Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Hapana! Hata waganda walisema haifai kumuacha Amin muuaji na kumfuata Obote muuaji tena. Huyu itakuwa kama kombolela: namtilia msahaka tangu uzoefu hadi elimu yake, imeungwa saaana!
Bora elimu ya huyu kuliko yule aliyeungaunga kutoka ualimu hadi phd feki
 
Tena anaowakaribisha ni wa Nigeria. Hatijasikia akiwahitaji wafanyabiashara wa Tanzania.
Walichofanywa wafanyabiashara wa tz hii miaka 5 ya muovu hata wana hamu tena? Wanahitaji muda wajipange upya, maana muovu aliwafanya kitu mbaya sana, wengi iliwapasa hata kuuza assets zao na kukimbia nchi yao. Yupo wapi Manji leo hii? Mtz aliyeajiri maelfu ya watz, muovu kwa mabifu yake ya kishamba akamsambaratisha
 
Mbona kipindi kile akina Rostam wameenda kuonana na ile maiti ya chato hamkuyasema haya

Mwacheni mama aipeleke nchi mahala salama kutoka kwenye ile diversion aliyokuwa anatupeleka bwana Mayanga/majanga
Aisee umetumia kauli ngumu
 
Chief hongera kwa ufafanuzi ...

Watanzania tulio wengi ni wajinga mno yanapokuja masuala mazima ya uwekezaji, yaani kila kitu tunaleta hisia hatuwazi critically

Wengi hawajui kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na wawekezaji wakubwa wanaozalisha ajira nyingi

Just imagine kampuni km voda ajira ilizozalisha tokea kuanzishwa kwake hpa nchini include ajira indirect km za uwakala m pesa

Sasa imagine kampuni km voda kwenye sekta tofauti tofauti ziwe 2000 ni watu wangapi wataajiriwa?

Ifikie kipindi tuache kuwa emotional na kuona kila anaetaka kuwekeza nchini ni mwizi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
hapana kama mliwahi kuita watendaji wa vijiji ikulu inakuaje mama anaita wafanyabiashara wanaolipa kodi ili ilipwe mishahara ,mshangae!
 
Halafu kwa miaka kadhaa sasa wanigeria wamevamia Tanzania eti investors...
Haijalishi awe mnigeria,mghana au mcameroon km ana uwezo wa kuwekeza na kuzalisha ajira za kutosha tunapaswa kumkaribisha kwa bashasha zote na sio kwa kejeli km unazoziandika hpa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Unampangia rais nani wa kukutana naye Ikulu?

Kwa kigezo gani?

Kama hupendi anaokutana nao Ikulu gombea urais upange nani aje Ikulu.

Rais ndiye mkuu wa nchi, hivyo, mikutano na wawekezaji wakubwa wanaoweza kubadilisha uzalishaji inamhusu.

Hili si jambo la Tanzania tu, linafanyika dunia nzima.

Au hamjui hilo?
 
Tatizo naliona kwa huyu Dangote. Yaani ni mgeni wa kudumu ikulu. Kwa Kikwete alifika, kwa magufuli alifika sasa kamuanza Samia. Bahati mbaya wote wanampokea utadhani ndo baba wa biashara nchini. Kiwanda chenyewe kimoja tu!

Kuna hadithi kwamba wanasiasa wanawinda kupewa shares kwenye kiwanda chake na ndo sababu aliahidiwa mengi nje ya sheria za nchi.
Dangote anasikilizwa dunia nzima.

Utawala uliopita uliharibu mahusiano naye. Huko nje akawa anaulizwa Tanzania vipi? Hakuonesha kutoa maneno mazuri, wawekezaji wengi sana wakasema kama Tanzania pamemshinda Dangote, sisi hatutii mguu.

Sasa hivi anaonekana kurudisha majeshi na kuisema vizuri Tanzania. Tegemea kuona wawekezaji wengi wa kimataifa kuanza kurudi.

Dangote qna uzito huo katika biasharq za Africa na dunia.

Ndiyo maana unamuona ni mtu wa kuongea na marais sana.

Na hili jambo si Tanzania tu. Sehemu nyingi anapofanya biashara ana effect hiyo.
 
Fuatilia changamoto anazopitia Dangote kwenye kiwanda chake cha saruji (cement) huko mtwara, kuna somo linaitwa mjasiriamali na yanayomzunguka 'the entrepreneur and his environment ' tumepitia kwenye sera zisizo tabirika (policy uncertainty) huwezi kupanga namna ya kukuza biashara kwa sera ambazo hazina muelekeo 'you can not plan business growth with policy uncertainty' wafanya biashara wengi waliumizwa na hicho kikosi chenu cha 'task force ' kazi ya ziada inahitajika kurudisha imani ya wawekezaji na wafanya biashara na ndicho anakifa fanya Mama
 
Back
Top Bottom