Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Wasaidizi wake waliweza kuyatatua lni, na umejuaje kwamba matatizo ya Dangote hayawezi kutatuliwa na wasaidizi wake. Ni nani anajitoa ufahamu hapa?

Alitakiwa aje mashambani siku ile alipomaliza kumweka kaburini Magufuli, that's how urgent it was, and remains so, mpaka kesho kutwa.
Rais wa nchi sio sawa na admin wa group la whatsapp la shule ya msingi uliosoma.

Ni taasisi pana yenye ratiba pana na kile sehemu ni muhimu.
 
Kundi la wafanyabiashara haliwezi kuridhika hata ulibebe mgongoni for long term plan watu wakucheza nao ni hawa wachini na ndio mana JPM alipendwa sana na hawa watu wa chini, Top layer ni wachache sana unless mama awe hana mpango wa kurun for president 2025 kama ndivo basi atuachie katiba mpya ajilipue tu atuachie mzigo unaoleweka wa katiba, Kudeal na top layer kwa sana watu wengi wanaona kama anazingua afanye ziara mikoani akutane na wachini kabisa Magu hapa ali win sana
Mama anachofanya ni kizuri sana kwa national level shida tu kundi kubwa la watanzania bado ni masikini na wajinga kiasi kwamba mtangulizi wake alijichanganya na alionekana Rais wa makundi yote
Trust me Wananchi wengi waliji feel confident kwa JPM tofauti na Samia anaonekana kama wakishua fulani kutoka na type ya watu anao deal nao
Washauri kama kweli mama na nia ya kuendelea na Urais 2025 basi hii approach yake itampa ugumu sana kwenye ballot box ukizingatia pia pro Magu bado wapo kwenye system japo wame lay low ila wataibuka mana hata sasa wanaonekana kwenye hujuma kibao, Nafahamu power za mwenyekiti wa Ccm na Rais wa JMT ila trust me hii power inahitaji strong Inner circle ndo mana hata JPM amekuwa ousted
 
Fikra duni kabisa. Dunia nzima, viongozi wakuu wamekuwa wakikutana na wawekezaji wakubwa ili kuwavuta wakawekeze kwenye mataifa yao.

Karibia kila mwaka, Rais wa China anaenda Ulaya kuongea na wawekezaji wakubwa ili wawekeze China. Leo China ndiyo nchi inayoongoza kuvutia uwekezaji wa nje. Zaidi ya dola bilioni 80 huwekezwa nchini Chija kila mwaka kutoka mataifa ya kigeni hasa toka nchi za Ulaya, America na Asia. Na hicho ndicho kilichoinuabkwa kasi uchumi wa China.

Hakuna kitu chenye impact kubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa lolote na utengenezaji wa ajira kama uwekezaji mkubwa. Unapoongelea ukuaji wa uchumi, unaongelea uwekezaji.

Jukumu kubwa hili linaloamua juu ya maendeleo ya nchi, haliwezi kufanywa na Waziri pekee yake, ni jukumu la kiongozi mkuu wa nchi. Nchi haiwezi kujengwa kwa kodi za kukata kwenye vocha za simu. Mtu ananunua vocha ya sh 500 anakatwa kodi, ni upuuzi.
 
Sisi tunanyamaza maana tukisema tunaitwa sukuma gangkwa sasa praise team wamebaki wa Msoga na ndugu zao Chadema,ndo kutwa na mapambio Daah nchi hii mmmhh
Haturudishi wasukuma ikulu, mmejua kutufunza. Mama chapa kazi
 
Tatizo naliona kwa huyu Dangote. Yaani ni mgeni wa kudumu ikulu. Kwa Kikwete alifika, kwa magufuli alifika sasa kamuanza Samia. Bahati mbaya wote wanampokea utadhani ndo baba wa biashara nchini. Kiwanda chenyewe kimoja tu!

Kuna hadithi kwamba wanasiasa wanawinda kupewa shares kwenye kiwanda chake na ndo sababu aliahidiwa mengi nje ya sheria za nchi.
Fikra mfilisi.

