Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
A hsante Hoyce ila nakumbuka nilisikia kwenye BBC pia lakini hakuna neno uzuri sasa wengi tunakubaliana na kukumbuka majibu ya JK
 
Mtu kama hajui chanzo cha umasikini wetu je anawajua adui zetu wakubwa?
Next time tusichague raus mcheza ngoma.
 
Kwa ushauri tu mr. President. Umaskini wa TZ unatokana na mfumo mbovu tuliourithi toka kwa wakoloni na kuishi nao mpaka leo.
1. Mfumo wetu wa elimu ni tegemezi usio endelevu, tunazalisha watwana badala ya wataalamu (Miaka 50 toka uhuru hakuna kitu cha kitaalam kilichovumbuliwa TZ, hata kiwanda cha kuunganisha redio kimetushinda). Wakati sisi tunazalisha vibarua wao wanazalisha wataalamu.
Hii imepelekea kubaki kuwa ombaomba wa utaalam.
2. Uzalendo. Uzalendo umekuwa ni wimbo tu wa majukwaani wakati mfumo umetengenezwa kupinga uzalendo. Wananchi hawatambui wajibu wao kwa nchi yao. Wizi wa rasilimali, ukwepaji kodi, uharibifu wa miundombinu, mauaji, na uovu aina aina ni zao la kuteketea kwa uzalendo.
3. Uongozi mbovu. Hili ni zao la uoza huo hapo juu. Viongozi waliotokana na mfumo wa elimu ya kitumwa daima watafikiri kitumwatumwa tu. Kwamba jambo lolote haliwezi kwenda mpaka ufadhili. Kwao wao hata kusafisha mitaa wanayoishi na kuzoa taka tu, watangojea fedha za wafadhili (utumwa wa dhahiri).
4. Taifa vivu. Uongozi goigoi huzaa serikali zezeta na mwisho hupelekea taifa vivu. Tunayo mifano inayoishi jinsi watendaji serikalini wanavyoteketeza muda wa kazi kwa kupiga soga, kunywa chai, warsha zisizo na mwisho n.k. Kwa wastani hatufanyi kazi. Vijana kushinda vijiweni kucheza kamari (pool tables), watu wazima ni bao na zumna muda wa kazi. Kila mvivu utakayemkuta na kumuuliza kwa nini yuko hapo, lawama zitaenda kwa serikali kutowapa ajira (taifa la watumwa kusubiri bwana awapangie kazi kwa mjeledi).
5. Nchi kujaa watenda kazi wasio na ujuzi (unskilled labourers).

Kazi kwako JK na timu yako, huu ni ushauri wa bure.
 
KWA NINI WATANZANIA WENGI NI MASKINI?

Sijawahi kumwona Mtanzania kwa wakati wowote ule ameondokana na umaskini, umaskini ambao sasa ni mkubwa mno na unakaribia kutudidimiza.

Binafsi nauchukulia umaskini kama kukosekana kwa mahitaji ya lazima ya kila siku kwa mwanadamu: malazi mazuri, chakula bora (ambavyo hivyo vyote vinapatikana kama binadamu huyo huyo anakuwa na njia ya kujipatia kipato) na uongozi bora wa haki unaofuata sheria (ili huduma mhimu za jamii: shule, hospitali, barabara, maji salama nk vipatikane).

Watanzania wengi tu maskini wa kutupa kwa sababu tunagharimia mno uendeshaji wa kila siku wa serikali yetu (isivyokuwa lazima).

Wanasiasa ndio watoa maamuzi hata ya kitaalauma hata kama si wana taaluma husika.

Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana. Kihio kutoka A. Kusini analipwa mamilioni ya pesa hata kama utendaji wake ni mbovu. Mfano NET GROUP SOLUTION, wanaishi maisha ambayo hata kwao hawana. Na wazawa waliokuwa nao wanajilipa pesa ambayo haina mfano.

Wanasiasa wanajilipa pesa nyingi ukilinganisha na wataalamu waliosomea taaluma mbali mbali.

Tatizo la wanataaluma kutothaminiwa limewasukuma baadhi yao kujiingiza ktk siasa. Hapa ndo kichekesho kinatokea. Mwana taaluma huyo huyo akiwa nje ya siasa anakuwa critic wa governing system! Kuna prof. mmoja ambaye ni waziri kwa sasa wakati akiwa chuoni alikuwa ni mtu ambaye aliponda jinsi nchi yetu inavyoongozwa shaghala baghala, alivyoukwaa ubunge huko kwao akateuliwa ktk baraza la mawaziri.. nasikia alikwenda kuwashukuru waliompigia kura kwa dege la jeshi kwa gharama ya serikali. Wako wengi wa aina hiyo.

