Kwanini utawala wa Nyerere ulikumbwa na misukosuko mingi ukilinganisha na utawala wa Mwinyi, Mkapa na wengine?

Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salamu, ningependa nijielekeze kwenye mada husika. Ndugu zangu watanzania, baba yetu wa Taifa mwl Julius K Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa muda wa miaka 25. Kwa muda wote huo wa uongozi wake, nchi yetu ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo haikuja kutokea katika tawala zingine. Mfano wakati wa utawala wa Nyerere tuliona majaribio mawili ya mapinduzi yalioshindwa, hali iliyopelekea mzee wetu aamue kung'atuka mwenyewe kabla haja ng'atuliwa, maana kwa hali ya nchi ilivyokuwa kipindi kile bila shaka mwenyewe aliona kwamba asingeweza kumaliza miaka mingine mitano akiwa madarakani.

Lakini pia ukiachana na hayo ya mapinduzi pia kulikuwa na misuko suko mingine, mfano yale mauaji yaliosababisha waziri wa mambo ya ndani wa wakati ule mzee wetu mh Ally H Mwinyi kujiuzulu uwaziri. Pia kulikuwa na misuko suko mingine iliyopelekea kina mzee Kawawa, bibi Tito Mohammed na wengineo kufungwa jela. Lakini kama hiyo haitoshi, wapo waliamua kukimbia hata nchi na kwenda kuishi ughaibuni, mfano mzee wetu hayati Oscar Kambona na wengineo.

Hapo sijagusia ukosefu wa vitu muhimu nchini kama vile chakula, mafuta ya kupikia na ya taa, ukosefu wa madawa hospitalini, usafiri kuwa washida mpaka yakaletwa yale magari yalioitwa chai maharage, mzunguko wa pesa mtaani ukawa wa mdondo. Nguo, viatu, soksi, mafuta ya kupaka, sabuni navyo vikawa havipatikani.

Cha kushangaza alipoondoka mwl Nyerere na kuingia Mwinyi, hali ilibadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuna aliethubutu kuwaza tena mapinduzi, bidhaa zote muhimu zilipatikana kwa urahisi mitaani. Mzunguko wa pesa ukawa mkubwa, mitumba ya nguo, viatu, soksi kila kona, madawa yakawa mengi hospitalini mpaka watu wakaamua kufungua na zahanati zao. Pia hakuna aliewaza tena kukimbia nchi, isipokuwa tuliishuhudia wale waliokimbia utawala wa kwanza wanaaza kurejea katika utawala huu wa pili nk.

Hali hii aliyoanza nayo Mwinyi, naona imeendelea hadi leo. Je, ni kwanini misuko suko ilikuwa zaidi wakati wa awamu ya kwanza na sio awamu zingine? Je mwl Nyerere alihujumiwa au sera zake mwenyewe ndio zili muhujumu? Inamaana mzee Mwinyi kwa kutumia uwezo wake na cheo chake aliweza kulisuka vizuri jeshi letu na kurejesha utiifu wao kwa serikali yao na raisi wao? Je inamanaa Mwinyi hakuwa na maadui wa kuitingisha serikali yake, hadi kupelekea wengine kukimbia kama walivyokimbia awamu ya kwanza? Mwenye kujua zaidi sababu zilizopelekea mwl Nyerere kushindwa kuituliza hali, hadi kuamua kung'atuka anakaribishwa kutujuza. Asanteni sana kwa kunisoma?
Kunenga Msingi wa Taifa lenye Falsafa na itikadi mpya kutoka ile ya kikoloni haikuwa jambo rahisi.
Ni watu wachache walipambana kwaajili ya maslahi ya wengi. Walafi wachache walikwamisha na kuwaumiza wengi
 
Inawezekana hao wachache ndio waliokuwa wanaididimiza nchi, na kuifanya serikali ya mwl Nyerere ionekane na hovyo.
 
