Radhia Sweety
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 4,433
- 1,771
umebadilika?? juzi tu ulikua unamsifia JK hapa
nchi yetu nitajiri tena sana lakini viongozi wetu wana maji kwenye vichwa na tamaa zimewazunguka na wanapenda kula na kuvimba matumbo
Nchi siyo maskini ila maskini ni nchi.
nchi yetu nitajiri tena sana lakini viongozi wetu wana maji kwenye vichwa na tamaa zimewazunguka na wanapenda kula na kuvimba matumbo
uvivu uliosababishwa na nini?sababu haiwezi kuwa moja tu zipo kadhaa lakini mojawapo ni uvivu wa sisi watanzania kukabiliana na changamoto za maisha
kuna vitu vingine havina mbadala. Katika biashara tunasoma kuhusu elastic/inelastic demand pamoja na substitute products. Mfano mdogo chumvi. Kadhalika kuna vitu vinaitwa MISINGI. Msingi haubadiliki bali unaimarishwa ili kuboresha kilichoko juu yake. WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA. Mengine yote blah blah tu. Sijui MKUKUTA, MKURABITA, MKUZA, KILIMO KWANZA, ETC. Yote hayo ni jitihada za kuukimbia ukweli. Labda watasema ndio mchakato wa kudadavua hizo variable nne, ila si kweli.
WATU
Human resource. Rasilimali watu. Ndio kusema hawapo? Wapo ila hawapewi kipaumbele. Tazama walimu, madaktari, wahandisi, etc. Wanauawa, wanapuuzwa, wanatorokea nje, n.k.
ARDHI
Ni ya kumwaga. Ina rutuba. Watawala wamehodhi ardhi kubwa na yenye rutuba. Ardhi nzuri inaporwa toka kwa wannanchi wanapewa wawekezaji. Rejea kanda ya ziwa, kigamboni, Tabora, Manyara, Pwani, etc. Hata hivyo bado tuna ardhi kubwa.
SIASA SAFI
Wizi wa kura na ubabe na vitisho na mauaji kwenye chaguzi ni ziashiria vya ubovu wa siasa. Viongozi kupishana kauli juu ya masuala muhimu ya kitaifa, mfano suala la walimu na madaktari, suala la afya za viongozi, ufisadi, kujilimbikizia mali, etc. Yote haya yanaondoa uhalisia wa siasa safi.
UONGOZI BORA
Kiongozi bora ni yule kwa kizungu wanaita proactive. Pale ambapo kiongozi anasubiri kuwa reactive madhara yake ni matukio kuongoza fikra na sio fikra kusababisha matukio. Viongozi ni waoga wa kutoa maamuzi na hasa maamuzi magumu. Maamuzi magumu yanashindikana kutolewa kutokana na viongozi kuwa sehemu ya kufanyiwa hayo maamuzi. Yaani kuwajibishwa. Mwenye dhamana ya kuwajibisha ana rundo la hatia. Uongozi bora ni kuwasikiliza wananchi, kutatua kero zao, kujibainisha nao, kuandaa miongozo ya kufikia malengo ya muda mfupi na mrefu, kusimamia sera, sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, na ikibidi, kuachia madaraka. Huo ndio uongozi bora.
Nje ya hayo mambo manne ni porojo tu. Ni sawa na mwanaume anayemuacha mke wake kitandani usiku na kwenda kutafuta malaya. Ni starehe ya muda mfupi sana, ni gharama, pia ni hatarishi. Majibu ya matatizo yetu yapo ndani yetu. Yapo ndani ya uwezo wetu. Zaidi ya hapo ni kujidhalilisha tu kwa kugeuka ombaomba. Bob aliimba 'Rat Race'. Ndani ya mashairi kuna maneno, Abundance of water a fool is thirsty...
Well said Iron Lady...I wish vijana wanasiasa wangepitia sana mjadala huu.. ni muhimu sana kuelewa mambo haya kwa ujumla wake.Nafiikiri kuna tatizo la kimfumo, kuanzia elimu kwani elimu ya mtanzania haisaii sana mtanzania kuwa mbunifu na muanzishaji wa mambo mbali mbali bali ni mkubali wa kila kiletwacho, tatizo lingine ni la ki uongozi hatujapata bado viongozi wa kuwa na dira ya kueleweka na uchungu wa maendeleo ya taifa, wengi wao ni walafi na wenye uchu wa utajiri, ndio maana ni ngumu kusimamia mali za taifa na wakati mwingine kusaini mikataba ya ajabu na yenye hasara kwa taifa.
Tatizo jingine ni malezi mila na destruri, hizi zina mchango mkubwa katika kuchangia umaskini wetu kama mtu mmoja mmoja, watanzania kulinganisha na kesha tuko tofauti sana hatuna haraka ya maendeleo ya mtu binafsi, na tumelelewa kutegemea sana familia zetu nikimaanaisha kijana anategemea kwao hadi anapofika umri wa miaka 25 wengine hadi 30 ndipo anapata ajira na kuanza kuhangaikia maisha yake binafsi hadi akae sawa na kutoka kimaisha umri umeshaenda, bado ndugu wanamtegemea na mambo mengi sana kama mzigo kwake. Lakini wenzetu wanalelewa kujitegemea na kutafuta vya kwao tangu wakiwa vijana wadogo ndio maana wapo agressive kuitafuta fedha. Hata hivyo walezi tuliyolelewa sisi sio ya kuwa watafutaji wa maendeleo labda siku hizi tumeanza kibadilika baada ya kuona wenzetu duniani wanaishi vipi.
Hivyo basi tukitaka mabadiliko kuna kazi kubwa ya kufanya katika maeneo haya.
Hatujawahi lakini unataka kusema maskini hawezi jiuliza kwa nini yeye ni maskini ikiwa yeye anataka maisha bora? Maskini asiyeweza kujiuliza hivi basi karidhika na Umaskini na hivyo kuishi kwa mtaji wa bakuri la kuombea sadaka.Kwani kuna siku Tanzania ilikuwa ni nchi tajiri?
Hatujawahi lakini unataka kusema maskini hawezi jiuliza kwa nini yeye ni maskini ikiwa yeye anataka maisha bora? Maskini asiyeweza kujiuliza hivi basi karidhika na Umaskini na hivyo kuishi kwa mtaji wa bakuri la kuombea sadaka.
Well said. Mwalimu Nyerere lihimiza kwamba fedha ni matokeo, sio msingi wa maendeleo, lakini baada ya kuondoka kwake, actually kuaga Dunia, tumekuwa tunaambiwa kwamba ili tuendelee, kuna suala la tano ambao tulilisahahu nalo ni MTAJI, hivyo kuwa: 1. ARDHI 2. WATU 3. SIASA SAFI 4. UONGOZI BORA 5. MTAJI.
Introduction ya mtaji ndio imetumaliza katika hii equation kwa sababu kama tatizo ni mtaji, inakuwaje huo mtaji unaotoka nje kuja Tanzania unakuja lets say as 2 units na unaondoka as capital flight of 100 units? Je ardhi sio mtaji tosha (madini, mbuga za wanyama, ardhi yenye rutuba) ya kutuwezesha kushinda umaskini?
Hiyo heading yako hapo juu hata Raisi wako JK alishasema hajui ni kwanini watanzania ni masikini! kwahiyo hilo swali labda ukamuulize tena JK anaweza kua amashapata jibu!