Kwanini wanaompokea Rais Samia huko Manyara wametokea Dar es Salaam?

Kwanini wanaompokea Rais Samia huko Manyara wametokea Dar es Salaam?

Nimekuelewa mkuu, hata kule India niliona team ya mapokezi pindi aliposhuka kwenye Ndege, miongoni alikuwepo January Makamba.

Hata hili nalo ni la kawaida!
Timu yenyewe hii hapa
Screenshot_2023-10-12-12-13-58-1.png
 
Natambua kwamba Mh Rais Samia Ph.D, anaanza ziara ya kikazi Mkoani Manyara, hongera kwake na kwa Wenyeji wake.

Lakini cha kushangaza kwenye ziara hii ni kitendo cha Rais kupokelewa na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam ! jambo hili kwangu ni geni mno, Inakuwaje Rais apokelewe na wakazi wa Dar, Je Manyarq haina watu?

Kwamba Mh Rais naye ameamua kusomba Watu kama anavyofanya Chongolo ili kuongeza Uwingi wa watu ?

Kumbe hata huelewi wanazikimbilia fursa za kuonana na mama?

Watu wakielewa tu mama ana ziara ya huku au kule, wanawahi mapema kabisa, hata mimi nikisikia na nikiwa na jambo langu nawahi kabisa, huko ndiyo pa kumpata kiwepesi.

Unafikiri ni wepesi kupata appointment Ikulu Dodoma au Dar? Utasota, tena unaweza kufanya appointment Dar ukapigiwa siku moja au mbili kabla ukaulizwa unaweza kwenda Mtwara, huko unaweza kumpata keshokutwa tutakuwekea slot yako kabla ziara hazijaanza. Ukiweza unakwenda au unawaambia mie ntasubiri mpaka nimpate hapahapa tu.

Ziara hizo zina faida sana. Mwenyewe saa nyingine anasangaa, akikuona anakuuliza, na wewe upo hapa? Hapana mama nimekuja kukuona wewe, una shida gani? Unamwagika hapo kwa raha zao.

Kitu nnachompendea mama Samia, hajawahi kukataa shida au ombi la mtu hata iweje, labda liwe halipo kabisa kwenye uwezo wake, nalo pia atakwambia ukweli, hili inabidi nilifatilie hivi na hivi, lakini utatafutwa. Basi ujuwe kweli atalifanyia kazi tena wakati huohuo, hana ngoja baadae huyo.

Mama samia Mweyezi Mungu amzidishie hekima maarifa na upendo alionao kwa Tanzania.

Jinsi anavyochapa kazi huyu mama, mpaka vijana wenyewe wanashika kiuno, muulizeni Zuhura Yunus, anaipatapata. Mie nadhani huyu mama Ma shaa Allah ni nusu robot.
 
Kwamba ili kusaidiwa nchi hii ni mpaka uonane na Rais ?
Sikiliza kijana, hakuna mtu anayetafutwa kuonana na watu Tanzania hii zaidi ya Rais. Na hii si Tanzania tu, karibia nchi zote duniani ni hivyohivyo.

Watu wana mambo yao mbalimbali, usifikiri wewe kwa kuwa yako yanaweza kuishia hukuhuku mitaani basi wote ni hivyo hivyo.
 
Cha kushangaza mnapompokea huyo Rais Dar mbona wa mikoani hamuwaaliki ?
Huwezi ukaona kwa kuwa Dar Tu pekee yake ina wakazi zaidi ya milioni 6 ambapo kutokana na msongamano mkubwa siyo rahisi kumuona kila mtu aliyepo eneo la Tukio.Alipo Rais wetu nasi tupo hapo hapo.
 
Natambua kwamba Rais Samia Ph.D, anaanza ziara ya kikazi Mkoani Manyara, hongera kwake na kwa Wenyeji wake...
Rais anatakiwa kupima kukubaliwa kwakwe kwa njia ya mapokezi, uungwaji mkono pamoja na kujisikia yuko nyumbani popote aendapo juu ardhi hii ya Tanzani!

Kupokelewa na wageni kama yeye alivyoenda ugenini sio ustaarabu, na hata hao wanaotangulia kumpokea ilipaswa wasifanye hivyo!

Basi na ngoma waimbe wao, na risala wasome wao, kero waziseme wao, na mbunge wawalete wabunge wao,
Kwa taratibu za mfumo wa maisha ya mtanzania sio uungwana kufika ugenini nakuanza kuingilia mfumo wa nyumba ya ugenini maana ni ushamba kama sio kukosa staha!

Mama ondoa that gang!
 
Sikiliza kijana, hakuna mtu anayetafutwa kuonana na watu Tanzania hii zaidi ya Rais. Na hii si Tanzania tu, karibia nchi zote dunuani ni hivyohivyo.

Watu wana mambo yao mbalimbali, usifikiri wewe kwa kuwa yako yanaweza kuishia hukuhuku mitaani basi wote ni hivyo hivyo.
Alafu wee Faza wewe!
 
Back
Top Bottom