ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Kwa nini isiachie ngazi kama imeshindwa kutoa uvivu na upenda porojo wa watanzania?
Ndiyo haijaingia kwa mtutu, lakini kama unaona hiyo ndiyo sababu ya umasikini, basi serikali yako ya CCM iachie ngazi, maana imeshindwa kazi.
Salaam wana JF!
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ni moja kati ya mataifa masikini sana duniani.
Umasikini huo upo licha ya maliasili lukuki zilizotapakaa kwenye kila kona ya nchi:
a. Maziwa makubwa yenye samaki na viumbemaji vya kutosha - Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Ruvuma n.k.
b. Mito mikubwa yenye samaki wa kutosha - Kagera, Mara, Ruvuma, Iringa, Mtwara, Tanga, Kilimanjaro, Rukwa n.k.
c. Misitu mikubwa yenye rasilimali mbao, wanyamapori, madawa ya asili, matunda, nyuki n.k. - Manyara, Tanga, Lindi, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Rukwa, Iringa n.k.
d. Wanyamapori wa kila aina - Mara, Arusha, Kigoma, Iringa, Tanga, Manyara, Pwani, Kilimanjaro, Rukwa, Zanzibar n.k.
e. Bahari ya Hindi yenye viumbebahari wa kila aina - Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi na Zanzibar.
f. Madini ya kila aina - Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, Kagera n.k.
g. Na sasa ina gesi - Mtwara
Pamoja na rasilimali watu, takribani milioni 45.
Sasa swali kwa wanachama, wapenzi, washabiki na wanazi wa CCM, kwa nini Tanzania bado ni masikini sana?
Ni swali jepesi sana, lakini lenye kuhitaji majibu ya uhakika na kina.
Cc: Ritz chama zomba Jichola3 ZeMarcopolo Nduka thatha @ Atongwele
Kawaambie CHADEMA fedha ya ruzuku wanayopewa kila mwezi takribani mil.300 fedha ya Tanzania waikatae kwani ingefaa zaidi ielekezwe kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa wa fedha kama zahanati n.k.
Ningewaona chadema waungwana kweli, kama walivyo wadanganya watanzania kuwa hawataki magari ya hanasa huku wanayachukua kwa siri.
Ulaji hauna chama, hata chadema wakiingia madarakani swali lako HALITAPATA JIBU.
hamy d habari za masiku?
Kwanini tanzania bado maskini chini ya ccm?
Hii dhana ya umaskini wewe unaielezeaje?
Maana wakati mwingine mwananchi anaweza akawa anakosa mahali fulani, ili kuficha kosa lake lisionekane basi anainyooshea serikali kidole, na serikali kwa sababu ni mzazi inakubali tu lawama.
Hapa najaribu kukuonyesha kuwa, serikali imekuwa ikitoa fursa sawa kwa kila mwananchi kuondokana na hali ngumu ya maisha, ili utakubaliana na mimi HASWA kwenye elimu. Hapa wengi wetu pametusaidia sana kufika hapa tulipo maana tulizingatia elimu ambayo kimsingi ilitolewa kiusawa kwa wote bila kujali jinsia, udini, ukabila na hata ukanda.
Wengi wanaolia njaa humu JF na hata hao wa huko vijiweni ni kutokana na kupuuzia kitu kinachoitwa elimu, ikiwa ni moja ya sababu ya kujiletea maendeleo yako binafsi na jamii yako kwa ujumla.
Lakini pia kuna swala la afya na ustawi wa jamii, serikali kupitia sera yake ya afya, tumeona imetoa ahueni kwa watanzania walio wengi kuweza kupata matibabu na dawa katika vituo mbalimbali, japokuwa bado hali haijaridhisha lakini kwa namna moja hama nyingine, kuwepo kwa huduma hii nyeti kwenye eneo lako, basi kunakupa fursa ya kupata huduma za kimatibabu kwa gharama nafuu ukifananisha na isingekuwepo kabisa.
Swala la ulinzi na usalama, unasema Tanzania ni maskini?
Mitandao ya miundombinu iliyotandazwa hapa nchini, inayowezesha kusafirisha bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?
Kwa uchache tu nimeelezea namna ambavyo serikali imejitahidi kuwezesha kuwaletea wananchi maendeleo, kwa kutimiza wajibu wake, LAKINI SWALI LA MSINGI LA WEWE RAIA KUJIULIZA, UMETIMIZA WAJIBU WAKO?