Elimu ya mafunzo ya darasani na hali halisi iliyoko nje katika jamii inapaswa kuwa lila na fila. Unaelimishwa ili uweze kutumia elimu katika maisha yako ya kila siku. Ktk hali hiyo, mwanafunzi anaye hitimu darasa la 12 au 14 ni vizuri aongeze na taaluma kama uhandisi (VETA), uhasibu nk. Wa chuo kikuu huyo tayari ni wakutumika ama kwa kujiajiri au kuajiriwa. Kujiajiri hapa ni kimbembe tatizo linakuwa mtaji.,..

Viongozi: Kama nilivyoeleza hapo juu, waviongozi wetu mara wachaguliwapo kuingia madarakani ni moja kwa moja wanona matatizo yao yamekwisha, hivyo swala la kumshirikisha mwanachi wa kawaida, labda ingekuwa kupiga kura kunakaribia.

Mila na desturi zetu: kuna jitihada za makusdi kuzifilisisha.... (ni mjadala mrefu).

KWA KIFUPI UMASKINI WETU UNATOKANA NA KUTOKUWA NA VIONGOZI WAADILIFU, kWAONGOFU, WACHA MUNGU. TULIOKUWA NAO NI WANAFIKI NA WAFISADI.
kwa kifupi hata viongozi cdm wana tabia hizo hizo wao si waganda wamezaliwa humu humu tz
 
Inashangaza sana tuna madini ambayo wazungu na mafisadi wa kizalendo wanayafaidi na sisi tunabakizwa na mashimo tu, eti ndege zilikuwa zinatua kwenye machimbo na kupakia madini kupeleka nje zaidi ya miaka saba ndio serikali baada ya kugujua madini yanakaribia kuisha ndio wakaweka sheria ya kukagua ndege kabla ya kuruka, mi nimesinzia lakini wabunge hasa wa chama tawala na serikali kwa ujumla wamelala tena wamewekewa na dawa ya usingizi kabisa
 
  • Thanks
Reactions: LEU
Hicho ni kilio cha waTanzania wengi...lakini jukwaa hili ni la kufutana machozi yanayotokana na kilio cha matatizo mbali mbali ya kiafya! Upo JF Doctor mkuu.
 
Tanzania ni maskini na itaendelea kuwa maskini kuliko nchi zote duniani kwa sababu ya CCM. CCM maana yake ni mfumo uliowekwa na CCM wa kuendesha serikali pamoja na utashi wa viongozi wa CCM. Viongozi wengi wa CCM ni wala rushwa, wazembe, na hawana utaifa hata kidogo. Ingawaji Tanzania ni nchi yenye raslimali nyingine kuliko nchi zote dunia lakini imekosa kuongozwa na chama kinachokerwa na watu wenye utashi wa kuondoa umaskini wa watu wake.

CCM mara nyingi wanajikita zaidi kujadili namna ya kuendelea kubaki madarakani kuliko kutafuta njia ya kuleta maendeleo kwa watu wake na taifa kwa ujumla. Ni heri wakae madaraka 5 mitano yenye mafanikio ambayo watanzania wataikumbuka kuliko kukaa zaidi ya miaka 50, watu wake wakiwa wanaendelea kuwa maskini, wanakosa hata mlo wa siku moja, na kukosa huduma za afya, na dawa angalao hata asprin

Kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa jinsi ya kuinusuru tanzania na hii hali. Kuna haja ya kupunguza marupuru ya viongozi wa juu serikalini, ofisi ya raisi, na wabunge ili kumsaidi mwananchi wa kawaida. Nchi imekuwa na matabaka. wengi wanatafuta ubunge kwa maslahi binafsi kuliko kusaidia kubadili hali iliyopo. wabunge wengi wa CCM hawapo kwa msalahi ya wananchi, bali yao na viongozi wa chama chao.

Tanzania haiwezi kuendelea hadi mwisho wa dunia hadi CCM itakapondoka madarakani. Wananchi wakichelewa kuindoa CCM madarakani mapema, mali zote za watanzania kama madini zitakua zimekwisha, na hii nchi watu wake watakua omba omba ktk nchi zingine.

Watanzania wanahitaji watu/viongozi ambao wanakerwa na umaskini wao. Kwa sasa hatuna viongozi kama hao. Wote wanafikiria matumbo yao tuu. Mtu anapewa shirika anaongoza kama anavyotaka yeye.anaweza akamfanya hata kimada wake director of idara mjawapo. No integrity,no ethics, no accountability. A hopeless country ever in the world.

Kuna haja ya viongozi kupewa kazi kwa contracts with clear deliverables. How comes mtu anapewa institution for 15-20 years, without any assessment for his performance. As long as ni kada wa CCM hata kama hafanyi chochote, anaendelea kuwepo wakati wafanyakazi na wananchi wanapata shida.