Tanzania na Malaysia, miaka ya 1960, zote zilikuwa kwenye level sawa ya maendeleo. Kwa taarifa ya UNDP ya miaka michache iliyopita, kwa spidi, tunayoenda nayo sisi, Malaysia wakibakia walipo leo, Tanzania kuifikia itachukua miaka zaidi ya 250!!

Lakini Malaysia, mwekezaji yeyote anayewekeza Malaysia zaidi ya dola milioni 100, anapewa hadhi sawa na ya kiongozi wa nchi. Dangote amewekeza zaidi ya dola 700 milioni nchini Tanzania. Kwa uwekezaji huo, hata ingekuwa ni US au UK, akitaka kuonana na Rais, anaonana naye mara moja, tena mapema kuliko Rais wa Tanzania au Burundi.

Tatizo bado mna fikra primitive. Walioendelea wanaangalia positive impact ambayo mtu anaweza kuileta katika jamii, ndiyo uzito wa huyo mtu unavyoangaliwa. Kutokana na uwekezaji wake, uzito wa Dangote ni zaidi ya kiongozi wa baadhi ya nchi.
 
Kwani huko kwenye biashara hakuna wahusika; wewe vipi bhwana, mbona unabwatuka tu bila kutumia akili.

Wakulima wa nchi hii hawana matatizo makubwa kushinda hayo ya kiwanda cha Dangote, au wewe unaishi wapi?

Walipo wakulima wa nchi hii ndiko anakotakiwa rais awepo. Ndipo penye uhitaji mkubwa wa miongozo yake ili kuleta mabadiliko chanya kwa walio wengi haraka.
Waziri wa kilimo na naibu wake wapo vizuri sana na kuna mapinduzi makubwa yanaendelea ndani ya hiyo sekta.
 
Nyie wasukuma mnapata shida Sana aisee , maana mmekua watu wa kupinga tu sasa , sijui mnapigia chepuo nani aingie ikulu , Kama magufuli hayupo tena na hawezi kuwepo tena.
Kama VIP hameni Nchi Kama walivyofanya wale waliokua hawamuelewi magufuli .
Hiki kinachowatesa wasukuma ni tabia yao ya kuendekeza ukabila.
Tulionya lakini hawakusikia, Sasa ni kama wanatengwa na jamii.
Najua si wote lakini wengi walijiunga kwenye kikundi cha kusifu ujinga wowote. Haya ametangulia mtu wao bado wameng'an'ana kumtengenezea legacy. Walitakiwa watulie ,wsahaulike kuhusu mapambio yao kwa baba yao ili wakribishwe kwenye jamii tena.
 
Dangote ni mfanyabiashara mkubwa

Ova
Gazeti la Forbes liliwahi kuandika, 'Dangote amewekeza zaidi ya dola milioni 700 nchini Tanzania. Dangote anaweza kumpigia simu Rais wa Marekani au Waziri Mkuu wa Uingereza hata saa 8 usiku, wakiambiwa ni Dangote aliyepiga, wataamka kwenda kupokea simu yake, huyo sasa anadharauliwa na utawala wa Magufuli nchini Tanzania'. Ni wakati ule Dangote alipoamua kuondoa kiwanda chake toka Tanzania. Marehemu akahaha sana, akamwalika ikulu na kumbembeleleza abakie nchini.

Siyo rahisi kumpata mwekezaji mkubwa kama Dangote nchini mwako. Ikumbukwe kuwa Dangote, kitega uchumi chake, ndiyo uwekezaji mkubwa wa mara moja kuliko uwekezaji mwingine wowote, na ndiye mwekezaji mkubwa wa mwisho kuwekeza Tanzania. Baada ya Dangote, hakuna mwekezaji mwingine aliyekuja Tanzania.
 
EeenHeee,

Utalia sana mkuu 'Zygot', huu ni mwanzo tu!

