Superfly
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 985
- 2,066
Niende moja kwa moja kwenye hoja, siku za hivi karibuni kila ukiingia mitandaoni kama Instagram, YouTube, twitter, na hata hapa jamii forums, au ukiangalia channels nyingi za habari hapa Tanzania lazima ukutane na taarifa nyingi za mauaji ya kikatili au watu kujiua (suicide). Kwanini vyombo vya habari vinazidisha utoaji wa taarifa hizi?
Hawaoni kufanya hivi kunaleta athari hasi kwa jamii? Kwa mtazamo wangu naona utoaji wa mara kwa mara wa taarifa hizi unachochea zaidi matendo ya ukatili, uhalifu na mauaji katika jamiii...
Ningeshauri matukio kama haya yaachwe yashughulikiwe na mamlaka husika kama polisi, na Mahakama, na taarifa zihe zitolewe baada ya utatuzi wa tukio husika. Yaani tupewe mrejesho mtuhumiwa amechukuliwa hatua gani kali ambazo zitakua fundisho kwa wengine...
Karibuni kwa mawazo mengine wakuu, hii mnaona imekaaje?