Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Katika mambo ambayo binafsi huwa sielewi chanzo chake, basi mojawapo ni umasikini na lingine ni utajiri. Maneno haya hunichanganya sana hasa ninapoangalia nchi zetu za kiafrika. Huwa najiuliza hivi utajiri unapimwa na nini? Je umasikini hutambuliwa na nini? Je ni kweli umasikini upo? Na kama upo nani kauleta? Kwanini? Wapi? Na lini uliletwa?

Kwa muda mrefu sana nimejiuliza maswali haya. Kuna kipindi huwa naamanini kuwa umasikini na utajiri vyote hutengenezwa na binadamu kwa manufaa ya binadamu. Mwanafalsafa wa Ujerumani amewahi kuandika kuwa binadamu hutengeneza historia yake mwenyewe lakini nguvu kutoka nje humfanya binadamu kutengeneza historia kinyume na matwaka yake.Katika hili Karl Marx hakuiandikia jamii ya kiafrika lakini aliyoyaandika leo ndiyo yanaonekana Tanzania na Afrika kwa ujumla. Binafsi pia naamini kuwa maisha ni kutengeneza historia tusiyoitaka, historia ambayo hatujawahi kuifikiria.

Historia inaonesha kuwa kabla ya karne ya kumi na tano Afrika na Ulaya zilikuwa sawa kimaendeleo lakini baada ya karne ya kumi na tano mambo yakawa kombo kwa Afrika na kule ulaya hali ikawa shwari.Si lengo langu kufundisha historia leo lakini naamini kuwa historia ya Afrika leo inatushitaki waafrika wenyewe. Wazungu walipokuja na kututawala waafrika, walikuja na mila na desturi zao na kufanya waafrika tusahau utu wetu NA KUKUMBATIA UGENI WA WAGENI HAWA.

Hapa ndipo tulipofanya kosa kwa kumkaribisha mgeni huyu si sebuleni bali tuliamua kuonyesha ukarimu (ujinga) wetu na kuamua kumkaribisha mpaka vyumbani mwetu na tukampa wake zetu kwani huo ndio ustarabu wa MWAFRIKA!!! Matokeo yake leo ni kilio na kusaga meno, vita visivyoisha, migogoro, maandamano na migomo isiyo na kikomo. Hii yote imesababishwa na ustaarabu na ukarimu wetu wa kumuachia mgeni ale chakula chetu kizuri huku sisi tukishindia maji ya kunywa na karanga mbili tatu.

Ustaarabu wetu ndio unaotufanya tuogelee kwenye bahari ya umasikini huku tukiwa tumekaria utajiri wa kutosha. Mtaalamu mmoja wa masuala ya uchumi bwana Nurkse anadadafua kuwa
“a society is poor because it is poor” yaani jamii ni masikini kwasababu ni masikini au kwa maana nyingine jamii ni masikini kwa sababu ya umasikini wake.

Kimsingi Tanzania ni masikini kwasababu ya umasikini wetu. Umasikini ninaozungumzia hapa ni umasikini wa kufikiri ambao ndiyo zao la ujinga. Watanzania sio “ creativity” na ndiyo maana tunatukuza ugeni na kuukataa uenyeji. Sisi ni watu wa kucopy na kupaste tu. Angalia vijana wa kileo huwaambii kitu kuhusu vimini, pedo, suruali zinazoonyesha maungo ya miili yao na vitopu vinavyoacha robo tatu ya mwili wazi ( kina dada) kinakaka wao ndio wameishiwa kabisa kwani wao ni walevi wa starehe, kuvaa suruali chini ya kiuno, kusuka ndicho wanachoweza, ukiuliza unaambiwa ndio kwenda na wakati. Ifahamike kuwa wakati tunahubiri kwenda na wakati akili zetu pia zinakwenda na maji matokeo yake ni ujinga unaoplelekea kuwa na mawazo ya kimasikini? Je kwa mantiki hii umasikini unatengenezwa au hautengenezwi? Kama kijana ni samadi ya taifa, taifa linaelekea wapi kwa hali hii? Nani wakuendeleza taifa? Ni hawa wanaokwenda na wakati au wengine? Wako wapi waokozi wa taifa hili JAMANI!!!?

