bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
Wadau
Kila kukicha asubuhi najiuliza swali "Kwa nini Tanzania ni Masikini kama tulivyo". Swali hili linanitatiza sana. Nasikia tuna migodi mikubwa tu ya Gold, Diamond, n.k. Tuna sehemu kubwa ya Ziwa kubwa kuliko yote Africa (Ziwa Victoria). Tuna ziwa lenye kina cha jini kuliko yote duniani (Ziwa Tanganyika). Tuna sehemu kubwa ya Bahari ya Hindi (Nchi nyingi zinalilia bahari). Tuna mbuga kubwa za wanyama na vivutio vingine vya utalii.
- Ni jinsi gani tunatumia hizi mali tulizonazo kujikomboa katika umasikini?
- Je tatizo ni viongozi tuliowahi kuwa nao na tulionao sasa hivi?
- Je tatizo ni sisi wananchi?
- Je tatizo ni rangi yetu?
- Je tatizo ni utamaduni wetu?
- Je tatizo ni mfumo mzima?
- Au je tatizo ni kuona kwetu na kufiria kwetu na kutojua maana ya maendeleo ni nini?
Sikubaliani na jibu la kuwa hatuna pesa. Nina imani kubwa nchi yetu kama serikali ina pesa za kutosha za kuleta tofauti kulinganisha na tulivyo. Nimetembelea nchi tofauti Africa, Ulaya na Marekani na nimeona tofauti kati ya nchi ILIYOENDELEA na nchi INAYOENDELEA. Nchi yetu kwa kweli bado hiko nyuma sana.
Kila nikipata kuendesha gari katika nchi za Ulaya i.e UK, huwa najiuliza swali, HAWA WATU WALIJENGA HIZI BARABARA LINI? Hizi ni barabara kuu (Motorways) na barabara ndogo (A & B) na hata barabara za vijijini. Watu Ulaya wanaosha magari yao mara moja kwa mwezi, si kwamba ni wachafu ila gari linakuwa bado safi kwani halijapita kwenye vumbi au matope. Sisi tulimkosea nini Mungu mpaka kila kukicha houseboy lazima aoshe gari kabla baba hajaondoka?
Mfumo wa reli (London Underground) ulianza kujengwa mwaka 1886. Je sisi sasa hivi hatuna akili ya Mzungu wa miaka hiyo? Je hatuna pesa kama walizokuwa nazo waingereza mwaka 1886? Kwa nini hata leo hii tunashindwa kubuni mbinu za kuondokana na foleni hapa Dar. Nina uhakika tukiwa na mfumo wa usafiri kama waliokuwa nao wenzetu miaka 75 iliyopita tutakuwa tumepiga hatua kubwa.
Kwa nini tunashindwa? Naomba msahada wa majibu.
Nchi yetu ni maskini kwa sababu idadi kubwa ya raia wake kama wewe hawajui kwa nini nchi hii ni maskini hivyo kupelekea kutojua nini cha kufanya.
Zakumi,
Sasa namwelewa Mwanakijiji alipozungumzia swala la UMASKINI kwa sababu tunaviumiza vichwa vyetu ktk kutafuta tafsiri na mazungumzo badala ya kuweka nguvu hizi ktk utekelezaji maana hakuna tafsiri ya UMASKINI ktk UCHUMI zaidi ya matokeo ya uwezo mdogo ktk kupata maendeleo. Ni hali halisi ulonayo regardless of what You have in store na ndio maana nikasema kamauna njaa wakati chakula kipo ndani ya friji huwezi kusema huna njaa ati nimeshiba wakati tumbo lako ni empty.
Labda ktk mfano huo huo naweza kusema kwamba Ulimbukeni wetu ulotokana na kutawaliwa ndio uliotuponza kiasi kwamba chakula kipo ghalani toka mahindi, mchele, mtama na mawele isipokuwa tunataka chakula cha Mlimani City na Shoppers ambacho kiko tayari chenye hadhi ya kimataifa na kieleezo za Utajiri.. bila kujua thamani kubwa ya mahindi na mawele tuloyaacha maghalani ambayo wazungu wanakuja tena kwetu kuyataka kutokana na wao kuthamini Organic.
