Kwanini vyombo vingi vya habari siku hizi vinareport sana matukio ya Mauaji na Vifo?

Superfly

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
985
Reaction score
2,066
Niende moja kwa moja kwenye hoja, siku za hivi karibuni kila ukiingia mitandaoni kama Instagram, YouTube, twitter, na hata hapa jamii forums, au ukiangalia channels nyingi za habari hapa Tanzania lazima ukutane na taarifa nyingi za mauaji ya kikatili au watu kujiua (suicide). Kwanini vyombo vya habari vinazidisha utoaji wa taarifa hizi?

Hawaoni kufanya hivi kunaleta athari hasi kwa jamii? Kwa mtazamo wangu naona utoaji wa mara kwa mara wa taarifa hizi unachochea zaidi matendo ya ukatili, uhalifu na mauaji katika jamiii...

Ningeshauri matukio kama haya yaachwe yashughulikiwe na mamlaka husika kama polisi, na Mahakama, na taarifa zihe zitolewe baada ya utatuzi wa tukio husika. Yaani tupewe mrejesho mtuhumiwa amechukuliwa hatua gani kali ambazo zitakua fundisho kwa wengine...

Karibuni kwa mawazo mengine wakuu, hii mnaona imekaaje?
 
Vinatekekeza wajibu, kazi ya vyombo vya habari ni kuhabarisha. Sasa vikikaa kimya mauaji hayatatokea?

Vv
 
Vinatekekeza wajibu, kazi ya vyombo vya habari ni kuhabarisha. Sasa vikikaa kimya mauaji hayatatokea?

Vv
Mauaji yatatokea ndio, lakini kuna taarifa zingne znakua hazina uzito wa kuitwa taarifa ya Habari, na content zake zinalenga zaidi kutengeneza picha mbaya kwa jamii... Mfano taarifa za mauaji kuhusiana na wivu wa kimapenzi n.k
 
WE UNAJUA MAANA YA TAARIFA?
 
Kwa hiyo unataka wasireport

Wakae kimya

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…