Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
umebadilika?? juzi tu ulikua unamsifia JK hapa

Tanzania ilishageuka kuwa shamba la bibi unajichumia na kuondoka,kwa stairi hii uzalendo ni mgumu sana hapa kikubwa ni kuutoa uongozi uliopo madarakani nikimaanisha chama washike wengine then wawajibishwe wale wote waliokwiba keki ya taifa kwa maslahi yao na familia zao then waende lupango
 
Da inabid wachukuliwe hatua kali sana maana wanatugueza sis kama sehemu ya kujinufaisha
 
nchi yetu nitajiri tena sana lakini viongozi wetu wana maji kwenye vichwa na tamaa zimewazunguka na wanapenda kula na kuvimba matumbo

Juzi kati ulikuwa unawasifia leo unawaulia mbali....ndo tulivyo wabongo
 
Nafiikiri kuna tatizo la kimfumo, kuanzia elimu kwani elimu ya mtanzania haisaii sana mtanzania kuwa mbunifu na muanzishaji wa mambo mbali mbali bali ni mkubali wa kila kiletwacho, tatizo lingine ni la ki uongozi hatujapata bado viongozi wa kuwa na dira ya kueleweka na uchungu wa maendeleo ya taifa, wengi wao ni walafi na wenye uchu wa utajiri, ndio maana ni ngumu kusimamia mali za taifa na wakati mwingine kusaini mikataba ya ajabu na yenye hasara kwa taifa.

Tatizo jingine ni malezi mila na destruri, hizi zina mchango mkubwa katika kuchangia umaskini wetu kama mtu mmoja mmoja, watanzania kulinganisha na kesha tuko tofauti sana hatuna haraka ya maendeleo ya mtu binafsi, na tumelelewa kutegemea sana familia zetu nikimaanaisha kijana anategemea kwao hadi anapofika umri wa miaka 25 wengine hadi 30 ndipo anapata ajira na kuanza kuhangaikia maisha yake binafsi hadi akae sawa na kutoka kimaisha umri umeshaenda, bado ndugu wanamtegemea na mambo mengi sana kama mzigo kwake. Lakini wenzetu wanalelewa kujitegemea na kutafuta vya kwao tangu wakiwa vijana wadogo ndio maana wapo agressive kuitafuta fedha. Hata hivyo walezi tuliyolelewa sisi sio ya kuwa watafutaji wa maendeleo labda siku hizi tumeanza kibadilika baada ya kuona wenzetu duniani wanaishi vipi.

Hivyo basi tukitaka mabadiliko kuna kazi kubwa ya kufanya katika maeneo haya.
 
kuna vitu vingine havina mbadala. Katika biashara tunasoma kuhusu elastic/inelastic demand pamoja na substitute products. Mfano mdogo chumvi. Kadhalika kuna vitu vinaitwa MISINGI. Msingi haubadiliki bali unaimarishwa ili kuboresha kilichoko juu yake. WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA. Mengine yote blah blah tu. Sijui MKUKUTA, MKURABITA, MKUZA, KILIMO KWANZA, ETC. Yote hayo ni jitihada za kuukimbia ukweli. Labda watasema ndio mchakato wa kudadavua hizo variable nne, ila si kweli.

WATU
Human resource. Rasilimali watu. Ndio kusema hawapo? Wapo ila hawapewi kipaumbele. Tazama walimu, madaktari, wahandisi, etc. Wanauawa, wanapuuzwa, wanatorokea nje, n.k.

ARDHI
Ni ya kumwaga. Ina rutuba. Watawala wamehodhi ardhi kubwa na yenye rutuba. Ardhi nzuri inaporwa toka kwa wannanchi wanapewa wawekezaji. Rejea kanda ya ziwa, kigamboni, Tabora, Manyara, Pwani, etc. Hata hivyo bado tuna ardhi kubwa.