Hapa nikiwa na maana kwamba tuna all economic resources ambazo zinaweza kabisa kutuondoa ktk umaskini (njaa) lakini sii chakula tunachokitaka na tunatumia nguvu kubwa ktk Imported good ili kujibadirisha sisi tuonekane sawa ama kama wazungu. Sisi tunashindwa kukubali reality, na kama nisemavyo kila siku WATU na MAZINGIRA ndio focus kubwa ya neno maendeleo. Maendeleo sio watu pekee bali mazingira yao pia na wlaa huwezi kuita utajiri in aconomic term ikiwa mazingira ni mabaya. Hivyo policies zote zinapowekwa hutazama kuboresha vitu hivi vyote na sii kimojawapo.
Huyo Mmasai sisi tutamwita tajiri kwa sababu tunazithaminisha hizo ng'ombe zake 500 ktk bei za soko na kutoa namba zinayomweka Mmasai ktk utajiri au laa, lakini maadam mazingira yake yapo ktk hali mbaya utajiri wake unabakia tumbo tupu kwa sababu kuwepo kwa ng'ombe hawa na kuthaminishwa kwake bila kubadirisha maisha na mazingira yake utajiri huu ni mtupu. Na ndio maana huyo mmasai hana habari kwamba yeye ni tajiri japokuwa ana ng'ombe 500 sawa na sisi wenye dhahabu ambazo hazibadilishi maisha wala mazingira yetu. Huyu Masai sii Fukara bali ni Maskini kwa sababu umaskini unakusanya hali na mali za watu na mazingira kiuchumi..
Navyofikiria mimi, tukiondoa leo neno maendeleo basi bila shaka hata neno maskini litapotea japokuwa fukara na tajiri yatabakia kwa sababu inawahusu WATU tu na sio mazingira waliyopo. Na ktk umaskini ndio unakuta vitu kama elimu vinachangia sana kutambua mahusiano ya watu na mazingira ktk uboreshaji wake. Na neno uchumi linatokana na elimu ya kuelewa, kutambua na kupima production, distribution, and consumption of goods and services. Maadam jamii zetu zinakua na mahitaji yetu yanazidi kupanda wakati uwezo wa kutosheleza mahitaji haya unazidi kupungua ndipo neno maskini linapochukua nafasi na hivyo kusema Umaskini ni matokeo ya kushindwa kukidhi mahitaji yetu.
Kuna jambo moja hunikera sana mimi japokuwa halikubaliwi na Watanzania wengi..nalo ni matumizi ya Lugha ya kiswahili. Tumejenga utamaduni wa kuiga hadi lugha ili kuwahudumia watanzania wasiojua kiingereza, hivyo kweli tunatumia lugha kama means of communication baina ya wananchi au na kina nani?. Sasa matokeo yake mashirika yote nchini utakuta ma CEOs, board mebers na executive officers ni wageni ambao wataajiri Watanzania wanaozungumza lugha yao hao ma TX ili ku serve Watanzania ambao hawajui kiingereza. Hii kweli hatufanyi kinyume?
Kwa nini nafasi zote za juu ktk ashirika yatu zichukuliwe na wageni ambao hawawezi kuwasiliana na wananchi ila kwa kumtumia Mtanzania anaye ajiriwa kama mkarimani baina ya mgeni na Watanzania halafu hata huyo Mtanzania anapoichukua kazi ile hafahamu kwamba yeye anatumiwa kama mkarimani ila naye anakuwa mzungu ktk mawasiliano kuwataka walio chini yake na wananchi wazungumze kiingereza..
Inakuwaje Wachina wanapoingia nchini inawachukua onlt miezi sita au mwaka wanazungumza kiswahili na sio kiingereza kuwasiliana na wananchi lakini MKenya atakuja tanzania na kupewa wadhifa na nafasi kubwa kwa sababu anazungumza kiingereza, pengine hana elimu kuliko Mchina au Mtanzania..Na mwisho nawaacha na swali jingine, kwa nini nchi zote zinazotumia lugha ya kigeni ambayo sii yao ndio wako nyuma ktk maendeleo?. Hakuna Mhindi wala Mchina asiyejua kusoma na kuandika Kichina hadi maofisini mwao vitu vimeandikwa Kichina au kihindi lakini sisi hata matangazo yetu yameandikwa kiingereza ilihali ni asilimia chini ya 20 ndio wanazungumza kiingereza. Hapa mlengwa wa matangazo hayo ni nani > Unamtangazia nani?
