Kwanini wanaoruhusiwa kuchinja ni Waislamu peke yao?

Kwanini wanaoruhusiwa kuchinja ni Waislamu peke yao?

Si kwamba Wakristo awaruhusiwi kuchinja, Waislamu awali nyama isiyotamkiwa maneno ya kuchinja, Wakristo hawana shida wao wanaamini
wapo salama kupitia kuombea chakula. but kibiashara imeshaurika achinje Muislamu Ili pasiwepo na kisingizio cha kutokula.
Hata mfumo wa uchinjaji kwa kutumia mashine umetengenezwa ni automatic unamuelekeza mnyama uelekeo wa Kaskazini na pia kisu kimeandikwa maneno ya kuchinja.
Sema wakristo hawana elimu ya kuchinja
 
Afu wakija huchinja kwa jina la nani? Wanamkabidhi Mungu yupi huyo mnyama wako?
Kuchinja kuna utaratibu wake kwanza uombe ruksa kwa Mwenyezi Mungu na kunauelekeo wa kumuweke myama,pili kunajinsi ya kupitisha kisu,yaani hutakiwi uchinje kama unakata mti,ili usimpe maumivu sana mnyama unayemchinja,unashauliwa kisu kianzie chini kwenda juu na kiwe kikali
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Hao Wakristo wanaopeleka kwa Waislamu hawaijui dini Yao inasema Nini kuhusu kuchinja mnyama.
Mkristo anaejua dini analo andiko linalomuelekwza namna ya kuchinja mnyama Wake.
 
Idhini ipi? Kabla ya uislamu nani alikuwa anachinja hivyo vitowewo?
Ndiyo maana tunawaambiaga Uisilamu kaanza nao Baba yetu Adamu kila kitu alipewa utaratibu na Mwenyezi Mungu,kuanzia kutembe,kulala,kujisaidia,kula kujamiana.kila kitu sema mitume kazi yao ni kutukumbusha pale tunaposahau
 
Hao Wakristo wanaopeleka kwa Waislamu hawaijui dini Yao inasema Nini kuhusu kuchinja mnyama.
Mkristo anaejua dini analo andiko linalomuelekwza namna ya kuchinja mnyama Wake.
Ebu tupe andiko lako,na nakuuliza kilichojifia chenyewe au kikapigwa na mnyama mwenzake kikafa pasipo kuchinjwa ni harali kuliwa kwa mkristo?
 
Yawezekana kwao kiboko sio mnyama bali yuko kundi la samaki fuatilia vizuri
Wanyama wengine ni hatari huwezi kumchinja kama unavyochinja kuku,mbona atakuchinja wewe,lakini Mwenyezi Mungu Mkalimu alishatuwekea utaratibu
 
Kuna siku nilimtembelea dada yangu pale Riverside-ubungo,akadaka kuku akawa anamchinja..... kumbe Kuna jamaa pale mvaa vipedo aliongea sana mpaka nikatoka nikamwambia kama ni mbona unaingilia maisha ya watu na kuwapangia Cha kufanya? Ooh hiyo ni kifuru, nikamuuliza maswali kadhaa nikaona anaanza kuniletea story za dini yake nikamcheka na kumuona mjinga sana...... yaani unalazimisha watu wafanye kitu kufuata dini yako?
 
Kuna siku katika mji fulani mnyama kiboko aliingia mtaani ikabidi mtu wa wanyapori aitwe akampige risasi, hilo lilipofanyika umati wa watu ulifurika kugawana nyama na hakuna aliyetaka kuuliza mchinjaji nani🙂
🤣🤣🤣
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Makobazi wengi wafuga majini.Waende wakachinje mdudu kitimoto waipate fresh.
 
Kuna siku nilimtembelea dada yangu pale Riverside-ubungo,akadaka kuku akawa anamchinja..... kumbe Kuna jamaa pale mvaa vipedo aliongea sana mpaka nikatoka nikamwambia kama ni mbona unaingilia maisha ya watu na kuwapangia Cha kufanya? Ooh hiyo ni kifuru, nikamuuliza maswali kadhaa nikaona anaanza kuniletea story za dini yake nikamcheka na kumuona mjinga sana...... yaani unalazimisha watu wafanye kitu kufuata dini yako?
Hapana alikuwa anakupa utaratibu unavyotakiwa,inawezekana kuku wako lakini wewe siyo uliyemuumba inabidi umuombe idhini aliyemuumba,vilevile aliyemumba ndiyo aliyetupa utaratibu wa kuchinja,
 
Hapana alikuwa anakupa utaratibu unavyotakiwa,inawezekana kuku wako lakini wewe siyo uliyemuuba inabidi umuombe idhini aliyemuumba,vilevile aliyemumba ndiyo aliyetupa utaratibu wa kuchinja,
Huo ujinga,siyo kila unachoamini wewe lazima Kila mtu aamini....... Muslim kuingia hata chooni lazima utangulize mguu wa kushoto ....Kila mtu abaki na chake na tusipangiane
 
Siyo Kwa wote,mwanangu mwenyewe Abdi kila siku tunagonga naye kitimoto na ni Swala 5 hadi anasigda........
Iko hivi kuna Uisilamu na Muisilamu,Uisilamu unabaki kama Dini isiyokuwa na Mapungufu,lakini huyu Muisilamu anamapungufu yake na sisi haturuhusiwi kumuhukumu ipo siku atamludia Mola wake akafanya toba,na sisi hatujui kesho yetu itakuwaje,tunaweza kuwa wakosefu zaidi yake
 
Huo ujinga,siyo kila unachoamini wewe lazima Kila mtu aamini....... Muslim kuingia hata chooni lazima utangulize mguu wa kushoto ....Kila mtu abaki na chake na tusipangiane
Ndiyo Maana Uisilamu haumlazimishi mtu kuifuata Dini ya Mwenyezi Mungu,bali ni hiari yake mwenyewe
 
Iko hivi kuna Uisilamu na Muisilamu,Uisilamu unabaki kama Dini isiyokuwa na Mapungufu,lakini huyu Muisilamu anamapungufu yake na sisi haturuhusiwi kumuhukumu ipo siku atamludia Mola wake akafanya toba,na sisi hatujui kesho yetu itakuwaje,tunawekuwa wakosefu zaidi yake
Inshallah
 
Hawa jamaa bhana kuanzia uchinjaji,uvaaji,,lugha na vyakula mfano alkasusi vyote ni utambulisho wao halafu wanadai kila mtu alizaliwa muislamu yaani ni usanii uliopitiliza!tuwaachie tu wachinje wasife njaa.
 
Back
Top Bottom