Nikirudi kwa ndugu zangu wasomi aaahaaa!! Uozo mtupu!!! Hawa ndiyo kabisa wameathirika na utandawazi hadi vichwa vyao vimekuwa wazi. Utandawazi umeharibu kabisa malengo chanya ya elimu ambayo baba wa taifa aliyaainisha katika kitabu chake cha ujamaa ambapo anaeleza “Elimu katika nchi yoyote duniani ni kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine maarifa na mila za taifa na kuwaandaa vijana wawe tayari kuchukua nafasi zao katika kulitumikia na kuliendeleza taifa. (ujamaa uk , 43) Je! Elimu ya Tanzania ina malengo yapi? Je! Elimu yetu inarithisha maarifa na mila za taifa kwa maendeleo na manufaa ya taifa? Au ndiyo kwanza inatufanya tuwe mabingwa wa kwenda na wakati? Au ndio chanzo cha mafisadi papa na mafisadi nyangumiiii? Kimsingi elimu ambayo haina shabaha ya kuendeleza taifa si elimu bali ni ujinga unaopelekea umasikini wa jamii na taifa kwa ujumla. Je kwa mantiki hii tutapata wapi wasomi watakao likomboa taifa hili?

Tanzania yenye neema ipo, tena ipo mikononi mwetu, akilini mwetu na majumbani mwetu. Ili kuipata Tanzania hiyo, hatuna budi kubadili mfumo mzima wa elimu hasa serikalini kwani mwanafalsafa mmoja aliwahi kuandika kuwa “the government tend not to solve problems but only rearrange them…” Yaani “serikali haina tabia ya kutatua matatizo bali kuyapanga upya” ( tafsiri ni yangu) hivyo hatuna budi kuishinikiza serikali sasa ijipangie utaratibu wa kutatua matatizo na siyo kuyapanga upya. Hili linawezekana ikiwa tu tutaweza kuwapata viongozi wasomi wenye shabaha ya kweli ya elimu siyo hawa wasasa wasiotaka mabadiliko

Tatizo sugu lililopo kwa viongozi ni kutokubali ukweli. Viongozi hawa ndiyo zao la elimu yetu ya Tanzania na kupitia viongozi ndipo tunaweza kujua kama shabaha ya elimu ya Tanzania ni sawa na ile aliyoizungumza baba wa taifa. Viongozi hawa ambao ndiyo wasomi wa leo ndiyo walioko mstari wa mbele kukumbatia wageni, ndiyo wanaoongoza kwa kashfa zisizo na idadi, ndiyo wanaongoza kusaini mikataba kama ya kina chifu Mangungo na Karl Peters. Leo hii viongozi hawa ndiyo wakwanza kuchekelea pale wanapomuona mwananchi wa kawaida anapohangaika katika umasikini. Nikiangalia wayafanyayo viongozi hawa huwa nashindwa kuamini kama kweli hawa wamerisishwa maarifa na mila za taifa ili kuliendeleza taifa.

Kimsingi viongozi wetu hawapo nasisi tena, badala ya kujenga daraja wao wametumia kura zeu kama mtaji wa kujenga ukuta ili kuwa mbali na sisi, wameamua kujenga ukuta ili kuficha yale mabaya wafanyayo. Kwa mujibu wa nadharia ya Plato anaeleza kuwa kiongozi mzuri ni yule aliyesoma, kiongozi ni yule anayetumia elimu kutatua matatizo ya wananchi, kiongozi ni yule anayetumia elimu kuweza kutambua wananchi wake wanataka nini? Kwa wakati gani? Na kwa namna ipi?

