Kwanini waislamu hawasherehekei Krismasi ila husherekea mwaka mpya?

je huwa mnasheherekea mwaka mpya..?

Ndio mkuu huwa tunasherehekea
Na sherehe zetu ni mbili tu
Ya kwanza ni baada ya mfungo wa Ramadhan na sherehe ya pili ambayo ndio ya kufungia mwaka ni Eid kubwa ambapo ni wakati wa Hijja, baada ya Hijja Eid na mwaka mpya unaingia na mwezi wa kwanza huitwa Muharram



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mlipotoka 1440 kuingia 1441 mlisheherekea?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio Mkuu tulisherehekea Eid kubwa ambayo ni baada tu ya Hijja
Hapo ndio mwaka mpya unaingia
Tuna sherehe mbili tu ambayo ni baada ya Ramadhan na tunafunga mwaka kwa kuhiji na ndio sherehe kubwa
Ukiona tunasherehekea baada ya Hijja ndio mwaka mpya unaingia Mkuu
Nafikiri umenielewa vizuri hapo


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Nimekwambia ulete ushahidi kwa mujibu wa dini ya uislamu kuwa waislamu wanasherehekea mwaka mpya au chochote kile kilicho kinyume na dini ya.
kwani kwa mfano,kama kuna mchungaji kakamatwa akiwanga,wakristo watahesabika ni wachawi,au basi tutazame kuhusu yale yalozuka katika kanisa la Anglikan,na ule nao ni ukristo.
Nabaki pale pale kwa juzi,lete ushahidi kwa mujibu wa uislamu kwamba waislamu wanasherehekea mwaka mpya.
 
Kwa mujibu wa uislamu ni haramu kusherehekea sikukuu wanazoziita za kikafiri.
1. Birthday.
2. Mwaka mpya.
3. Noel (Krismasi).
4. Valentine.
5. Pasaka.

.
Wewe V.U haki naapa katika hizo tano tatu unazisherehekea kila zinapowadia ukitoa Noel na Pasaka unabisha?
 
Sniper birthday yako husherehekeagi?
 
Sujawahi mkuu
Kwa sababu sio utamaduni wetu
Tangu nimezaliwa sijawahi kufanyiwa wala kusherehekea birthday
Mkuu kila siku ni birthday kama umeamka salama na kumshukuru Mungu



Sent from my iPhone using Tapatalk
Unaungana na mimi kwamba waislamu karibu wote isipokuwa wachache Tanzania husherehekea siku zao za kuzaliwa?
 
Haya yote ni Mabalaa ya Masufi.
Hawa watu wapo kwenye sikukuu yao ati na Nyie mnaandaa vitamasha vyenu sijui vya waimba Kaswida siku zote mlikuwa wapi masiandae mpaka maubirie Mwaka Mpya?
 
Unaungana na mimi kwamba waislamu karibu wote isipokuwa wachache Tanzania husherehekea siku zao za kuzaliwa?

Wapo wengi tu
Nasema hivyo kwa sababu nimeona ila kwa takwimu sijui na siwezi kutoa ushahidi huo
Dini ni kufuata yaliokubaliwa na kuacha yaliyokatazwa ni hilo tu
Wanaofanya yao ni wao na kila mtu atabeba thawabu zake na dhambi zake Mkuu



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Sasa kwa nini musiite hiyo sikukuu mwaka mpya sasa, mnaita majina ya kiarabu
 
Wasipokuelewa na hapa basi ile aya inayosema "hawatokuwa radhi mayahudi na manaswala hadi mfate....."
 
Sasa kwa nini musiite hiyo sikukuu mwaka mpya sasa, mnaita majina ya kiarabu

Mkuu ukiangalia majina na maneno hata neno Swahili ni la kiarabu
Maneno mengi sana ya kiswahili ni ya kiarabu au kihindi
Hata Xmas sio la kiswahili Mkuu




Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…