KUWEZESHWA KUWEZESHANA NA KUTOPENDA VYA KWETU NI CHANZO CHA UMASIKINI
Sehemu ya umasikini tulioao inatokana na kasumba tuliyokaririshwa na kuikubali kuwa
eti bidhaa zetu sio Bora. Hiiinapigiwa msumari na biashara huru na ya ushindani amabapo hakuna mpango maalum wa kupendelea na kuzibeba bidhaa zetu nyumbani.
Inachekesha pia kuna hata watu wanabeza "ubora" wa bidhaa za china dihidi ya zile za magharibi kumbe unaweza kuacha kununua vigae vya Tanzania na china kwa kuwa eti s bora ukanunua vya spain amabvyo vimetengenzwa kwa teknolojia ya china .
Nakumbuka zamani sana tulichekwa na kuonekana MASIKINI kwa Kuvaa viatu laba za "DH" zilizokuwa zinatngenezwa na kiwanda cha bora . Lakini leo hii eti ni fashion kwa kuwa tu viatu aina hizo vinavaliwa na akina "nanihii" wa majuu. Mtu yuko tayari kununua design ya yenye nembo ya NIKE ya USA lakini sio DH ya Bora ya Tanzania........ kwa hiyo tuko radhi kuwatajirisha wenzetu........
Kwenye majukwaa ya siasa viongozi wanaimba tupende na tununue bidhaa za Tanzania. Lakini ni viongozi wachache wanaishi hivi. Sidhani kama kuna mbunge yuko tayari japo katika seti zake za suti ashoneshe tatu kutoka wa fundi wa jimboni/wilayni kwake ili asaidie kundoa umasiikni na kukuza ajira..
Sababu ya kisingizio cha ya "ubora" wabunge wengi utakuta wanaagiza suti za italy na kama kuzinunua Tanzania basi wanazinunua Dar sio wilayani au mikoani kwao.. So unakuta mbunge au iongozi ya matumizi anayofanya hata 10% haitumiki eneo lake. Mwingine wa kuwa ni kingozi anaona sio level yake kununua vitu kwenye soko la local. anapoishi
Ukiondoa vingozi na wanasisa kama wabunge nadhani hata sisi "watu wa kati" wengi tunaamini ni kujishusha hadhi kuchongesha viatu japo pair mbili au tatu kwa mwaka kwa fundi wa mtaani.
Kuna vitu vidogo mtu mmoja mmoja anaweza kufanya vikasiaida kundoa umasikini kwenye jamii . Mfano wa vitu vyenyewe ni kama hivyo viatu na nguo. Naamin wanasiasa na vingozi wakiwa mfano watu watafuata. Mandela shirt iilipata sifa na inajulikana dunia nzima sababu ilipromotiwa na kiongozi. Sababu ya image ya mandela ikapata soko ubwa ndani na nje ya nchi. sasa sisi viongzi wetu wanatakiwa watafute jinsi ya kupromote vya kwetu.
Itapendeza watu wajue au watangaziwe kuwa katika suti na mavazi anazovaa jK zimo chache zimetengenezwa na Khadija mwanamboka . Au itapendeza vijana wajue katika suti au viatu wanavyovyaa kina Zitto kabwe au January makamba au Mnyika chache kati yake zimeshoneshwa au kutengenezwa na fundi Masawe wa Sinza au Fundi Zuberi wa Ubungo au dada Kalumanzila wa Mwandiga Kigoma.
Kwenye picha ya Ikulu Rais wetu aliyopiga na viongzi walikuwa wakikutana kuhussu mchkato wakatiba mpya zaidi ya uatza sura nilijaribu kupepesa na kujilza je kaitika kile chumba
WHAT IS MADE or DESIGNED IN TANZANIA . Mpaka leo napenda kujua je zle sanamau na picha za kuchora za ukutani zimetoka nje. Kama ni za mtanzania ni kazi ya msanii gani tumpe sifa.....
Tunaweza kukubali iasi kuwa Kwa tanzaia hakuna anayeweza kudesgn na kutenegza milango ya ikulu au hakua anayweza kutengeneza zulia la ikulu au samani viti nameza za ikulu haziwezi kutoka wa mafundi wa keko............
Lakini kama tungekuwa tunajitambua basi zingewekwa level ili wajsirimali wa ndani wajijue ni wapi wana nafasi ni wapi hawana .
OK let say si aibu ikuu i inaagiza 90 % fenisha kutoka china. Lets say ni aibu kidogo pia Wizara zinaagiza 90% ya viti na meza kutoka china. Lakini ni aibu Ofisi za Mikoa na wilaya zinaagiza 90 % ya viti na meza kutoka china na hata Ni aibu kubwa zaidi ofisi ya mbunge asiyotumia sana . anaaagiza viti 90% na meza kutoka china . Hivi itakuwa kosa l kimataifa tukitengea kuwa kuanziangazi ya wilaya au Mkoa asilimia (%) fulani ya tender ipatikane wa bidhaa na wazalishaji kutoka nchini.
So utaona wakati wanasiasa wetu wanaongea mambo ya ajira na umasikini kwenye majukwaa lakini maamuzi na vietendo wanavyofanya na kusiamami , na maisha wanayosihi hayaendani maneno yao
Mbunge akishonesha suti mbil au tatu kwa fundi jimbon ikwake kila mwaka atasaidia kuondoa umasikini kuuza ajira na hata kungeza ubora na ufanisi wa yule fundi...
Na sisi mimi na wewe tuna mtazamo gani na bidhaa zinazotengenzwa Kubuniwa na kuzalishwa na watanzania wenztu.......