Plato hakuishia hapo anaendelea kuelezea kuwa kiongozi mwenye elimu ni yule aliye tayari kufuata utawala wa sheria, aliyetayari kusikiliza wananchi wanataka nini, Plato anamalizia kwa kueleza kuwa kiongozi mwenye elimu yuko tayari kufanya kazi kwa namna yoyote ile kwa maslahi ya taifa na siyo kwa maslahi yake binafsi. Katika hili Plato anatuonya juu ya viongozi wanafanya mambo kwa maslahi yao binafsi. Je! Viongozi wetu wapo katika msimamo upi wa Plato? Je ni kweli wanafata yale yayotakiwa kufanywa na kiongozi kama yalivyoainishwa na Plato? Kama hawafanyi je elimu wakiyopewa na watanzania ina shabaha gain kwao?
Ukistaajabu ya MUSA kweli hutayoona ya FIRAUNI, wasomi wetu wa leo ndiyo hawa waliotayari kupiga marufuku maandamano ya wanafunzi na walimu kwa kile wanachodai kuwa wanamadai yasiyo ya msingi, wasomi wetu ambao ndiyo viongozi wetu wako tayari kufungia vyombo vya habari kwa kile wanachodai kuwa vinapotosha umma, wasomi wetu ambao ndiyo viongozi wetu wako tayari kusaini mikataba ya madini inayoliingizia taifa hasara zaidi ya dola milioni 20 kila mwaka. Wasomi hawa hawa ambao ndiyo viongozi wetu wanamuona mtu yeyote kuwa adui pale tu anapoamua kusema ukweli. Je! Kwa hali hii ni wasomi gani watakaolikomboa taifa? Ni wasomi gani wenye uwezo wa kutambua nini wananchi wanataka?

Kuna haja kubwa sana ya kubadili sekta hii ya elimu kwani kimsingi sekta hii imekufa na kuoza. Malalamiko yote yaliyopo yanayoelekezwa kwenye sekta ya elimu na mambo yote yanayofanywa na viongozi ambao ndiyo matokea ya sekta hii ni ishara tosha kuwa sasa mabadiliko yanahitajika kama kweli tunataka kulikomboa taifa na hii haihitaji shahada wala stashahada kulielewa.

Ifahamike kuwa mabadiliko katika sekta hii ambayo binafsi naiona ni muhimu kuliko sekta zote ikifuatiwa kwa ukaribu sana na sekta ya afya kutaleta na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa wananchi na kufyeka kama siyo kuondoa kabisa bahari ya ujinga nchini mwetu. Maendeleo ya taifa lolote huletwa na wasomi, je kama tusipowekeza katika elimu tutapata maendeleo kweli? Au ndiyo tutakuwa wasindikizaji katika mbio ndefu za kusaka maendeleo huku tukiwa tumelalia vitega uchumi vingi kuliko nchi yoyote duniani.

Badala ya kuwekeza katika elimu yenye shabaha ya kuliendeleza taifa, tunaamua kuwekeza kwenye malumbano ambayo kimsingi yahana kichwa wala miguu. Tuko tayari kupigana na mtu anayetaka kupunguza ulaji wetu badala ya kupigana na ufisadi ambao ni chanzo cha umasikini unalitufuna taifa hili bila huruma. Haiingii akilini kung’ang’ania Tsh. 200,000 kwa siku wakati mama yako anayefundisha shule ya msingi anapewa Tsh.250,000 kwa mwezi, baba yako askari analipwa si zaidi ya Tsh. 300,000 kwa mwezi, wakati huo huo dada yako anashindwa kumlipia mwanae anayesoma sekondari Tsh. 20,000 kwa mwaka na mtoto wako aliyeko chuo kikuu anapewa Tsh. 7,000 kwa siku bila kuangalia gharama za maisha zilivyopanda Je! Huu ndiyo ukarimu na ustaarabu tulionao watanzania? Tumewapa viongozi kura zetu wakatusemee au wajinufaishe?

Tubadilike, tuijenge nchi. Tuwe na roho ya huruma kama kweli sisi ni ndugu, tuwe na upendo kama kweli tunataka amani, tuwe wastaarabu kama kweli tunataka heshima, tuwe na mshikamano kama kweli tunataka umoja na mwisho tuwekeze katika elimu, tuingie darasani, tusikilize mawazo ya wengine kusaka maarifa mapya kama kweli tunataka maendeleo na kuipata Tanzania yenye neema. TANZANIA YENYE NEEMA IPO.


Waheshimiwa wananchi naomba kuwasilisha.
 
WIKI kadhaa zilizopita nilialikwa katika mkutano wa vijana uliofanyika Arusha, ambako nilikwenda kama mzungumzaji.

Katika mazungumzo yetu, kijana mmoja aliuliza swali kuhusu sababu za Tanzania kuendelea kuwa taifa masikini.

Bila shaka hata wewe unayesoma makala haya, ni kati ya Watanzania ambao wamekuwa wakijiuliza; kwa nini Taifa hili bado ni duni? Achilia mbali Tanzania bara ambalo ni eneo kubwa, vipi kuhusu eneo dogo kama Zanzibar?