Mzunguko gani mkuu wangu ikiwa Wajerumani wanaongea wote kijerumani na kiingereza ni baadhi ya watu tu hao hawana mbona kusema hivyo kuwa uchumi wao haulengi wajarumani!. Nenda India, China na duniani kote wanaona umuhimu wa kutumia lugha zao ktk mawasiliano na hujifunza za kigeni ktk maswala kwa sababu ndogo kabisa ya mawasilinao tu ya kawaida..Ukienda Ujarumani toka gari unayoendesha, mitambo ya viwandani, maofisini, microwave, radio magazeti TV station ni Kijarumani tupu na sio wao tu sehemu zote nilizowahi kutembelea.Mkandara,
Hata nchi zinaotusaidia zina tafsiri ya kwanini sisi ni masikini. Wanaweza kusema kuwa kipato cha wastani cha mTanzania ni chini ya dollar moja ya kiMarekani kwa siku.
Ndani ya nchi tunaweza kuwa na tafsiri ambayo itatumika kupima maendeleo yetu. Kutokuwa na tafsiri ndio sababu ya nchi kuwa na mipango mingi isiyo na matokeo yoyote yenye kuweza kufanyiwa tathmini. Na kutokuwa na tafsiri imefanya watu wapende mambo yenye kuwapa status katika jamii kuliko kufanya vitu vyenye kuboresha maendeleo.
Napenda unielewe kuwa tafsiri hiyo sio lazima ieweke mpaka ngazi za chini za kijamii. Lakini kwa watu wenye kushika madaraka na wasomi, ni muhimu kuwa na tafsiri fulani ya kuanzia.
Kwa mfano, tunaweza kusema kuwa mtanzania mwenye maisha bora ni lazima aishi au familia yake iishi kwenye nyumba ya kudumu ambayo ina vyumba vitatu. Yenye huduma za choo na maji safi. Na wakazi wa nyumba hiyo wasizidi saba.
Ukichukua tafsiri hii ya maisha bora. Utaona familia nyingi za kitanzania kwa kutumia rasimali chache na tena zinazopatikana ndani ya nchi wanaweza kufikia ubora wa maisha.
Na baada ya muda fulani unaweza kuongeza kuwa nyumba hizi ziwekewe umeme au ziwe karibu na barabara na mashule.
Kuhusiana na matumizi ya lugha. Mzungumko mzima wa uchumi haulengi watanzania wa kawaida. Hivyo umuhimu wa lugha yetu wenyewe unakuwa haupo. Lakini mChina, mHindi au Mwarabu anapokuja Tanzania anakuja kufanya biashara na watanzania wa kawaida. Hivyo yeye kuelewa lugha yetu anaona kuna faida.
Kwa maana hiyo, nadhani hili ndio tatizo letu kujibu tafsiri hizi:- Ikiwa fukara kinyume chake ni Tajiri. Je Maskini kinyume chake ni nini?..We mtu utamaduni wake unamwambia kuzaa watoto wengi na kuwa na wake/ ng'ombe wengi ndio utajiri.
Nchi yake tajiri kiasili na wala nakuwa na historia ya ushindani mkubwa.
Halafu unataka kumpangia utajiri kwa minajili ya kizungu.
Unafikiri anaweza kuwa tajiri?
Kwa maana hiyo, nadhani hili ndio tatizo letu kujibu tafsiri hizi:- Ikiwa fukara kinyume chake ni Tajiri. Je Maskini kinyume chake ni nini?..
Nyani Ngabu,
Mkuu tupe wewe sababu zake na sio ile ya Miafrika ndivyo Tulivyo! nadhani kubadilishana mawazo kunaweza kuchangia sana tukubali makosa au mapungufu yetu.