SIASA SAFI
Wizi wa kura na ubabe na vitisho na mauaji kwenye chaguzi ni ziashiria vya ubovu wa siasa. Viongozi kupishana kauli juu ya masuala muhimu ya kitaifa, mfano suala la walimu na madaktari, suala la afya za viongozi, ufisadi, kujilimbikizia mali, etc. Yote haya yanaondoa uhalisia wa siasa safi.

UONGOZI BORA
Kiongozi bora ni yule kwa kizungu wanaita proactive. Pale ambapo kiongozi anasubiri kuwa reactive madhara yake ni matukio kuongoza fikra na sio fikra kusababisha matukio. Viongozi ni waoga wa kutoa maamuzi na hasa maamuzi magumu. Maamuzi magumu yanashindikana kutolewa kutokana na viongozi kuwa sehemu ya kufanyiwa hayo maamuzi. Yaani kuwajibishwa. Mwenye dhamana ya kuwajibisha ana rundo la hatia. Uongozi bora ni kuwasikiliza wananchi, kutatua kero zao, kujibainisha nao, kuandaa miongozo ya kufikia malengo ya muda mfupi na mrefu, kusimamia sera, sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, na ikibidi, kuachia madaraka. Huo ndio uongozi bora.

Nje ya hayo mambo manne ni porojo tu. Ni sawa na mwanaume anayemuacha mke wake kitandani usiku na kwenda kutafuta malaya. Ni starehe ya muda mfupi sana, ni gharama, pia ni hatarishi. Majibu ya matatizo yetu yapo ndani yetu. Yapo ndani ya uwezo wetu. Zaidi ya hapo ni kujidhalilisha tu kwa kugeuka ombaomba. Bob aliimba 'Rat Race'. Ndani ya mashairi kuna maneno, Abundance of water a fool is thirsty...
 
Well said. Mwalimu Nyerere lihimiza kwamba fedha ni matokeo, sio msingi wa maendeleo, lakini baada ya kuondoka kwake, actually kuaga Dunia, tumekuwa tunaambiwa kwamba ili tuendelee, kuna suala la tano ambao tulilisahahu nalo ni MTAJI, hivyo kuwa: 1. ARDHI 2. WATU 3. SIASA SAFI 4. UONGOZI BORA 5. MTAJI.

Introduction ya mtaji ndio imetumaliza katika hii equation kwa sababu kama tatizo ni mtaji, inakuwaje huo mtaji unaotoka nje kuja Tanzania unakuja lets say as 2 units na unaondoka as capital flight of 100 units? Je ardhi sio mtaji tosha (madini, mbuga za wanyama, ardhi yenye rutuba) ya kutuwezesha kushinda umaskini?
 
Katika mdororo wa uchumi. Tumesikia vingozi wetu wakisema na kutoa majibu mepesi kuwa tatizo ni la kidunia . Lakini ukweli kuna mataifa hayajaingia kwenye mdororo wa uchumi kama Brazil,India na hata china...... Je tumejiuliza kwa nini tunajiligansha na matatzo waliondelea zamani na sio kujifunza kutoka kwa mataifa yanachipuka

Kupata majibu ya suluisho sahihi la umasikini viongzi wetu na watunga sera wanataiwa kuepuka majibu mepesi mepesi.
 
Nafikiri Nyerere alijitahidi sana.

Kwanza alikuwa mzalendo, lakini pia tukumbuke kwamba wakoloni walishatuacha choka mbaya vile vichache walivyotuachia mwalimu alivisimamia kwa moyo wote kwa faida ya nchi mashule, majengo, miundo mbinu nk. Na kama haitoshi akaanzisha viwanda akaanzisha alichoamini kingesaidia (mfumo wa siasa na kujitegemea),akapeleka watanzania nje kusoma ili waje wasaidie taifa.

Japo teknolojia haikuwa nzuri sana angefanya mambo makubwa laiti angekuwapo leo alitengeneza jamii ya watendaji na sio wavivu, alianza vizuri mali za taifa alizitumia kwa maendeleo ya taifa kodi za wananchi zilifanya kinachostahili, alipotoka katika uongozi waliokuja baada ya kuendeleza wakaharibu na kuturudisha nyuma zaidi. Ujamaa uliwasaidia china hadi wakafika hapo walipo sasa.