Hakuna wa kumlinganisha na Nyerere katika awamu zote. Amekuta pori akaanza kufyeka, kung'oa visiki halafu unauliza kwa nini wakati wake alikutana na nyoka wengi? Labda tukuulize kwa nini Nigeria hakuna mapinduzi Kama ilivyokuwa 60/70/80 na 80s? Nao walikuwa wajamaa?
Dogo una akili sana weye....unakunywa kinywaji gani labda!!!!.......Naongezea hapo mchonga alikuwa mw/kiti makao makuu ya nchi zilizo mstari wa mbele ktk ukombozi wa nchi za kusini mwa Bara la Africa.na sasa SADDAC..maadui jirani na wengi wa kusini makaburu/wareno/ hawakulipenda hilo.....walitamani kumkomesha km adui yao. ili waendelee kunyonya kwa amani.walishindwa vibaya.ivo alikuwa na adui wenye nguvu tena walio karibu yake mnoo.....pili kitendo cha siasa za kutofungamana na upande wowote kiliwaumiza Mabeberu....tatu walijua TZ itafanikiwa mbaya kwa kuanzisha viwanda vyake yenyewe....aliacha viwanda vizimaa 1500 vilivyokuwa vina fanya kazi usiku na mchana mfano Tanga nyika packers..mwatex mutex nk. Hapo tu tuliuza sana tu....alikuwa mbunifu mfano aligundua sabuni ya magwanji, kiwi ya mishumaa nk......ubunifu huu kwa beberu aliumia sana.....walipoona hatuwapigii magoti....kitendo cha nyerere kukataa wazi waxi misaada ya Uk/ujermani...tena akawarudishia hela yao cash...kiliwaumiza sanaaaa.mabeberu....kitendo cha kusadia sana kwa hali na Mali wapigania uhuru wa Africa nzima....lazima beberu hakupata usingizi.......kifupi mchonga alitawala kipindi ambacho alizungukwa na maadui wengi wenye nguvu....hapo bado vibaraka wa ndani na nje walio sumbua sana utulivu wa ndani na nje ya nchi...mfano ni wale vibaraka km Kamuzu Banda.....Mobutu seseseko,Idd Amin....Alfonso Dhlakama...nk. Ilibidi apigane nao kwa level ya nchi..kidunia na maisha yake binafsi....pia apigane kiuchumi nchi iweze kisimama imara....wengi ulaya walimtamani sana hadi kufika mbali wakisema na kukiri wazi yule siyo damu ya kiafrica.....wakaomba kumuazima.....akakataa!!!walio fuata wooote walisalimu amri kwa Beberu.....Pia jua kwamba mapinduzi yalikuwa hot miaka ya nyuma wkt Dunia iko hot yaani .....imegawanyika sehemu mbili western na eastern...kote kote Rais una chagua ukae upande upi.....sasa wasaliti wakoloni wako uone cha moto mfano mzee j/kenyatta alionywa na beberu asithubutu kufuata siasa ya ujamaa km anautaka urais.wala asithubutu kuunga mkono harakati za ukombozi africa lkn mchonga aliwakatalia waziwazi so waka ahidi kumkomesha kiuchumi,kisiasa hata kugharimu maisha yake binafsi km walivo wafanya nkwame Nkrumah..Tafawa balewa...Lumumba, nk!! Kwa kumtishia julius....Lkn mwanaume alikomaa na msimamo wake wakashindwa mbayaaaa!........leo hayo yapo lkn siyo hot km miaka hiyo....hii ilimjengea heshima Duniani hakika hkn km Nyerere!
 
Sera za ujamaa hazikuwa mbaya ila Kambarage alipoteza mapato ya nchi kusaidia wengine wapate uhuru wewe fikiria kule Kongwa walikuwa wanalishwa tu bure bure na hizo nchi kwa Sasa hazina hata shukrani kwa Watanzania ,unakijua kisa Cha Kambarage kuuza Meli ya serikali kimyakimya na Sokoine akataka kumtumbua bosi wake.
Acha uongo wakimbizi wote Duniani wanalishwa na shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani....kuanzia nguo kula na tibank...mpaka sasa. Na hata km unawasaidia ndg zako kuna ubaya gani??....aliamini binadamu wote ni sawa na Africa ni moja
.....stop dat primitive nosense behaviour!...but sorry!
 
Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salamu, ningependa nijielekeze kwenye mada husika. Ndugu zangu watanzania, baba yetu wa Taifa mwl Julius K Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa muda wa miaka 25. Kwa muda wote huo wa uongozi wake, nchi yetu ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo haikuja kutokea katika tawala zingine. Mfano wakati wa utawala wa Nyerere tuliona majaribio mawili ya mapinduzi yalioshindwa, hali iliyopelekea mzee wetu aamue kung'atuka mwenyewe kabla haja ng'atuliwa, maana kwa hali ya nchi ilivyokuwa kipindi kile bila shaka mwenyewe aliona kwamba asingeweza kumaliza miaka mingine mitano akiwa madarakani.

