Kwanini tunachukiana makazini? Yani shida inakuwa nini?

Kwanini tunachukiana makazini? Yani shida inakuwa nini?

nadhani kwa sisi waafrila chuki makazini ni kitu kimezoelekana

kuna jamaa alikuwa ananichukia kazini bila sababu ...nikaja kugundua sababu kuna dda tunaitana homeboy na homegirl wote tunatoka mbeya

jamaa huwa anamtaka demu halafu demu hamtaki jamaa so jamaa chuki zake akazileta kwangu

niikuwa nampuuza mpaka yeye mwenyewe akaja kujua mimi ni tofauti na alivyonidhania
 
From no where mtu huna time nae ananza kukuletea visa visa vya hapa na pale kuna mda unaweza pata hasira hizi kazi za kuajiriwa ni upuuzi.

Yani ukijichaganya uka react tu unaweza timuliwa kazi. Swali langu wakuu kwanini hasa hawa Wanawake wanakua ni sosi ya mashindano kazini? Na nini kifanyike kuepukana na haya mambo?
Piga kazi,ukiingiza battle za kijinga utashtuka slip unasoma one year to retire,ukifeli simama Tena,huko mbele hakuna mtu wa kujibu hoja ngumu isipokuwa wewe,ukimaliza kazi go home,ukiona vipi chili na wanao fanya yako ya dunia hayana mwisho
 
nadhani kwa sisi waafrila chuki makazini ni kitu kimezoelekana

kuna jamaa alikuwa ananichukia kazini bila sababu ...nikaja kugundua sababu kuna dda tunaitana homeboy na homegirl wote tunatoka mbeya

jamaa huwa anamtaka demu halafu demu hamtaki jamaa so jamaa chuki zake akazileta kwangu

niikuwa nampuuza mpaka yeye mwenyewe akaja kujua mimi ni tofauti na alivyonidhania
Watu wa mbeya tunachukiwa in Advance sababu ni kupambana,kila mtu anapambana na shida ni kufunguka codes watesi wanajiona hawana jipya.
 
Katika taasisi zote nilizowahi kufanya kazi, watu wake wote wanafanana kitabia. Nadhani hii ni common African behavior. Wafanyakazi wenzio hawatakaa wapende mabadiliko chanya katika hali yako ya kimaisha, iwe ni kiuchumi, kiimani, kijamii nk.

Unaweza ukakuta daraja fulani la wafanyakazi ambalo linapokea kiwango sawa cha mshahara au gape la mshahara ni dogo tena ni kutokana na uzoefu. Sasa itokee umeamua kuchagua maisha ya kutokula bata zisizo na maana (pombe na wanawake) ukaamua kutumia hela yako kuboresha hali yako ya kimaisha kwa kufanya vitu vya maana (kununua assets au shughuli yakukuongezea kipato) chuki, fitina, visa na vitendo vya kishirikina utakavyokutana navyo kama humtegemei Mungu na hujasimama kiimani nakwambia huwezi toboa hapo kazini.

Na jinsi binadamu walivyo wa ajabu, wanaweza wakakusaka kote huko kisirisiri ila wakikushindwa kuna siku tu watakwambia kabisa jinsi lifestyle yako inavyowanyongorota, iwe kwa bahati mbaya au makusudi.

Nadhani hii hulka huenda ndio sababu kuu iliyomfanya shetani akachagua mizizi wa Uchawi Mweusi (Black Magic) aichimbie Afrika.
Mkuu umeongea kweli tupu

With experience
 
From no where mtu huna time nae ananza kukuletea visa visa vya hapa na pale kuna mda unaweza pata hasira hizi kazi za kuajiriwa ni upuuzi.

Yani ukijichaganya uka react tu unaweza timuliwa kazi. Swali langu wakuu kwanini hasa hawa Wanawake wanakua ni sosi ya mashindano kazini? Na nini kifanyike kuepukana na haya mambo?
Posho n vyeo
 
Back
Top Bottom