Natambua kwamba Mh Rais Samia Ph.D, anaanza ziara ya kikazi Mkoani Manyara, hongera kwake na kwa Wenyeji wake.
Lakini cha kushangaza kwenye ziara hii ni kitendo cha Rais kupokelewa na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam ! jambo hili kwangu ni geni mno, Inakuwaje Rais apokelewe na wakazi wa Dar, Je Manyarq haina watu?
Kwamba Mh Rais naye ameamua kusomba Watu kama anavyofanya Chongolo ili kuongeza Uwingi wa watu ?
Kumbe hata huelewi wanazikimbilia fursa za kuonana na mama?
Watu wakielewa tu mama ana ziara ya huku au kule, wanawahi mapema kabisa, hata mimi nikisikia na nikiwa na jambo langu nawahi kabisa, huko ndiyo pa kumpata kiwepesi.
Unafikiri ni wepesi kupata appointment Ikulu Dodoma au Dar? Utasota, tena unaweza kufanya appointment Dar ukapigiwa siku moja au mbili kabla ukaulizwa unaweza kwenda Mtwara, huko unaweza kumpata keshokutwa tutakuwekea slot yako kabla ziara hazijaanza. Ukiweza unakwenda au unawaambia mie ntasubiri mpaka nimpate hapahapa tu.
Ziara hizo zina faida sana. Mwenyewe saa nyingine anasangaa, akikuona anakuuliza, na wewe upo hapa? Hapana mama nimekuja kukuona wewe, una shida gani? Unamwagika hapo kwa raha zao.
Kitu nnachompendea mama Samia, hajawahi kukataa shida au ombi la mtu hata iweje, labda liwe halipo kabisa kwenye uwezo wake, nalo pia atakwambia ukweli, hili inabidi nilifatilie hivi na hivi, lakini utatafutwa. Basi ujuwe kweli atalifanyia kazi tena wakati huohuo, hana ngoja baadae huyo.
Mama samia Mweyezi Mungu amzidishie hekima maarifa na upendo alionao kwa Tanzania.
Jinsi anavyochapa kazi huyu mama, mpaka vijana wenyewe wanashika kiuno, muulizeni Zuhura Yunus, anaipatapata. Mie nadhani huyu mama Ma shaa Allah ni nusu robot.