Lakini pia ukiachana na hayo ya mapinduzi pia kulikuwa na misuko suko mingine, mfano yale mauaji yaliosababisha waziri wa mambo ya ndani wa wakati ule mzee wetu mh Ally H Mwinyi kujiuzulu uwaziri. Pia kulikuwa na misuko suko mingine iliyopelekea kina mzee Kawawa, bibi Tito Mohammed na wengineo kufungwa jela. Lakini kama hiyo haitoshi, wapo waliamua kukimbia hata nchi na kwenda kuishi ughaibuni, mfano mzee wetu hayati Oscar Kambona na wengineo.

Hapo sijagusia ukosefu wa vitu muhimu nchini kama vile chakula, mafuta ya kupikia na ya taa, ukosefu wa madawa hospitalini, usafiri kuwa washida mpaka yakaletwa yale magari yalioitwa chai maharage, mzunguko wa pesa mtaani ukawa wa mdondo. Nguo, viatu, soksi, mafuta ya kupaka, sabuni navyo vikawa havipatikani.

Cha kushangaza alipoondoka mwl Nyerere na kuingia Mwinyi, hali ilibadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuna aliethubutu kuwaza tena mapinduzi, bidhaa zote muhimu zilipatikana kwa urahisi mitaani. Mzunguko wa pesa ukawa mkubwa, mitumba ya nguo, viatu, soksi kila kona, madawa yakawa mengi hospitalini mpaka watu wakaamua kufungua na zahanati zao. Pia hakuna aliewaza tena kukimbia nchi, isipokuwa tuliishuhudia wale waliokimbia utawala wa kwanza wanaaza kurejea katika utawala huu wa pili nk.

Hali hii aliyoanza nayo Mwinyi, naona imeendelea hadi leo. Je, ni kwanini misuko suko ilikuwa zaidi wakati wa awamu ya kwanza na sio awamu zingine? Je mwl Nyerere alihujumiwa au sera zake mwenyewe ndio zili muhujumu? Inamaana mzee Mwinyi kwa kutumia uwezo wake na cheo chake aliweza kulisuka vizuri jeshi letu na kurejesha utiifu wao kwa serikali yao na raisi wao? Je inamanaa Mwinyi hakuwa na maadui wa kuitingisha serikali yake, hadi kupelekea wengine kukimbia kama walivyokimbia awamu ya kwanza? Mwenye kujua zaidi sababu zilizopelekea mwl Nyerere kushindwa kuituliza hali, hadi kuamua kung'atuka anakaribishwa kutujuza. Asanteni sana kwa kunisoma?
Screenshot_20220812-173209.jpg

Learn from here
 
Acha uongo wakimbizi wote Duniani wanalishwa na shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani....kuanzia nguo kula na tibank...mpaka sasa. Na hata km unawasaidia ndg zako kuna ubaya gani??....aliamini binadamu wote ni sawa na Africa ni moja
.....stop dat primitive nosense behaviour!...but sorry!
Wewe ndio nonsense, aliyekuambia walikuwa wakimbizi nani ingekuwa wakati huu kwa taarifa yako wale wote terrorist
 
Kwa aina hii ya maneno ya mzee ruhusa, ni kama vile Kikwete alitaka kuuza uhuru wetu kwa weupe 😂😂😂.
Cha ajabu nyerere aling'atuka baada ya kukosa mkopo imf na wb mpaka abadili sera,mwinyi alikopa mpaka tukawa hatukopesheki,mkapa alilipa madeni ili tusamehewe madeni na tukopesheke...na bajeti ya serikali zote hizo ni tegemezi kwa wafadhili na wakopeshaji
 
Ukitazama trend utajifunza jambo tunaamka cherekochereko tunalala hatujui kesho yetu
 
Wewe ndio nonsense, aliyekuambia walikuwa wakimbizi nani ingekuwa wakati huu kwa taarifa yako wale wote terrorist
Bado unaonyesha umburula tu.....hata km siyo wakimbizi..ndg yako akila unaumia nini?..
Tulisha waambia maneno rahisi tu......africa ni moja....mipaka hii aliiweka Babu yako??? Anaijua???....Leo tokea Bagamoyo indian ocean mpaka pacific kuree kinshasa....ni kiswahili tuuu.....kwa nini watenganishwe??.....tena usirudie kuwaita terrorists!! Vinginevyo tunaanza na wewe kukula kichwa...msaliti nyambaf!!!
 
