Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Tumezungumza mengi sana kuhusu umaskini wa Mtanzania na nadhani kwa mapana yake tumekubali kwamba nchi yetu ni tajiri kati ya nchi matajiri duniani lakini tumeshindwa kabisa kutumia nafasi, mtaji na vipaji vyetu kuweza kuutumia utajiri huo kwa faida ya wananchi au hata Taifa lenyewe.
Sasa kinachofuata ni - TULIKOSEA WAPI? ni wakati gani tumefanya maamuzi ambayo yanaendeleza hali hii iliyopo maana kama tutarekebisha hicho ama hivyo kutajenga tumaini jipya kama tulivyokuwa wakati tunaingia Ubepari mwaka 1985 na nakumbuka vizuri sana furaha tulizokuwa nazo. Leo tumepoteza kila kitu ni mateka wa kifikra na Utaifa, hatuna uzalendo wala tumaini tena kibaya zaidi hadi roho za watu zimejenga chuki na unafiki kiasi kwamba tumerudi nyuma hadi kifikra na imani za uchawi zimeshehena vichwani mwa kila mtu - WHAT'S WRONG?
Tatizo kubwa ni IGNORANCE mtalumbana miaka mianane na hizo policies, mapendekezo na mengineo mengi mnayobishania hapa ni kazi bure hiwapo watekelezaji hawana uwezo na mtaendelea kuwachagua sijui kupitia baba zao, hela za campaign na upuuzi mwingine uliojaa kwenye chaguzi zetu.
What you need foremost ni katiba yenye kuweka misingi ya uongozi na sheria yenye msumeno, ikiweka usawa kuanzia campaign za uchaguzi (we umeona wapi duniani watu wananunulia wapiga kura ubwabwa) zaidi ya third world countries hiyo ni bribery tu; na kuja kumalizia sheria yenye msumeno wa ukweli, kupunguza nguvu za baadhi ya viongozi na taasisi (the need for the balance and checks). Vinginevyo hata akija mtu mwenye miakili kama ya 'Gordon Brown' hataishia kuwa mwizi asilimia kubwa ya binadamu bila usamizi uishia kuwa na tamaa. Hata Nyerere ingawa hakuwa na tamaa na mali, lakini alikuwa na tamaa ya uongozi kwa hivyo kuweza kuwa comfortable na uongozi wako unahitaji wajinga wengi kwenye jamii na kuweka viongozi wasio wasomi wa vile karibu.
Ndiyo Khali maisha ni learning process. Ngoja niendelee kulia.