu hawana huruma kabisa
 
Kula watu wale lakini mengine ni mambo ya msingi sana! Kuacha roho za watu rehan ni kujitaftia laana ndo maana viongozi wanaandamwa na mapooza
Hii ndiyo bongo land. Watu wanapiga pesa.
Afrika kuna matatizo mengi sana.
 
Tungeweka sheria za kunyonga wote wanaoidhinisha hujuma!
Inakuwaje pesa nyingi namna hiyo zinaidhinishwa kizembe!
Kosa kubwa tulilolifanya Tanzania.
Kila kitu kinaongozwa na viongozi ( viongozi wapo juu ya sheria. Ilitakiwa iwe hivi
1. Viongozi wajitegemee. Hapa hautaona Mkuu wa mkoa anaenda shule fulani kuchapa wanafunzi viboko.
2. Mahakama ijitegemee
3. Sheria na katiba ijitegemee
4. NEC ijitegemee
5. Jeshi la polisi lijitegemee
6. Vyama vya siasa vijitegemee
7. Elimu ijitegemee
Tukifanya hivi, 1-7 vitakuwa na nguvu kwasababu gharama za matengenezo ya meli yatafanywa kwa usahihi kwa gharama stahiki. Kwasababu 1-7 havijitegemei ndipo unapoona kiongozi ambaye hana ABC anatenga bajeti kwa mtizamo wake anaruhusu bajeti hiyo akijua hakuna sheria itakayomshitaki kwasababu 1-7 anavisimamia yeye.
Hii ndiyo Afrika ndugu. Kama kibanda cha mlizi kinajengwa kwa milion 10 huwezi kushangaa bajeti hii
 
Hawa Jamaa ni wapuuzi sana ,watanzania wasasa sio wajinga ,watu wameelimika,yaani Temesa na waziri wanajitokeza hadharani kutetea wizi inafikirisha sana.

Mh Rais embu zuia kwanza huu wizi ,huu ni upigaji wa waziwazi ,wananchi tunachukia kwasababu mnatutoza mikodi ya kila aina ambayo haina kichwa wala miguu halafu kumbe fedha mnawapa wezi wanazibanjua tu,mnamuongezea mwananchi ugumu tu wa miasha.

Eti waziri anajitokeza na kusema eti kivuko gharama yake ya sasa ni 25B ,hes serious? Hivi meli ya mwaka 2008 iliyokuwa na thamani ya 8.5B kwasasa inauzwa 25B? Its utter non-sense ,Fukuza huyo waziri maana anatufanya waTZ wote ni Mapoyoyo.......Kipindi Range Rover zinaingia hapa TZ tena enzi hizo alikuwa nazo Nimrod Mkono zilikuwa zinauzwa 200m+ ,je kwasasa hizo range gharama yake ni 600m+?? Kipindi Murano zinashika kasi nakumbuka Mwanadada Lady JayDee alinunua kwa mil 50+ ,Je kwa soko la sasa zinauzwa 150m+? Kwa kifupi nataka kusema kwamba devices huwa inashuka thamani kutokana na muda kwasababu ladri muda unavyoenda devices za kisasa zinaundwa na kuifanya ile ya nyuma isiwe na soko hivyo inapunguza price,hii ni kwa vitu vyote hata S9 wakati zinaingia price yake ilikuwa hatari lakini sasa hadi mchunga ngombe akizichanga anamiliki s9.
 
Lakini hebu ifike mahali tujeshimiane kwakweli, hii nchi hamuongozi ng’ombe jamani, hebu acheni huu ushetani mara moja, upigaji gani huu?! Kuweni na huruma!!
 
Hiyo ndiyo Serikali ya CCM,

Hao Ndiyo Wachawi Wetu.
 
Sisi watanzania ni wajinga sana aisee

Mwaka 2008 kivuko kilikua ni 8b leo mwaka 2023 kukarabati kivuko icho ni 7.5b je tumejiuliza bei ya kivuko icho kwa mwaka huu 2023?

Maana ni takribani miaka 15 imepita toka kinunuliwe...
 
Endapo kivuko kimenunuliwa mwaka 2008 je watu walikuwa wanavuka bure?

Kama hapana je hizo pesa mnazopata Kama nauli ya Mtu kuvuka katika kivuko Cha MV Magogoni Tangu 2008 hadi 2023 je hazitoshi kununua kivuko kipya na kukarabati kilichopo.

Mbona Mimi bodaboda naweza kuendesha bodaboda iloyotumika Hadi nikanunua bodaboda mpya yaani boda moja ikazaa nyingine.

Naomba ufafanuzi juu ya hili swala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…