Cha ajabu nyerere aling'atuka baada ya kukosa mkopo imf na wb mpaka abadili sera,mwinyi alikopa mpaka tukawa hatukopesheki,mkapa alilipa madeni ili tusamehewe madeni na tukopesheke...na bajeti ya serikali zote hizo ni tegemezi kwa wafadhili na wakopeshaji
Kwa namna Mwinyi alivyoikuta nchi yetu, kwa kweli hapakuwa na namna yoyote ya kuendesha nchi bila kukopa ili apate hela za kuleta maendeleo kama vile kujenga hospital (kabla yake hospital zilikuwa chache, tena zimechoka kutokana na hali mbaya ya uchumi.
Nyingi zilikuwa hazina madaktari wala manesi wa kutosha, na hospital zingine zilifungwa kabisa kwa sababu madaktari waligoma kufanyakazi isiyo na malipo) alinunua madawa mbali mbali baada ya hospital nyingi kukosa madawa, alijenga barabara (kabla yake pia barabara zilikuwa zimechoka, mfano morogoro road ilikuwa na njia mbili tu, Mwinyi ikabidi aipanue, na ndio hizi zilizoendelea kutumika hadi hapa juzi serikali ipoamua kuja na plan ya njia 8),

kajenga shule ktk baadhi ya maeneo ambayo hayakuwa na shule, kajenga ofisi mbali mbali za serikali baada ya kukuta zilizopo zilikuwa hazina hadhi hata ya kutumiwa na mjumbe wa nyumba 10, ilibidi akope ili kupata hela za kuwalipa watumishi wa serikali kama vile mawaziri, makatibu, madaktari, walimu, wafanya kazi mbali mbali katika ofisi za umma, askari wa vyombo vya ulinzi na usalama (hili lilikuwa kundi muhimu kupewa mshahara maana bila hivyo lingeendelea kufanya uasi dhidi ya serikali),
hii ilisababisha nchi kufunguka. Watu wakafungua maduka, dispensary, zahanati, pharmacy mbali mbali za kuuza madawa, maduka ya nguo za mitumba na dukani, maduka ya tv, radio na vyombo vingine vya moto.

Hela ikaanza kuonekana mtaani, maisha yakaanza kuwa ya kawaida kama zilivyo nchi za wenzetu za Kenya, Uganda nk ambapo hapo awali walituona kama sisi tunaishi kitumwa nk. kupatikana kwa wingi mtaani.
 
Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salamu, ningependa nijielekeze kwenye mada husika. Ndugu zangu watanzania, baba yetu wa Taifa mwl Julius K Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa muda wa miaka 25. Kwa muda wote huo wa uongozi wake, nchi yetu ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo haikuja kutokea katika tawala zingine. Mfano wakati wa utawala wa Nyerere tuliona majaribio mawili ya mapinduzi yalioshindwa, hali iliyopelekea mzee wetu aamue kung'atuka mwenyewe kabla haja ng'atuliwa, maana kwa hali ya nchi ilivyokuwa kipindi kile bila shaka mwenyewe aliona kwamba asingeweza kumaliza miaka mingine mitano akiwa madarakani.

Lakini pia ukiachana na hayo ya mapinduzi pia kulikuwa na misuko suko mingine, mfano yale mauaji yaliosababisha waziri wa mambo ya ndani wa wakati ule mzee wetu mh Ally H Mwinyi kujiuzulu uwaziri. Pia kulikuwa na misuko suko mingine iliyopelekea kina mzee Kawawa, bibi Tito Mohammed na wengineo kufungwa jela. Lakini kama hiyo haitoshi, wapo waliamua kukimbia hata nchi na kwenda kuishi ughaibuni, mfano mzee wetu hayati Oscar Kambona na wengineo.

Hapo sijagusia ukosefu wa vitu muhimu nchini kama vile chakula, mafuta ya kupikia na ya taa, ukosefu wa madawa hospitalini, usafiri kuwa washida mpaka yakaletwa yale magari yalioitwa chai maharage, mzunguko wa pesa mtaani ukawa wa mdondo. Nguo, viatu, soksi, mafuta ya kupaka, sabuni navyo vikawa havipatikani.

