mkulimamwema
Senior Member
- Apr 14, 2011
- 153
- 18
A hsante Hoyce ila nakumbuka nilisikia kwenye BBC pia lakini hakuna neno uzuri sasa wengi tunakubaliana na kukumbuka majibu ya JK
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mi ckumchagua labda weweMtu kama hajui chanzo cha umasikini wetu je anawajua adui zet wakubwa?
Next time tusichague raus mcheza ngoma.
Kikwete ni zuzumagic bin Vasco da Gamma msimhukumu, hajui analolifanya zaidi ya kuzunguka dunia
kwa kifupi hata viongozi cdm wana tabia hizo hizo wao si waganda wamezaliwa humu humu tzKWA NINI WATANZANIA WENGI NI MASKINI?
Sijawahi kumwona Mtanzania kwa wakati wowote ule ameondokana na umaskini, umaskini ambao sasa ni mkubwa mno na unakaribia kutudidimiza.
Binafsi nauchukulia umaskini kama kukosekana kwa mahitaji ya lazima ya kila siku kwa mwanadamu: malazi mazuri, chakula bora (ambavyo hivyo vyote vinapatikana kama binadamu huyo huyo anakuwa na njia ya kujipatia kipato) na uongozi bora wa haki unaofuata sheria (ili huduma mhimu za jamii: shule, hospitali, barabara, maji salama nk vipatikane).
Watanzania wengi tu maskini wa kutupa kwa sababu tunagharimia mno uendeshaji wa kila siku wa serikali yetu (isivyokuwa lazima).
Wanasiasa ndio watoa maamuzi hata ya kitaalauma hata kama si wana taaluma husika.
Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana. Kihio kutoka A. Kusini analipwa mamilioni ya pesa hata kama utendaji wake ni mbovu. Mfano NET GROUP SOLUTION, wanaishi maisha ambayo hata kwao hawana. Na wazawa waliokuwa nao wanajilipa pesa ambayo haina mfano.
Wanasiasa wanajilipa pesa nyingi ukilinganisha na wataalamu waliosomea taaluma mbali mbali.
Tatizo la wanataaluma kutothaminiwa limewasukuma baadhi yao kujiingiza ktk siasa. Hapa ndo kichekesho kinatokea. Mwana taaluma huyo huyo akiwa nje ya siasa anakuwa critic wa governing system! Kuna prof. mmoja ambaye ni waziri kwa sasa wakati akiwa chuoni alikuwa ni mtu ambaye aliponda jinsi nchi yetu inavyoongozwa shaghala baghala, alivyoukwaa ubunge huko kwao akateuliwa ktk baraza la mawaziri.. nasikia alikwenda kuwashukuru waliompigia kura kwa dege la jeshi kwa gharama ya serikali. Wako wengi wa aina hiyo.
Elimu ya mafunzo ya darasani na hali halisi iliyoko nje katika jamii inapaswa kuwa lila na fila. Unaelimishwa ili uweze kutumia elimu katika maisha yako ya kila siku. Ktk hali hiyo, mwanafunzi anaye hitimu darasa la 12 au 14 ni vizuri aongeze na taaluma kama uhandisi (VETA), uhasibu nk. Wa chuo kikuu huyo tayari ni wakutumika ama kwa kujiajiri au kuajiriwa. Kujiajiri hapa ni kimbembe tatizo linakuwa mtaji.,..
Viongozi: Kama nilivyoeleza hapo juu, waviongozi wetu mara wachaguliwapo kuingia madarakani ni moja kwa moja wanona matatizo yao yamekwisha, hivyo swala la kumshirikisha mwanachi wa kawaida, labda ingekuwa kupiga kura kunakaribia.
Mila na desturi zetu: kuna jitihada za makusdi kuzifilisisha.... (ni mjadala mrefu).
KWA KIFUPI UMASKINI WETU UNATOKANA NA KUTOKUWA NA VIONGOZI WAADILIFU, kWAONGOFU, WACHA MUNGU. TULIOKUWA NAO NI WANAFIKI NA WAFISADI.