Hapana, mimi sitaki wakulima mashuhuri pekee ndio waende ikulu. Mimi nasubiri awafuate walipo; hasa hao hohehahe wenzetu wanaolanguliwa mazao yao na nisikie mipango yake kuwainua ikoje.

Mpaka hapo atakapofanya hivyo, nitaendelea kuungana nawe na kuililia Tanzania inayoandaliwa kurudi kwenye uchuuzi.
Hatari.
Jiwe alipofanya mikutano kama hii watu walibaki kusifu na kuabudu, eti leo tunaikosoa ccm kisa siyo jiwe sasa ila ni mama.
Tuumalize unafki huu watanzania.
 
Sisi tunanyamaza maana tukisema tunaitwa sukuma gangkwa sasa praise team wamebaki wa Msoga na ndugu zao Chadema,ndo kutwa na mapambio Daah nchi hii mmmhh
Wakati unafikiria kusema lakini unaamua kunyamaza kwa hofu ya kuitwa Sukuma Gang, je ulishawahi kusema wakati Jiwe akikutana na akina Rostam Aziz au hata huyo Dangote huko huko Ikulu?!
 
Mbona kipindi kile akina Rostam wameenda kuonana na ile maiti ya chato hamkuyasema haya

Mwacheni mama aipeleke nchi mahala salama kutoka kwenye ile diversion aliyokuwa anatupeleka bwana Mayanga/majanga
Walionana na maiti!!???
hebu kuwa na adabu ama tutakuchapa kwa sentesi ngumu
 
Kuna watu sijui hata kama wanasoma wanachoandika, Kiwanda kimoja ndio chenje direct investment of 750 Million dollar hiyo unaona ndogo kwa hiyo wewe uko interested na quantity au quality ukataka kuturudisha enzi zile tunasema viwanda vipya alfu 8000 bila kusema thamani ya uwekezaji wakaja kusema hata cherehani 2 kiwanda tunatakiwa tuwe serious.

Dangote ni tajiri number moja Africa ukimvuta yeye wengine watakuja kirahisi tu sababu kama mkuu kawekeza Tanzania basi uwekezaji salama watakuja. Kuna watu wana pesa huyu unataka apokelewe na waziri mtu utajiri wake kama budget nzima ya mwaka ya Tanzania? budget yenyewe ya kwetu kuna mikopo humo na misaada. Vuta papa samaki wadogo watakuja tu, kuna watu kabla ya kuja kuwekeza wanatizama nani na nani yuko pale wanakuja. Kuna mtu alishawahi kuniambia ukiona sehemu Roman cathoilic wamenunua ardhi basi na wewe nenda kanunue jirani utafaidikia.
 
EeenHeee,

Utalia sana mkuu 'Zygot', huu ni mwanzo tu!

Hapana, mimi sitaki wakulima mashuhuri pekee ndio waende ikulu. Mimi nasubiri awafuate walipo; hasa hao hohehahe wenzetu wanaolanguliwa mazao yao na nisikie mipango yake kuwainua ikoje.

Mpaka hapo atakapofanya hivyo, nitaendelea kuungana nawe na kuililia Tanzania inayoandaliwa kurudi kwenye uchuuzi.
Ulikuwa na mawazo sawa na haya wakati Magu akikutana na akina Rostam au hata huyo Dangote hapo Ikulu?!

Unaweza kueleza hapa utofauti wa Dangote aliyekuwa amekutana na Magu na Dangote aliyekutana na SSH ili tuamini Dangote huyu anayekutana na SSH ni mwando tu wa kuturudisha kwenye uchuuzi lakini Dangote yule wa Magu alikuwa ni wa kutupeleka kwenye industrial nation!

Magu.png


Hapo juu ni Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise!!

Haya sasa... tofauti ya ukutanaji huu wa sasa ni ipi ukilinganisha na ule wa zamani hadi uone huu wa sasa unataka kuturudisha kwenye uchuuzi?!
 
Back
Top Bottom