Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Hilo la wazungu kuililia Tanzania ni kweli kabisa. Nimeshawahi kufanya kazi na wazungu toka Denmark na Sweden ambao walikuwa wanakuja Tanzania kwa mikataba ya miaka miwili na kuruhusiwa kuongeza mara moja mkataba wa miaka miwili mingine.
Wote waliokuwa wanakuja walikuwa wanaongeza mkataba kwa miaka miwili mingine na wote walikuwa wanataka waruhusiwe kuendelea kuishi Tanzania pamoja na sheria za mikataba yao ilikuwa hairuhusu hivyo. Wengine walikuwa wanaangusha mchozi kwa kuwa walikuwa wanaondoka Tanzania. Kilichokuwa kinatushangaza wengi tuliofanya kazi na wazungu wao ni kwamba nchi zote hizo ni matajiri na kiwango cha maisha ni cha juu mno kuliko hata cha Marekani, lakini bado walikuwa wanapenda kuendelea kuishi Tanzania.
Miaka ya karibuni nimekutana na wamarekani, waingereza, wacanada wanaoishi Tanzania ambao wanadai wao ndio wameshafika katika nchi ambayo wanataka kuishi for the rest of their lives, hawataki kabisa kurudi makwao, wanaenda makwao kutembea tu. Hivyo basi hilo la wazungu kuililia Tanzania ni la kweli kabisa
Na suggest the answer is both kwenye highlighted!mnakumbuka tulipokuwa darasa la kwanza au la pili tulikuwa tukiimba hivi:
Tanzania, Tanzania
nchi yenye mali nyingi
watu wengi wa ulaya wanaililia sana
niliona ndege wengi
chini wanatia fora
wanapendeza mlio kama mtoto wa nyumbani
my take:
jamani hivi ni kweli watu wengi wa ulaya wanaililia sana Tanzania , au watu wengi wa Tanzania wanaililia Ulaya.
pengine mafunzo haya ya toka elimu ya msingi ndo yamepelekea watu kuwa na mitizamo inayokinzana kuhusu mali zenyewe , je hizo mali ni wealth au ni natural resources?
Kwenye highlighted..Nadhani tofauti kubwa ya misemo yote hii miwili ilikuwa ni ktk tofauti za ARDHI na WATU..
Mheshimiwa rasi alikuwa akizungumzia WATU hali Mengi na Dr. Slaa walikuwa wakizungumzia ARDHI... sasa swala la kujiuliza kinachounda Tanzania ni ARDHI ama WATU!...
Sio tu kuiga mfano..Bali pia kuchagua viongozi wenye fikra kama hizo!Hakuna haja ya kuimba umaskini bila kuchukua hatua. Mengi aliona hiyo nafasi na kapambana kadri inavyowezekana kujiletea maendeleo yeye mwenyewe na jamii ya Tanzania.
Sasa ni wajibu wa Watanzania wengine pia kuiga mifano ya akina Mengi.
Mh Zitto..Did you mean kuwa kauli zote za Kikwete,Slaa na Mengi zinamaanisha "Tanzania ni nchi tajiri yenye watu masikini" ama ulikuwa unauliza if kauli zote kutoka kwao zina maana sawa?Tanzani ni nchi tajiri yenye watu masikini. Inajumuisha kauli zote za watu watatu Kikwete, Slaa na Mengi?
Jmushi1,
Statements zote ni sahihi, Tanzania na Afrika kwa ujumla ni tajiri kwa maana ya resources kama ardhi, madini, mafuta nk. Lakini watu wake ni maskini kwasababu tumeshindwa kutumia akili zetu kutengeneza added values kutoka kwenye hizo resources zetu.
Umaskini uko kwenye vichwa vyetu, akili zetu, fikra zetu nk. Hata tukipata uongozi bora sana bado itachukua miaka mingi kwa Watanzania kuwa matajiri. Ni rahisi kubadili uongozi lakini ni ngumu sana kubadili culture ya uvivu
na kutokuwajibika ambayo imejengeka Tanzania na Afrika. Sisemi Waafrika ni wavivu, maana wakija huku nje wanajituma kweli kweli.
Culture yetu ndio ya kimaskini, culture ya kukimbilia majibu rahisi na common sense. Culture ambayo haitufanyi tukae chini na kuwaza nje ya our comfort zone. Kuibadili hii itatuchukua muda mrefu sana na juhudi kubwa mno kuanzia level ya individuals mpaka kwenye viongozi wa nchi.