Tanzania ni maskini na itaendelea kuwa maskini kuliko nchi zote duniani...
Tanzania ni maskini na itaendelea kuwa maskini kuliko nchi zote duniani kwa sababu ya CCM. CCM maana yake ni mfumo uliowekwa na CCM wa kuendesha serikali pamoja na utashi wa viongozi wa CCM. Viongozi wengi wa CCM ni wala rushwa, wazembe, na hawana utaifa hata kidogo. Ingawaji Tanzania ni nchi yenye raslimali nyingine kuliko nchi zote dunia lakini imekosa kuongozwa na chama kinachokerwa na watu wenye utashi wa kuondoa umaskini wa watu wake.
CCM mara nyingi wanajikita zaidi kujadili namna ya kuendelea kubaki madarakani kuliko kutafuta njia ya kuleta maendeleo kwa watu wake na taifa kwa ujumla. Ni heri wakae madaraka 5 mitano yenye mafanikio ambayo watanzania wataikumbuka kuliko kukaa zaidi ya miaka 50, watu wake wakiwa wanaendelea kuwa maskini, wanakosa hata mlo wa siku moja, na kukosa huduma za afya, na dawa angalao hata asprin
Kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa jinsi ya kuinusuru tanzania na hii hali. Kuna haja ya kupunguza marupuru ya viongozi wa juu serikalini, ofisi ya raisi, na wabunge ili kumsaidi mwananchi wa kawaida. Nchi imekuwa na matabaka. wengi wanatafuta ubunge kwa maslahi binafsi kuliko kusaidia kubadili hali iliyopo. wabunge wengi wa CCM hawapo kwa msalahi ya wananchi, bali yao na viongozi wa chama chao.
Tanzania haiwezi kuendelea hadi mwisho wa dunia hadi CCM itakapondoka madarakani. Wananchi wakichelewa kuindoa CCM madarakani mapema, mali zote za watanzania kama madini zitakua zimekwisha, na hii nchi watu wake watakua omba omba ktk nchi zingine.
Watanzania wanahitaji watu/viongozi ambao wanakerwa na umaskini wao. Kwa sasa hatuna viongozi kama hao. Wote wanafikiria matumbo yao tuu. Mtu anapewa shirika anaongoza kama anavyotaka yeye.anaweza akamfanya hata kimada wake director of idara mjawapo. No integrity,no ethics, no accountability. A hopeless country ever in the world.
Kuna haja ya viongozi kupewa kazi kwa contracts with clear deliverables. How comes mtu anapewa institution for 15-20 years, without any assessment for his performance. As long as ni kada wa CCM hata kama hafanyi chochote, anaendelea kuwepo wakati wafanyakazi na wananchi wanapata shida.
Kwanini CCM inadhamanisha watu binafsi (individuals) kuliko wananchi walio wengi? unaona kabsa kuna mtu mwana ccm ananyanyasa wananchi walio wengi lakini hachukuliwa hatua. Is an individual CCM member better than majority Tanzanians. hata kama siyo ccm members lakini ni watanzania. chama kilichopo madarakani kinatumikia watanzania wote.
very sad. sijui ni lini tutaondoka na ccm ili tuondokane na maskini, wizi, ufisadi, na kurudisha hadhi ya tanzania kama nchi zingine duniani.
Tanzania ni maskini na itaendelea kuwa maskini kuliko nchi zote duniani kwa sababu ya CCM. C. Ingawaji Tanzania ni nchi yenye raslimali nyingi kuliko nchi zote dunia
sawa lakini badala ya kujaza CCM kila sehemu nakushauri ungekuwa unawataja watu hao wasiojali wananchi. it makes a lot of sense hapa JF ni ukweli na uwazi. kuna hata wabunge/viongozi nje ya CCM ni hopeless.
Fanya analysis kwenye private organizations pia. Fikiria kwanini watanzania hatutoki iwe kwenye filamu, mpira, bongo flava, mbio, nk ukiacha big brother ambako tumefunika kiasi. hata maeneo ambayo hayategemei CCM na serikali yake bado tumedorora? why????
ccm kweli mnatuyayusha!