Unakuta eneo fulani lina utitiri wa viongozi kuanzia balozi wa nyumba kumi, Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa, Mtendaji wa Kata, Diwani, Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa Halmashauri na viongozi wengine, lakini bado eneo linaendelea kuwa duni. Tatizo ni nini?

Hivi ni kwa nini maeneo mengi ya Zanzibar kasi ya wasio na ajira ni kubwa, wakati kisiwa hicho kikiwa na wakazi wachache? Ni swali ambalo kila mwenye akili timamu anaweza kujiuliza.

Hata Tanzania bara, bado tunaweza kuendelea kujiuliza kwa nini hali ya maisha ya walio wengi ni duni wakati tumekuwa tukiahidiwa mengi hasa nyakati za kampeni?

Nafikiri shida kubwa iliyoko Tanzania ni kushindwa kuthubutu; kuna Watanzania wengi ambao hawajiamini kuanzisha mambo.

Kwa mfano, wahitimu wengi wanafikiri kilicho muhimu kwao ni kuajiriwa. Mtu anaweza kusomea sheria, lakini yuko tayari kufanya kazi hata ya kuuza duka kwa sababu ndio kazi aliyopata ya kuajiriwa.

Wengi wanafikiri kuajiriwa ndio maisha lakini tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa watu ambao maisha yako yote wanategemea ajira, ndio ambao hufa wakiwa maskini.

Kwa nini? Nakubaliana na hili kwani ni ukweli kuwa baada ya kumaliza ajira, kinachofuatia ni kupewa posho zako na kurudi nyumbani. Hakuna njia nyingine ya kuweza kuishi zaidi ya kusubiri kifo, huku ukila mafao yako.

Hata kama wewe ni Mbunge, Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa, kazi hiyo bado haina chochote kama hutakuwa na kitu kingine cha kufanya.

Kuna watu ambao walikuwa wakuu wa wilaya, leo hii wanafanya biashara ya mama ntilie. Kuna watu walikuwa wana fedha, leo hii hata nauli ya daladala kwenda huku na kule ni shida.

Ndugu yangu ni lazima kuwa makini na kufikiria kuanzisha miradi yenye maana. Miradi mizuri zaidi, miradi ambayo inaweza kweli kusaidia kukufanya kuwa na mafanikio zaidi.

Ni vigumu kufikiri kwamba unaweza kuwa na maendeleo makubwa, ikiwa fikra zako za aina ya miradi ni kuhusu miradi yenye kukuletea mafanikio madogo.

Ni kwamba unaweza kuanza kwa miradi yenye fedha ndogo, nikimaanisha kwamba anzisha mradi kulingana na fedha ulizonazo, lakini lililo la msingi ni kuangalia aina ya miradi ambayo inaweza kuleta mafanikio makubwa zaidi mbele.

Ninachotaka kueleza hapa ni kwamba sababu kubwa ya Tanzania kuendelea kuwa maskini ni wananchi wenyewe kutokuwa na uelewa wa nini ambacho wanatakiwa kufanya ili kuwa na maendeleo. Katika hili inawezekana hata walio madarakani nao hawakuwa na uelewa juu ya hilo.

Hata baada ya baadhi ya viongozi kuanza kufahamu umuhimu wa namna ya kuwafanya wananchi kuwa na maendeleo ya haraka, wengi walishindwa kufanya mikakati hiyo kwa staili inayotakiwa.

Uongozi usiofaa au viongozi wasiofaa, kwa maana ya kuwa na watu ambao wanashindwa kuwaendeleza wengi, ni kati ya sababu za msingi za kudumaa kwetu kimaendeleo.

Kwa nini tumsifie mwalimu kuwa anajua kufundisha ikiwa idadi kubwa ya wanafunzi wake wanafeli mitihani?

Hata kama labda mtoto mwenyewe anayefundishwa, kichwani anasumbuliwa na kero nyingi na kusababisha ashindwe kusoma vizuri, bado hatuwezi kusahau mchango wa mwalimu kwa kufeli mwanafunzi huyo.

Ndiyo maana nasema kwamba umasikini unaoendelea Tanzania unachangiwa na viongozi wasio na huruma na wananchi. Hawana mikakati mahsusi katika kusaidia maendeleo katika maeneo wanayoyaongoza.