Ukanda ni nini na kitambulisho chake ni kipi katika dhana nzima ya nchi. Zipi ni raslimali za nchi na zipi niza ukanda?.Dawa ni moja tu. Nchi igawanywe kila ukandaulinde resilimali zake,serikali kuu ipelekewe asilimia kidogo ya kuendesha nchi. Na viongozi serikali kuu wasiwe na mamlaka ya kubadili mikakati ya kiuchumi ya jimbo. Rushwa itapungua kwa asilimia 80% kama si 100%
Jibuni hoja,achane uongo uongo,huo unafuu wa matibabu unaouongelea ktk afya upi?Umezunguka vijijini ukaona jinsi Zahanati zilivyo na uhaba wa dawa?Au unaongea tu kwasababu uko mjini?Unazungumzia Tz ni kitovu cha amani,amani gani?Viongozi wa dini wanauwawa,makanisa yanachomwa,vita za Koo Mara,waandishi wa habari na raia wa kawaida wanauwawa na Polisi,halafu unasema kitovu cha amani.Acheni kuwadaa watanzania.Na 2015 mtaona ni jinsi gani watanzania tulivyoamka,na mtaona ni jinsi gani hizo porojo zenu zisivyopewa nafasi.Hii dhana ya umaskini wewe unaielezeaje?
Maana wakati mwingine mwananchi anaweza akawa anakosa mahali fulani, ili kuficha kosa lake lisionekane basi anainyooshea serikali kidole, na serikali kwa sababu ni mzazi inakubali tu lawama.
Hapa najaribu kukuonyesha kuwa, serikali imekuwa ikitoa fursa sawa kwa kila mwananchi kuondokana na hali ngumu ya maisha, ili utakubaliana na mimi HASWA kwenye elimu. Hapa wengi wetu pametusaidia sana kufika hapa tulipo maana tulizingatia elimu ambayo kimsingi ilitolewa kiusawa kwa wote bila kujali jinsia, udini, ukabila na hata ukanda.
Wengi wanaolia njaa humu JF na hata hao wa huko vijiweni ni kutokana na kupuuzia kitu kinachoitwa elimu, ikiwa ni moja ya sababu ya kujiletea maendeleo yako binafsi na jamii yako kwa ujumla.
Lakini pia kuna swala la afya na ustawi wa jamii, serikali kupitia sera yake ya afya, tumeona imetoa ahueni kwa watanzania walio wengi kuweza kupata matibabu na dawa katika vituo mbalimbali, japokuwa bado hali haijaridhisha lakini kwa namna moja hama nyingine, kuwepo kwa huduma hii nyeti kwenye eneo lako, basi kunakupa fursa ya kupata huduma za kimatibabu kwa gharama nafuu ukifananisha na isingekuwepo kabisa.
Swala la ulinzi na usalama, unasema Tanzania ni maskini? BASI UMASKINI TUNAJITAKIA WENYEWE, taifa linalotambulika ulimwenguni kote kuwa kisiwa cha amani, kwa juhudi zinazofanywa na serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, kwa kuwa na mbinu madhubuti za ki-intelijensia, watu wanatoka sehemu moja kwenda nyingine bila kubugudhiwa, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?
Mitandao ya miundombinu iliyotandazwa hapa nchini, inayowezesha kusafirisha bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?
Kwa uchache tu nimeelezea namna ambavyo serikali imejitahidi kuwezesha kuwaletea wananchi maendeleo, kwa kutimiza wajibu wake, LAKINI SWALI LA MSINGI LA WEWE RAIA KUJIULIZA, UMETIMIZA WAJIBU WAKO?
kama ni swala la kuachia ngazi kwa sababu ya rushwa basi itabidi mimi na wewe pia tuachie ngazi. Hata CCM wakiachia ngazi na wakaja wengine hiyo haitazuia watanzania kuomba na kutoa rushwa.Rushwa? Sasa serikali ya CCM inaendeleaje kuongoza taifa la wapenda rushwa? Kwa nini isiseme imeshindwa na iachie ngazi?
Mbona hujataja sifa moja muhimu sana
h. kuwa na watu wavivu wanaotegemea porojo za wanasiasa ziwaletee maendeleo.
.....

.......
Salaam wana JF!
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ni moja kati ya mataifa masikini sana duniani.
Cc: Ritz chama zomba Jichola3 ZeMarcopolo Nduka thatha Atongwele
......
kama ni swala la kuachia ngazi kwa sababu ya rushwa basi itabidi mimi na wewe pia tuachie ngazi. Hata CCM wakiachia ngazi na wakaja wengine hiyo haitazuia watanzania kuomba na kutoa rushwa.
Ni kweli kabisa watu wavivu porojo wakisaidiwa mikopo na taasisi hawataki kurudusha wakipewa maeneo ya madini kama wachimbaji wadogo wakipata madini hayo hukwepa kulipa kodi na kuwauzia wafanya magendo.
Hawa ndio watanzania na milele na milele tutabaki vilevile kutafuta mchawi wa umasikini wetu
Jibu lako ni RUSHWA. Watanzania ni wapenda rushwa. Kila mmoja anataka kujichumia zake. Na hili tatizo liko kwa wote sio CCM bali kwa watanzania wote.