Mzunguko gani mkuu wangu ikiwa Wajerumani wanaongea wote kijerumani na kiingereza ni baadhi ya watu tu hao hawana mbona kusema hivyo kuwa uchumi wao haulengi wajarumani!. Nenda India, China na duniani kote wanaona umuhimu wa kutumia lugha zao ktk mawasiliano na hujifunza za kigeni ktk maswala kwa sababu ndogo kabisa ya mawasilinao tu ya kawaida..Ukienda Ujarumani toka gari unayoendesha, mitambo ya viwandani, maofisini, microwave, radio magazeti TV station ni Kijarumani tupu na sio wao tu sehemu zote nilizowahi kutembelea.
Hakuna nchi inatumia lugha ya Kigeni ktk mawasilino ndani ya nchi yake isipokuwa nchi maskini ambazo hatujaendelea na tunazidi kuwa maskini. Huoni kama tayari tumekubali matokeo ya Utumwa wa fikra na pengine kikwazo cha maendeleo yetu kutoweza kuwasiliana sisi wenyewe..Utaendeleza vipi kilimo kama msomi wako kasomea Kilimo kwa kiingereza akienda kwa mkulima anashindwa kumwelekeza Mkulima kwa kiingereza maana mkulima hajui kiingereza, na Huyo msomi anashindwa kujieleza kwa kiswahili?. Sasa utaweza vipi kuzalisha kilimo ili kujitosheleza ikiwa mwanzo tu tumegota ktk mawasiliano baina yetu wenyewe..
Leo kule FB kwa Mwanakijiji nimeandika hivi, Ebu wabunge wetu waende vijijini wakaombe kura za wananchi kwa kiingereza tuone kama wataeleweka!..Hata Hii JF iwekwe kwa kiingereza tuone kama itapata umaarufu huu. Kwa hiyo kuendelea kwa JF na kufanikiwa kwa JF au wabunge kunatokana na lugha kwanza inayotumika baina ya makundi wanaolengwa. Maendeleo ya Tanzania hayamlengi mgeni isipokuwa sisi wenyewe na sisi ndio tutakaoijenga Tanzania. Sioni sababu kabisa ya mashirika yetu ku hire wageni kwa sababu ya kiingereza ili hali walengwa - consumers hawazungumzi lugha hiyo. Huu ni ulimbukeni kufikiria kwamba mgeni anayezuungumza kiingereza atakuwa na ufanisi wa kazi ama kuongeza uzalishaji..Hii kasumba mbaya sana.
Hao wageni tunafanya biashara nao ambao duniani kote kila mmoja wao ana lugha yake na anaithamini, sisi ombaomba ndio hubadilisha lugha zetu tunapokutana nao lakini sio wao. Alipokuja Waziri mkuu wa China alizungumza Kichina akawa na mkarimani wake akitafsiri sio kiswahili bali kiingereza! wakati huyo huyo Waziri mkuu wa Mchina akienda France ataongea Kichina na Mfaransa ataongea Kifaransa wakarimani katikati haukna aliyelazimika kutumia lugha ya mwenzake na the all Europe na jumuiya yao, ni asilimia ndogo sana kwa kila nchi wanazungumza kiingereza tena as a second language wala hakuna uhalisia wa matumizi ya lugha kama tunavyofikiria sisi.
Na swala la Kipimo cha Umaskini kuhusiana na pato la mwananchi mimi huwa siliwekei maanani sana ikiwa hiyo Dollar moja ingemwezesha mtu kununua chakula kwa siku nzima isingekuwa na maana kwetu... lakini sivyo kwa sababu kinacho thaminishwa ni pato la taifa kwa fikra za kusadikika hata kama ni asilimia 1 tu ndio wenye kushika asilimia 99 ya utajiri huo..
We mtu utamaduni wake unamwambia kuzaa watoto wengi na kuwa na wake/ ng'ombe wengi ndio utajiri.
Nchi yake tajiri kiasili na wala nakuwa na historia ya ushindani mkubwa.
Halafu unataka kumpangia utajiri kwa minajili ya kizungu.