Aidha, Watanzania wengi bado ni wazito katika kupambanua mambo. Msingi hasa wa kuwa na maendeleo ni pamoja na kutokuwa na urafiki wa kudumu au uadui wa kudumu na wanasiasa.Mataifa mengi yaliyoendelea tabia zao ni kwamba hawana urafiki wa kudumu wala uadui wa kudumu.

Kwa mfano, kinachoendelea Zanzibar sio sahihi hata kidogo, kwamba kila uchaguzi, ni lazima kuona Pemba inachukuliwa na CUF, Unguja inachukuliwa zaidi na CCM. Au hata kwa Tanzania bara, ni makosa mno kukubali kuendelea kukipigia kura chama fulani miaka nenda miaka rudi.

kwa mfano, kama katika uchaguzi uliopita ulikipigia kura Chadema, TLP au CCM, ni muhimu katika uchaguzi ujao, kumpima kiongozi alifanya nini kabla ya kupiga kura yako.

Kama hajafanya chochote, hakuna sababu ya kukipigia kura wala kumpigia kura mgombea wake ambaye ameshindwa kutekeleza ahadi alizotoa katika uchaguzi uliopita.

Chanzo: hapa
 
kibaridi mbona umejijibu swali lako.
hatuna cha kuchangia.
 
Heading ingekuwa "Sababu ya watz na tz kuwa masikini" ingeleta maana ya stori nzima
 
kwani sababu ya wakenya kuwa masikini nin nini...wakenya mbona mbunye sana hawa, yaani umasikini wa machokoraa kula majalalani, umasikini wa wapwani waliowatenga hadi leo wanataka kujingátua, umasikini wa maeneo yote isipokuwa nairobi hauoni, anakuja kutuchunguza sisi wabongo...haujauona umasikini wenu? nyine wakenya mnaangalia vya wenzenu tu kumba madudu ya kwenu hamyaoni...nyani haoni kundule...akili kubwa ya mkenya huwa anajiona yeye nchi yake imeendelea sana, nchi yake ni tajiri, nchi zingine ni masikini...ni ujinga wa kupindukia,,,hata mjusi au kenge angebadilishwa kuwa mkenya, asingekuwa na akili kama za hawa nyangáu....after all, huwa nafurahia kuwatungua kwa risasi pindi tunapowawinda kama majambazi wakija kwetu arusha kuhemea....majambazi wakubwa nyie...
 
Watz niliweka makali hii ili tuangalie kwanini umaskini unazidi Afrika mashariki. Hute munasema eti CCM ndio jinamizi inayoila TZ na kueneza/kusambaa haraka kwa umaskini. Mimi naona hii dhana ni kinyume. Alivosema Mw. Nyerere, mungu amlinde peponi, kila mkenya ni "nyangau" na lazima atupiwe macho/darubini. Hii ndio "mindset" ambao inaila Tz kama cancer. Mtz amesalia tu kuona mtu ambaye hana uraia wa tz kama "nyangau"

..........kwanza Kwa nini tusiseme umaskini tz /umeenea kwa kukosa ushirikiano, hasa katika misingi za elimu/kusawazisha/kustandardize, kuboresha/privatization ya usambazaji wa huduma muhimu ambazo serikali ya siku inshindwa kutekeleza. Hapo ndipo private sector huingilia kuziba ufa. Mbona tusiwaachie waafrika nafasi bila kujali uraia wake, maana tunaotegemea wazungu, tumegundua ni wanyonyaji. Waganda hapa wanapiga watz bao ikija kwa masuala ya kushirikiana au kuiga miradi ya maendeleo. Mimi sikutaka tujadili mengi lakini kuna sehemu ambayo inahuzunisha.

Baada ya jubilee, bado waliohitimu wameshindwa kupata ajira kutokana na mafunzo waliopata vyuo vikuu..........Mtu ambaye ana shahada la sheria, anaingilia kazi ya kuuza dukani....Swali ni alienda chuoni kupokea shahada kwa lengo gani? .............Afadhali angetumia pesa hizo katika matumizi mengine, labda akanunue shamba na mifugo ya kulea.................. Hii picha ina maanisha nini kwa kuzingatia umoja wa EAC?
 
the point is, wewe masikini na chokoraa wa kenya, una ubavu gani kuja kujadili umasikini wa tz wakati umasikini wa kwako umeuacha kule kenya?....ondoa kamasi zako hapa, hua point....shughulikia matatizo yako kwanza, ndio uje kwa haya ya kwetu kama bado yatakuwepo.......
 