Naamini kabisa mwalimu angekuwapo leo madarakani tungekuwa mbali. Mapungufu anayo kwani yeye sio malaika ila kwa haki ameisaidia nchi yetu
 
Kwani kuna siku Tanzania ilikuwa ni nchi tajiri?
 
Nafiikiri kuna tatizo la kimfumo, kuanzia elimu kwani elimu ya mtanzania haisaii sana mtanzania kuwa mbunifu na muanzishaji wa mambo mbali mbali bali ni mkubali wa kila kiletwacho, tatizo lingine ni la ki uongozi hatujapata bado viongozi wa kuwa na dira ya kueleweka na uchungu wa maendeleo ya taifa, wengi wao ni walafi na wenye uchu wa utajiri, ndio maana ni ngumu kusimamia mali za taifa na wakati mwingine kusaini mikataba ya ajabu na yenye hasara kwa taifa.

Tatizo jingine ni malezi mila na destruri, hizi zina mchango mkubwa katika kuchangia umaskini wetu kama mtu mmoja mmoja, watanzania kulinganisha na kesha tuko tofauti sana hatuna haraka ya maendeleo ya mtu binafsi, na tumelelewa kutegemea sana familia zetu nikimaanaisha kijana anategemea kwao hadi anapofika umri wa miaka 25 wengine hadi 30 ndipo anapata ajira na kuanza kuhangaikia maisha yake binafsi hadi akae sawa na kutoka kimaisha umri umeshaenda, bado ndugu wanamtegemea na mambo mengi sana kama mzigo kwake. Lakini wenzetu wanalelewa kujitegemea na kutafuta vya kwao tangu wakiwa vijana wadogo ndio maana wapo agressive kuitafuta fedha. Hata hivyo walezi tuliyolelewa sisi sio ya kuwa watafutaji wa maendeleo labda siku hizi tumeanza kibadilika baada ya kuona wenzetu duniani wanaishi vipi.

Hivyo basi tukitaka mabadiliko kuna kazi kubwa ya kufanya katika maeneo haya.
Well said Iron Lady...I wish vijana wanasiasa wangepitia sana mjadala huu.. ni muhimu sana kuelewa mambo haya kwa ujumla wake.
 
Kwani kuna siku Tanzania ilikuwa ni nchi tajiri?
Hatujawahi lakini unataka kusema maskini hawezi jiuliza kwa nini yeye ni maskini ikiwa yeye anataka maisha bora? Maskini asiyeweza kujiuliza hivi basi karidhika na Umaskini na hivyo kuishi kwa mtaji wa bakuri la kuombea sadaka.
 
Nimeuliza hilo swali kwa sababu ni lazima tutofautishe nchi masikini ambazo hazijawahi kuwa na maendeleo, na nchi masikini ambazo tayari zilichawahi kuwa ya namna fulani ya maendeleo lakini kutokana na sababu zinazoeleweka na zisoeleweka zinarudi nyuma na kuwa masikini.

Kuhusiana na umasikini wa Tanzania kuna mambo mengi. Moja ya matatizo hayo ni watanzania kuambiwa kuwa wao ni masikini kwa kutumia mtazamo wa jamii zingine. Hivyo umasikini ni relative term. Ukienda Bagamoyo, unaweza kumkuta mtu na minazi yake 1000 ambayo inatosheleza mahitaji yake. Katika jamii yake yeye ni tajiri, lakini kwa sababu utajiri wake hau-meet your definition utamwita masikini.

Vilevile maisha ya mmasai mwenye ng'ombe 500, yataitwa ya kimasikini kwa sababu tu mfumo wake wa maisha ni tofauti na wa kwako.