Unafikiri anaweza kuwa tajiri?
Nguruvi3, mara nyingi huwa nadhani wewe ni alias ya Dr Slaa, many times michango yako inakuwa kama the real Slaa, inawezekana siye, however i admire youre ideas many times!Mkuu Jmushi1, narudi kule nilikoanzia ya kuwa uongozi ndiyo chanzo cha umasikini na wala sio culture. Kama kuna watu rahisi sana kuwabadilisha kwa culture ni Watanzania.
Tunayo mifano kama ya Nyerere, yeye alikuwa mkali kiasi kwamba pesa ikidhamiriwa kujenga shule au kituo cha Afya itafanyika hivyo. Haina maana ulaji haukuwepo, la hasha! tofauti ni kuwa mlaji alijua kuwa hatima yake ipo matatani.
Yupo Sokoine na tunakumbuka mambo aliyoyafanya.
Augustino Mrema hakutumia hata senti tano kuwaambia watu wa soko la kariakoo kusafisha na kujiwekea utaratibu.
Keenja yeye alikaa kidete na jiji hadi tukaona japo vibara bara vya watembea kwa miguu vinasakafiwa, jiji linakuwa safi.
Paseko Kone yeye alisimama na kuwaambia wana singida itajengwa hospitali ya kisasa na imejengwa kwa kiwango alichoweza yeye.
Nimetoa mifano hiyo kuonyesha kuwa hakuna culture ya kudumu ili kuna culture inayolelewa.
Mifano ipo mingi sana na orodha ni ndefu ya viongozi hadi ngazi za wailaya waliojaribu japo tukaona.
Huwezi kuondoa umasikini kama hakuna nidhamu. Leo CAG anasema mabilioni yanayoweza kuedesha wizara yametafunwa na hakuna kiongozi yoyote anayohoji hatua gani zimechukuliwa ili kuziba mianya na wahalifu kuadhibiwa.
CAG amebaki kukabidhi ripoti katika televisheni na magazeti.
Hakuna kiongozi anayejiuliza je tunatumia tunachozalisha au tulicho nacho? Kwasababu hawaulizi na wameamini kuwa kuna wafadhili watatoa 40% ya bajeti, mipango iliyokichwani ni fenicha na VX achilia mbali kulamba pesa kwa njia haramu. Nusu karne hatujaweza ku-balance bajeti lakini unasikia ya akina Makinda na kujiuzulu kwa wabunge
Hakuna kiongozi anayetoka asubuhi akiwaza atawasadiaje watanzania wajikombea. Kama yupo nitashangaa kwasababu haiwezekani mahindi yaoze Sumbawanga halafu katibu mkuu au waziri anatia sahihi mkataba wa kuletewa mchele na mahindi kutoka korea. Hawana hata aibu sasa wazo la kuondoa umasikini watalipata wapi.
Culture ya uvivu na kutowajibikaji inajengwa na viongozi. Kwanini mfagizi wa ofisi awe muungwana sana na aache kuuza maandazi kama mbunge anayepokea milioni 12 kwa mwezi bado anaona maisha magumu.
Kwanini nimshataki afisa aliyeiba laki 3 kwa kufoji halafu Jairo astaafishwe na marupu rupu juu.
Nimalizie kusema, hoja yangu ni kuwa hata kama una vitu na rasilimali zote kama hakuna wa kuongoza namna ya kuzitafuta, kuzikusanya, kuzipangia na kuzigawa ili ziwe na tija hakuna chochote kitakachofanyika.
Mkuu Mkandara kasema sisi ni kama wamasai wenye ng'ombe 3,000 lakini hana mahali pa kulala.
Angalia sehemu zote duniani zilizopiga hatua, chagizo kubwa ni uongozi.
Naamini kabisa umasikini wetu unachangiwa na uongozi kama chanzo mengine ni sehemu tu ya tatizo.
Nguruvi3, mara nyingi huwa nadhani wewe ni alias ya Dr Slaa, many times michango yako inakuwa kama the real Slaa, inawezekana siye, however i admire youre ideas many times!
Nakubaliana all the way na analysis yako.