Kwanini CCM inadhamanisha watu binafsi (individuals) kuliko wananchi walio wengi? unaona kabsa kuna mtu mwana ccm ananyanyasa wananchi walio wengi lakini hachukuliwa hatua. Is an individual CCM member better than majority Tanzanians. hata kama siyo ccm members lakini ni watanzania. chama kilichopo madarakani kinatumikia watanzania wote.

very sad. sijui ni lini tutaondoka na ccm ili tuondokane na maskini, wizi, ufisadi, na kurudisha hadhi ya tanzania kama nchi zingine duniani.
 
Tanzania ni maskini na itaendelea kuwa maskini kuliko nchi zote duniani...

#~Takwimu, takwimu, takwimu !! x 2
#~ source, source, source !! x 2
 
sawa lakini badala ya kujaza CCM kila sehemu nakushauri ungekuwa unawataja watu hao wasiojali wananchi. it makes a lot of sense hapa JF ni ukweli na uwazi. kuna hata wabunge/viongozi nje ya CCM ni hopeless.
Fanya analysis kwenye private organizations pia. Fikiria kwanini watanzania hatutoki iwe kwenye filamu, mpira, bongo flava, mbio, nk ukiacha big brother ambako tumefunika kiasi. hata maeneo ambayo hayategemei CCM na serikali yake bado tumedorora? why????
 
Tanzania ni maskini na itaendelea kuwa maskini kuliko nchi zote duniani kwa sababu ya CCM. C. Ingawaji Tanzania ni nchi yenye raslimali nyingi kuliko nchi zote dunia

Kimsingi una haki ya kuwa na chuki na CCM lakini tafadhari naomba kidogo udhibitisho wa haya!!
 
source takwimu nenda leo hospital kuu ya rufaa muhimbili angalia wodini wagonjwa wanavyolala chini sakafuni,pia andikiwa kipimo xray,ultra sound,ecg,eeg utaambiwa hapa muhimbili hakuna au utapimwa baada ya mwezi.nenda agha khan au regency na mgonjwa akapimwe kisha umrejeshe na majibu!compare na idadi ya ma v8,posho za safari,na faida wapatao wahindi kupitia tenda za serikali!
 
ni kweli ndg yangu gdp ranking 2010 tanzania ni kati ya nchi kumi maskini saaana
 
sawa lakini badala ya kujaza CCM kila sehemu nakushauri ungekuwa unawataja watu hao wasiojali wananchi. it makes a lot of sense hapa JF ni ukweli na uwazi. kuna hata wabunge/viongozi nje ya CCM ni hopeless.
Fanya analysis kwenye private organizations pia. Fikiria kwanini watanzania hatutoki iwe kwenye filamu, mpira, bongo flava, mbio, nk ukiacha big brother ambako tumefunika kiasi. hata maeneo ambayo hayategemei CCM na serikali yake bado tumedorora? why????

Hakuna ku fail bila kuhusisha ccm hapa, system mbovu ya ccm ndo inasababisha tusitoke kwa lolote, huwezi kuwa na filamu nzuri bila kuwa na shule nzuri ya kufundishia wacheza au watengeneza filamu, huwezi kuwa na bondia au mkimbiaji mzuri anayekula mlo mmoja tena usiokuwa balanced, huwezi kuwa na taifa stars nzuri kwa kutegemea wachezaji wanaotegema mkalimani ili kumwelewa mwalimu wao, huwezi kuwa na mtaalamu wa komputer anayejifunza computer kwa ubao mweusi na chaki nyeupe huku akiwa amekaa juu ya tofali, huwezi kuwa na engineer mzuri anayesoma kwa mshumaa tena baada ya kuuza maandazi ili kusidia kuinua kipato cha familia, ccm imeua nchi yetu wakae pembeni tuanze upya kuijenga. Nilimsoma william malecela akisema eti tuliacha kulima zabibu hapa tz kwa sababu, kuna kampuni kutoka south afrika ilianza kuleta wine hapa, kwa nini tz haikupeleka wine SA ili mashamba yao yafungwe na wanunue wine kwetu, hebu fikiria tanzanite tunayo peke yetu lakini kenya wanauza tanzanite kuliko sisi. Now what is this???????????
 
CCM hovyooo kabisa hopeless chama kisichokuwa na msaada kwetu wa tanganyika. na hatutakaa tuendelee under this hopeless trash called CCM
 
Kama mna saini mikataba ya madini hoteli kwanini Tanzania isiwe maskini
Kama Rais hajui wamiliki wa Dowans kwanini Tanzania isiendelee kuwa maskini
Kama Rais hajui kwanini Tanzania ni maskini, kwanini Tanzania isiendelee kuwa maskini
 
Back
Top Bottom