Hoja yangu sio kutetea watanzania. Lakini Tanzania ikitaka kuondoa umasikini na kuboresha maisha ya watu ni lazima iwe na definitions za umasikini.
 
Well said. Mwalimu Nyerere lihimiza kwamba fedha ni matokeo, sio msingi wa maendeleo, lakini baada ya kuondoka kwake, actually kuaga Dunia, tumekuwa tunaambiwa kwamba ili tuendelee, kuna suala la tano ambao tulilisahahu nalo ni MTAJI, hivyo kuwa: 1. ARDHI 2. WATU 3. SIASA SAFI 4. UONGOZI BORA 5. MTAJI.

Introduction ya mtaji ndio imetumaliza katika hii equation kwa sababu kama tatizo ni mtaji, inakuwaje huo mtaji unaotoka nje kuja Tanzania unakuja lets say as 2 units na unaondoka as capital flight of 100 units? Je ardhi sio mtaji tosha (madini, mbuga za wanyama, ardhi yenye rutuba) ya kutuwezesha kushinda umaskini?

Mchambuji,

Mtaji hususa pesa ni msingi wa maendeleo. Nionyeshe jamii yoyote duniani iliyowahi kuwa center of civilization ambayo haikutumia unit of transaction (money). Hivyo pesa sio matokeo kama Nyerere alivyosema.

Pesa ni msingi wa maendeleo, pesa ni nzuri kuweka akiba. Pesa ni rahisi kuisafirisha. Pesa ni kipimo cha kazi na juhudi. Na pesa ni ufanisi wa biashara.

Kuonyesha umuhimu wa pesa angalia jamii zilizoendelea na zile zenye kuangaika kutafuta maendeleo. Jamii zilizoendelea zinatumia pesa vizuri. Na zile masikini ni za zinafuja matumizi ya pesa.

Kuhusiana na swali lako kuhusu investor kuleta Tanzania 2 Units na kuondoka na 100 Units. Huo ni ulimbukeni wenu tu watanzania. 2 Units za investment zinapatikana hapo hapo Tanzania, iwapo watanzania mtaanza kufikiri kibiashara.
 
Swali hili limekuwa likiulizwa sana miongoni mwetu, tumekuwa tukijiuliza kwanini Tanzania ni maskini pamoja na maliasili zite tulizonazo?

Nakumbuka Raisi wetu kama sikosei aliwahi kuulizwa na runinga za nje kuhusu swali hili naye alishindwa kujibu. Leo ningependa kutafakari kuhusu jambo hili kwa kina na kwa mantiki ili wote tujue kwanini Taifa letu ni maskini na njia gani tufuate ili tutoke hapa tulipo.

Kwenye maandiko yangu mengi nimeandika kuhusu nini maana ya Taifa na kwanini watu wanaishi pamoja kama Taifa, leo sita gusa sana huko lakini tulijua Taifa ni kusanyiko la watu wenye malengo mamoja, tulifahamu pia Taifa lazima liwe na dira ya sehemu inayotaka kuelekea na dira hiyo lazima iliridhishwe kizazi hadi kizazi, kama Taifa ni lazima liwe na malengo, na mwelekeo wa Taifa lolote ni ''nguvu'' na ''utawala''. Lakini pia kama Taifa tunahitaji mafanikio yatayotupa faraja na heshima miongoni mwa mataifa mengine.

Sababu ya kwanza ya kutofanikiwa kama Taifa ni kuwa na viongozi wasiokuwa na malengo na kama yapo basi sio dhabiti. Hii inaonekana katika mfumo wa uongozi wetu unaoyumbayumba na usio na msimamo juu ya masuala inayosimamia. Lakini pia tumeona poor organization ya serikali yetu pale kauli mbilimbili zinapotoka katika serikali moja hii inaonyesha udhaifu katika mfumo wa uongozi.

