Forex sio utapeli kweli isipokuwa kuna watu wanasababisha ionekane ni utapeli pale wanapotapeli wengine kupitia forex, mfano hao wanaofundisha kuwatapeli wengine nakutokuwapa elimu sahihi.
pili inategemea movement za mabenki makubwa au watu wenye uwekezaji mkubwa!, hawa kuna muda wakiweza kuamua soko liende huku wanaweza.. isipokuwa hawatakiwi kufanya hivyo kwa njia zisizo halali hili lilishawahi kujitokeza na walipobainika hatua zilichukuliwa. hata baadhi ya ma broker hufanya hujuma na ndio maana unatakiwa ujua unafungua akaunti kwa aina gani ya broker na ikibainika amefanya hujuma ni rahisi kumchukulia hatua maana huwa wanaleseni!. haya yote yanahitaji elimu watu wengi hawana!.
kama ilivyo biashara yoyote forex nayo ipo hivyohivyo kuna upande wa faida na hasara!, jana tu kuna mtu kanihadithia kuwa amekula hasara kwenye biashara yake ya matikiti je nayo tuite ni utapeli..?
biashara nyingi za kisasa zinahitaji elimu kitu ambacho naona watu wengi hawana ama ni wavivu kwenye kutafuta elimu!. na watu waliofanikiwa huko sio watu wenye kupiga makelele hovyo wameridhika na wanachokipata na wanafocus na bashara zao..
structure ya forex ni lazima thamani ya fedha ishuke ama ipande na ndipo hapo kuna faida!, hata mtu alietunza fedha cash kwa muda fulani halafu akaja leo kuziuza anaweza kupata faida ama kula hasara kutokana na soko lilivyoathirika, vipi huo nao tuite utapeli..?