Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya Darasa la Saba?

uko sahihi
 
Ndio nilitaka kukisema hiki ila umenisemea tayari.
Kwa mfano mimi shule ya msingi masomo ya sayansi nilikuwa siyapendi na nilikuwa mdhaifu lakini nilivyofika sekondari nikawa mtabe kwenye masomo ya sayansi na ndio yanayonipa msosi hii leo.
Mimi wapo ninaowajua walikuwa hatari sana katika somo la sayansi primary na mpaka secondary wakawa bado wanatesa.

Vp wanao-fail masomo ya sayansi katika mtihani wa mchuyo wa kidato cha pili na kuambiwa kwenye mchepuo wa arts? Ina maana licha ya ku-fail kwako wanaweza kubadilika huko mbeleni na kufanya vema katika matokeo ya kidato cha nne?...
 
Ndio hvyo.
Kufeli kwa mwanafunzi hutegemea condition tu ya wakati huo wa mtihani sio kitu permanent.
Kufaulu mtihani hutegemea vitu vifuatavyo
1.Maandalizi wakati huo wa mtihani
2.Confidence wakati huo wa mtihani,mwanafunzi anaweza kujiandaa vizuri na kuelewa concepts zote lakini akakosa confidence akafeli.
3.Mood ya wakati huo wa mtihani,mwanafunzi anaweza akajiandaa vizuri lakini akashindwa kufaulu kutokana na stress alizonazo wakati huo.
Wewe hujawahi kuona mwanafunzi anafeli darasa la 7 kisha anafeli form 4 Lakini anapasua form 6 na kuingia chuo kikuu.
Halafu mwanafunzi mwingine anafaulu darasa la 7,anafaulu form 4 Lakini anafeli form 6 anakwama kuingia chuo kikuu.
Wewe unafikiri sababu ni nini?
 
Nakazia
 
Sawa mkuu...
 
Mkuu, kwa maelezo yote haya uliyoyatoa ina maana basi wanafunzi woooote wa secondary wasome masomo sawa mpaka form 4. Hii ndio mantiki niliyoipata katika huu ufafanuzi wako mrefu.
 
ahsante sana
 
Kabla hujaamua hivyo inabidi kwanza ujiulize lengo kuu la elimu katika maisha ya binadamu ni nini hasa? Kama ni kumpatia ajira tu basi uko sahihi. Specialization zianze mapema kadri inavyowezekana.
Mkuu, lengo la elimu hapa Afrika ni lipi haswa katika ya kumpatia mtu ajira na kumpa maarifa ya kimaisha?
 
Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza "directly" na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya darasa la saba na sio kusubiri mpaka afike kidato cha pili?



Umesahau Bookkeeping na Commerce mkuu....au hawa tuachane nao???
 
(Education Curriculum ) me nadhan mtaala wa elimu upo sawa Ila unahitaji marekebisho makubwa yanayoendana na mahitaji
 
Sawa mkuu upo sahihi. Tunaomba mchango wako zaidi kama hutojali ndugu yangu ili na sisi tuzidi kujifunza
Ninachotaka kusema na uelewa wangu juu ya maendeleo na elimu mwanzon nchi nyingi za ulaya walikuwa Wana community centered education curriculum hapa ni kwamba mwanafunzi anasoma apate elimu aisaidie jamii inayomzungunguka later on wakaboresha ili kuruhusu ubunifu katika ujuzi wakahama kwenda kwa learner centered curriculum ambapo tunasema kuwa Kila mtoto anazaliwa na kipawa chake kwa hio kazi ya mwalimu ni kugundua kuwa huyu mtoto interest yake ipo katika nn na kuhakikisha una msubject huko ili kukuza kipaji chake na ndio maana unaona innovation katika kazi zao
 
Turudi katika maada mtoto anatakiwa asome masomo mbali mbali ambayo yatamsaidia kuwa na atleast basic knowladge ili kupata hao wataalam wanasayansi inabidi pawe na uwekezaji mkubwa katika elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka vyuoni pia waencourage zaidi learner centered curriculum ambayo ni very expensive
 
Turudi katika maada mtoto anatakiwa asome masomo mbali mbali ambayo yatamsaidia kuwa na atleast basic knowladge
Sawa mkuu. Pia nimependeza namna ulivyotumia hilo neno "at least basic knowledge" bila shaka ulikuwa una maana kwamba sio kila knowledge inapatikana shuleni bali ni ile ya msingi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…