Kabla ya kwenda mbele tuangalie kazi ya kiongozi ni nini katika Taifa.
1. Mobilization
2. organization
3. Direction
4. Govern
MOBILIZATION

kiongozi lazima awe na uwezo wa kuwashawishi watu cause anayopigania kwa manufaa ya Taifa, ni lazima ajenge uaminifu kwa raia na kuwaonyesha mambo ambayo anapigania ni kwa manufaa ya wote na yatakuwa na faida kubwa sana kwa Taifa na kuwashawishi kulitumikia Taifa lao wenyewe na kujenga umoja miongoni mwao.

ORGANIZATION.

Baada ya kuwashawishi na kumkubali jambo linalofuata ni ku organize jamii ili wafanya kazi kwa manufaa ya umma. Tunafahamu ya kuwa bila organization no function unit will work.

Kwahiyo Taifa linaundwa na watu tofauti, tofauti sawa? kuanzia katika makabila na ndani ya kabila hizo tofauti tofauti kuna dini tofauti na familia tofauti hivi vyote vinaunda Taifa moja na kufanya a ''complex thing'' Kazi ya kwanza ni kuunganisha na ya pili ni kuwaonyesha malengo ya ''Taifa''. Kwanini sisi ni Taifa ndoto zetu ni nini na matumaini yetu ni yapi na jinsi gani tutayafikia kama Taifa. Kwahiyo juhudi ya kwanza ni kuunganisha na ya pili kufanya organization and structuriling.

Sehemu ya pili tutatengeneza Taasisi zinazoserve public na zile binafsi na jinsi zitakavyokuwa zinaingiliana. Lengo la sekta zote hizo mbili ni kuwa na functional unit itakayofanya kazi kwa faida ya umma lazima tuangalie jinsi ya kufanya coordination kati ya sekta hizo mbili. Lakini hatutaweza kufanikiwa pasipo kujenga umoja na uzalendo miongoni mwetu.
Tukiisha jenga umoja na uzalendo, tukiisha ji organize sasa linakuja suala la management of our resources na jinsi gani tutazitumia kwa faida ya umma kumbukeni kwamba bila ya '' order'' '' harmony'' na coordination katika organization yeyote hakuna kitu kitazalishwa iwe kwenye mitambo au taasisi kama organization.

Mfano wa gari na components zake kwenye gari kila kifaa kina kazi yake na system yote inafanya kazi kama kitu kimoja na dereva akiwa mfano wa kiongozi ni sawa sawa na katika nchi hakuna tofauti sana.
'' Effeciency of any government depend on the unit of it's parts to form a functional unit '' Kwahiyo inategemea raia, Taasisi zilizoundwa kutumikia jamii kufanya kazi kama kitu kimoja ili kuzalisha na kusiwe na any discordant element.
Kwa Wanaonifutatilia nilianza kwa ku organize familia ni jinsi gani zina uhusiano mkubwa na Taifa na umuhimu wake katika Tafakari yangu ya Mwanzo ya UJENZI, MUUNDO na MWELEKEO wa Taifa. Tuki order vizuri familia zetu itakuwa rahisi kuzi govern na majukumu ya kila mzazi kwa familia yake is for the sake of the nation sio kwake yeye tu, a health nation is the one which has strong families. Without order nothing Valuable we can produce.

'' Operation of any organization depend mainly on the function of it’s parts in order to produce results ''
Tunapozungumzia kuhusu system ni mfumo unaofanya kazi kwa pamoja ili ku produce result na kama hakuna result kuna tatizo katika parts za hiyo unit, hiyo structure organization na structure organization inamhusu kila raia kwasababu ni sehemu ya nchi. Kwahiyo ni lazima tufanye reformation ya jamii yetu kama tunataka tuendelee na kui order upya na mifumo mingine kama ya elimu ili ifanye kazi kama kitu kimoja.