Cha kushangaza alipoondoka mwl Nyerere na kuingia Mwinyi, hali ilibadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuna aliethubutu kuwaza tena mapinduzi, bidhaa zote muhimu zilipatikana kwa urahisi mitaani. Mzunguko wa pesa ukawa mkubwa, mitumba ya nguo, viatu, soksi kila kona, madawa yakawa mengi hospitalini mpaka watu wakaamua kufungua na zahanati zao. Pia hakuna aliewaza tena kukimbia nchi, isipokuwa tuliishuhudia wale waliokimbia utawala wa kwanza wanaaza kurejea katika utawala huu wa pili nk.

Hali hii aliyoanza nayo Mwinyi, naona imeendelea hadi leo. Je, ni kwanini misuko suko ilikuwa zaidi wakati wa awamu ya kwanza na sio awamu zingine? Je mwl Nyerere alihujumiwa au sera zake mwenyewe ndio zili muhujumu? Inamaana mzee Mwinyi kwa kutumia uwezo wake na cheo chake aliweza kulisuka vizuri jeshi letu na kurejesha utiifu wao kwa serikali yao na raisi wao? Je inamanaa Mwinyi hakuwa na maadui wa kuitingisha serikali yake, hadi kupelekea wengine kukimbia kama walivyokimbia awamu ya kwanza? Mwenye kujua zaidi sababu zilizopelekea mwl Nyerere kushindwa kuituliza hali, hadi kuamua kung'atuka anakaribishwa kutujuza. Asanteni sana kwa kunisoma?
Alikuwa dictator sana yule mzee...mpaka tufike stage tuwe tayari kuukabili ukweli wote ndiyo tutatoka hapo tulipo...
 
Yule si alikuwa anaongea maneno mengi sana huku utekelezaji hakuna,misemo na nahau zisizoisha..

Alikuwa hapendi ukosoaji na hataki changamoto za wasomi ndio maana hakutaka kusambaza elimu kwa watu wengi,aliwafanga watu wengi kuwa wajinga Ili awatawale kirahisi.

Miaka 25 ya utawala alichofanikiwa kikubwa ni kujenga utaifa na yeye binafsi kuwa muadilifu ila hakuna succession aliyofanya na aliondoka madarakani kutokana na Hali mbaya ya uchumi na sera zake mbovu za Uchumi..
Ulichokiona wewe ni misemo tu, ushabiki ni ugonjwa.
Kwanza kabisa tuna bahati kuwa rais wetu wa kwanza alikuwa J. K. Nyerere na tuna bahati kuwa aliamua kutumia siasa ya ujamaa.
Miaka ya 60, watu wengi Tanzania hawakuwa wasomi, hivyo angeweza kutorosha mali za taifa na kuhifadhi kwa manufaa yake, lakini hakufanya hivyo( Angalia nchi nyingine zilizofuata mfumo wa kibepari, viongozi wakuu walivyojimikisha mali.
Siasa ya ujamaa ndio iliyokuwezesha wewe Leo hii kupata maeneo sehemu mbalimbali Tanzania kwa bei rahisi au bure ( Kwasababu, ardhi ni mali ya serikali).
Pili, elimu wakati wa Nyerere ilikuwa inatolewa bure na kila mtu mwenye uwezo darasani alipata elimu( Kwahiyo, hakuwabania watu kupata elimu).
NYERERE alinusurika kupinduliwa mara mbili Kwasababu wakati huo, vuguvugu la mapinduzi lilitawala Afrika nzima.
Viongozi baada ya NYERERE hawakupata msukosuko wa mapinduzi Kwasababu wale waliojaribu kumpindua NYERERE hawakufanikiwa malengo yao( walikosa uungwaji mkono na mabepari. Na kisha waliishia pabaya). Hivyo wengine hawakuthubutu Kwasababu, wanajua kuwa mwisho wao utakuwa mbaya.
Jambo jingine ni kuwa kulifanyika maboresho ya jeshi.
NYERERE alikuwa anaona mbali hasa katika suala la matumizi ya rasilimali za taifa( dhahabu, mafuta, gesi, nk).
 
Back
Top Bottom