Salaam wana JF!
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ni moja kati ya mataifa masikini sana duniani.
Umasikini huo upo licha ya maliasili lukuki zilizotapakaa kwenye kila kona ya nchi:
a. Maziwa makubwa yenye samaki na viumbemaji vya kutosha - Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Ruvuma n.k.
b. Mito mikubwa yenye samaki wa kutosha - Kagera, Mara, Ruvuma, Iringa, Mtwara, Tanga, Kilimanjaro, Rukwa n.k.
c. Misitu mikubwa yenye rasilimali mbao, wanyamapori, madawa ya asili, matunda, nyuki n.k. - Manyara, Tanga, Lindi, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Rukwa, Iringa n.k.
d. Wanyamapori wa kila aina - Mara, Arusha, Kigoma, Iringa, Tanga, Manyara, Pwani, Kilimanjaro, Rukwa, Zanzibar n.k.
e. Bahari ya Hindi yenye viumbebahari wa kila aina - Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi na Zanzibar.
f. Madini ya kila aina - Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, Kagera n.k.
g. Na sasa ina gesi - Mtwara
Pamoja na rasilimali watu, takribani milioni 45.
Sasa swali kwa wanachama, wapenzi, washabiki na wanazi wa CCM, kwa nini Tanzania bado ni masikini sana?
Ni swali jepesi sana, lakini lenye kuhitaji majibu ya uhakika na kina.
Cc:
Ritz chama zomba Jichola3 ZeMarcopolo Nduka [MENTION=95413]thatha
Atongwele