Ndio viongozi wa Afrika wameiba mabilioni ya resources zetu lakini mimi siamini kama ndio chanzo cha umaskini wetu. Matatizo yetu yanaenda ndani zaidi. Mwalimu Nyerere alijaribu kushughulikia kiini cha matatizo ya Watanzania lakini bahati mbaya akachagua siasa mbaya na chama kushika hatamu mpaka ikafikia mahali ambapo hakuwa challenged na hivyo kudumaa kama viongozi wetu wengine.
Tujikwamue?Nimekubaliana na mengi hapo juu, upanuzi mzuri walakini...
nabaki kujiuliza -Tunaweza kujikwamua vipi na hii culture
Kauli ya mh Rais the same day akisema kuwa sisi ni masikini huku akishauri gharama zisipewe kipaumbele bila kujali kama upandishaji gharama huo utamnufaisha mkandarasi ama utainufaisha kazi/tenda na kuona kama gharama zinaendana na quality ya kazi pamoja na mazingira ya utoaji wa tenda hizo!Hakuna sababu wizara, TANROADS kumchagua mtu mwenye hesabu ndogo, mnapotangaza tenda lazima kuangalia kama kazi ataiweza, ingawa wale watakaokosa watasema mnajali mafisadi,... hayo msiyajali?,`` alishauri.
Nakumbuka hili suala alisha lisema balozi wa Sweden Tanzania, kuwa jamani akilinganisha mali walizonazo Tanzania na Sweden Tanzania ina laslimali za kutosha.
Lakini vile vile Sweden yenye mali kidogo bado inaendelea kuisupport Tanzania.
Kwa hiyo unaweza kuona jinsi hata na watu walioko kwenye diplomasia wanavyoona jinsi tulivyo matajiri.
Tatizo kubwa la Taifa letu ni uongozi mbovu, sheria mbovu zilizokaa kinadhalia kuliko vitendo, Rushwa(ambayo inachochewa na uongozi tulionao).
Haya yote ndiyo yanarudisha maendeleo ya mtanzania nyuma hivyo kuitwa masikini.
Suala la Jk kusema hivyo nafikiri tuna kiongozi aliyekuwa anajua fika matatizo ya wananchi mara tu alipopata madaraka akasahau.
JK alisha ulizwa kwa nini nchi yako ni masikini? Angeulizwa swali hili kabla ya kuwa mkuu wa kaya angemwaga data za kutosha lakini tangia awe president hata suala dogo kama hili linamshinda.
Sishangai maana yeye sasa ni mdau katika kuwafanya watanzania masikini.
Hilo la wazungu kuililia Tanzania ni kweli kabisa. Nimeshawahi kufanya kazi na wazungu toka Denmark na Sweden ambao walikuwa wanakuja Tanzania kwa mikataba ya miaka miwili na kuruhusiwa kuongeza mara moja mkataba wa miaka miwili mingine.
Wote waliokuwa wanakuja walikuwa wanaongeza mkataba kwa miaka miwili mingine na wote walikuwa wanataka waruhusiwe kuendelea kuishi Tanzania pamoja na sheria za mikataba yao ilikuwa hairuhusu hivyo. Wengine walikuwa wanaangusha mchozi kwa kuwa walikuwa wanaondoka Tanzania. Kilichokuwa kinatushangaza wengi tuliofanya kazi na wazungu wao ni kwamba nchi zote hizo ni matajiri na kiwango cha maisha ni cha juu mno kuliko hata cha Marekani, lakini bado walikuwa wanapenda kuendelea kuishi Tanzania.
Miaka ya karibuni nimekutana na wamarekani, waingereza, wacanada wanaoishi Tanzania ambao wanadai wao ndio wameshafika katika nchi ambayo wanataka kuishi for the rest of their lives, hawataki kabisa kurudi makwao, wanaenda makwao kutembea tu. Hivyo basi hilo la wazungu kuililia Tanzania ni la kweli kabisa
Swali jingine la kujiuliza, je ni kipi muhimu kuwa nacho, utajiri wa rasilimali pamoja na uongozi mzuri au kinachohitajika ni uongozi mzuri tu na mengine yatajipa yenyewe?
Nauliza hivyo kwa sababu wakati mwingine nashindwa kabisa kuelewa ninapoangalia nchi kama Japan (the second largest economy) na maendeleo waliyonayo ukizingatia historia (II WW) na rasilimali walizonazo. Juzi nilikuwa naangalia documentary fulani hivi iliyokuwa inaelezea maendeleo ya Japan ktk miaka 30-40 iliyopita. It's remarkable what they have done given their meager (meagre) natural resources.