Hili sio suala la ubinafsi bali ni suala la kila mmoja wetu anazalisha nini kwa manufaa ya taifa na vizazi vyetu vijavyo. Kwasababu bila ya hivyo hatutaenda salama kama Taifa kama kila mtu akijiangalia mwenyewe boti yetu haitofika salama sisi sote tuliopo duniani sasa hivi tunawajibu wa kuwafikishia salama vizazi vyetu vijavyo Taifa hili, tuna majukumu ya pamoja. Kwahiyo kila mmoja wetu anamajukumu ya aina mbili kwasababu sisi tumeamua kuwa Taifa lazima tuliangalie Taifa letu na tujiangalie wenyewe as induviduals lazima tulijali na tuli preserve kama kingo zinavyo preserve mto na kupeleka maji yake baharini na hivyohivyo taifa letu lazima liwe ni lenye kutoa faida na wakati huo huo tukilinda kile ambacho Tayari tumeisha kijenga.

DIRECTION

Tumeishajenga organization yetu na kui structure in a very coordinated way iko katika order kama completely ''thing'' sasa inakuwa ni kazi ya kiongozi wa kuendesha huo mfumo kama nilivyosema hapo mwanzo ni kama gari na components zake sasa ni kazi ya kiongozi kuonyesha mwelekeo ni wapi Taifa lielekee lakini ili kulinda mfumo ni lazima tuwe na polisi kwaajili ya maadui wa ndani na jeshi kwaajili ya maadui wa nje.
Ili jamii yetu iwe pamoja lazima iwepo haki na tunajua haki ni harmony ya jamii kwahiyo mahakama lazima ziwepo kuhakikisha jamii inaendelea kuwa moja na haki inatendeka. Tunatakuwa na bunge ambao watakuwa wawakilishi wananchi jambo la tutawapataje ni la kutafakari zaidi lakini mfumo wa sasa unafanya watu wasiostahili kuingia bungeni.

Govern

Suala la ku givern ni kulinda mfumo ambao tayari umeisha tengenezwa na unafanya kazi kama kitu kimoja.
Kuna mambo mengi sana yanayofanya Taifa hili lisiendelee kitu kikubwa kingine ni ''motive'' Iliyopekea watu wengi kuingia kwenye siasa kusema kweli sio kuleta maendeleo ya nchi bali wengi wao ni kupata faida binafsi na hawajali kabisa kuhusu utaifa na Taifa ambalo ni muhimu pia na kwao, Taifa hili likikosa mwelekeo sisi sote tutakosa mwelekeo. Tutambue kwamba sisi tulio duniani sasa hivi tunatengeneza maisha ya generation ijayo na kama tumeamua kuwa Taifa kutoka makabila mbambali sisi ni Taifa na lengo letu ni moja kuhifadhi kizazi chetu na kujiletea maendeleo yetu sote.

''Tukikumbuka kwamba mafanikio ya pamoja huleta furaha ya Taifa zima na kila mtu atafarijika na kila mtu anastahili heshima katika Taifa lake mwenyewe''
Sasa ni wakati wetu wa kubadili fikra zetu jinsi tunavyofikiri kuhusu Taifa letu, Tunalibomoa wenyewe na hakuna atakayeathirika zaidi yetu, tukumbuke kwamba hatuna ardhi nyingine zaidi ya hii tulioachiwa na mababu zetu na jukumu letu ni kuangaliana na kujaliana na sio kuharibu Taifa letu.
Tunavyofanya sasa ni hatari sana ni sawasawa na kukata Tawi ambalo tumekalia tutaanguka hakuna kitu chochote utakacho mfanyia mtu wa Taifa lako ambacho hakita kurudia kumbukeni ya kwamba sisi ni ''Taifa'' which means we are one and we share the same destiny.

Itaendelea.
 
Hiyo heading yako hapo juu hata Raisi wako JK alishasema hajui ni kwanini watanzania ni masikini! kwahiyo hilo swali labda ukamuulize tena JK anaweza kua amashapata jibu!

hawezi kuwa na majibu.na hata kama ingekuwa homework naamini hakuifanyia kazi pale alipoulizwa hivyo si mtu wa kumtegemea kutoa majibu.
 
Back
Top Bottom