Kabaridi acha uchokozi, tafadhali nenda ukaimarishe ile sub-forum mpya tuliyowatengenezea...
Bantugbro, huu si uchokozi....Ni hali ya kujaribu kujadili kiustarabu..Na niseme wazi mijadala kama hii huaribiwa na watu wasio na hoja...Nitaweka makala ya umaskini kenya baada ya uzi huu...lakini kwanza wacha tujadili TZ.
 
Last edited by a moderator:
the point is, wewe masikini na chokoraa wa kenya, una ubavu gani kuja kujadili umasikini wa tz wakati umasikini wa kwako umeuacha kule kenya?....ondoa kamasi zako hapa, hua point....shughulikia matatizo yako kwanza, ndio uje kwa haya ya kwetu kama bado yatakuwepo.......
Hute wewe ni mmoja wa watz ambao munadhihirisha uzalendo thabiti lakini ambao haujakomaa...Kuna pointi ambazo tunaeza jifunza na siyo kujaribu tu kuharibu mijadala...This is a very weak character kutoka kwako na naomba kuwa baadhi ya watu kama ninyi tz ni wachache.
 
Bantugbro, huu si uchokozi....Ni hali ya kujaribu kujadili kiustarabu..Na niseme wazi mijadala kama hii huaribiwa na watu wasio na hoja...Nitaweka makala ya umaskini kenya baada ya uzi huu...lakini kwanza wacha tujadili TZ.

Haya Mkuu, tunasubiri uweke hiyo ya umaskini wa Kenya maana hii ya TZ haina wachangiaji wengi.:sick:
 
tatizo watanzania wengi hasa wa vijijini bado hawajaelimishwa vizuri kujua haki yao ya kimsingi. Tumeshazoea uonevu na kukubali kila kitu tunachoambiwa. Mtu anaona yeye kwa vile ni ccm basi lazima uchaguzi ampe kura ccm au chadema hivyo hivyo. Nchi za ulaya utakuta mtu ni mwanachama wa chama fulani lakini wakati wa uchaguzi kama anamuona mgombea wa chama chake hafai basi atachagua mgombea wa chama kingine ambae anamuona anafaa. Hiyo kitu inabidi iingie kwenye akili ya watanzania kutumia haki yao ya kupiga kura vizuri na waache kulainishwa na baiskeli,khanga na shs 10000
 
na hatutaki hio sub forum ya Kenya, if we want to discuss issues with Kenya we post at Kenyan sites, hapa jf tunataka kujadili na watanzania. kama mnatufukuza mtupatie permanent ban, hii yakutufukuza polepole hatutakubali
 
Kwanza tuna viongozi :-
1. Wasio na uchu wa maendeleo
ukiachia mbali mwl nyerere na mzee ruksa, kuanzia kipindi cha mkapa tumekuwa na janga la kitaifa. Kwa kuwa na viongozi wafanya biashara na wanajikuta kushindwa kuwachukulia hatua wa chini yao kwa hofu ya kuanikwa mazambi yao.

Matokeo yake wote wanakuwa wezi kuanzia juu mpaka chini, makusanyo ya kodi na kila kitu wanajimilikisha- serikari inakosa fedha.

2. Viongozi wasio na vision wala mikakati ya dhati kuwakombowa watz, mkukuta, mkurabita, kilimo kwanza, wizi tu!!

3. Hawako teyari kuiamsha, kuielimisha na kuindeleza jamii.
 
the point is, wewe masikini na chokoraa wa kenya, una ubavu gani kuja kujadili umasikini wa tz wakati umasikini wa kwako umeuacha kule kenya?....ondoa kamasi zako hapa, hua point....shughulikia matatizo yako kwanza, ndio uje kwa haya ya kwetu kama bado yatakuwepo.......

Mkuu wala husipoteze muda kujadiliana nao maswala ambayo yako obvious, si rahisi kubadirisha mind set za baadhi yao. Mkuu, baadhi ya hawa jamaa wana malengo fulani katika forum hii na wako well organized, wanafikili wakisema sema Tanzania basi hilo tu litatufanya tubadirishe misimamo yetu thabiti kuhusu certain issues ambazo wanaona tulisha washtukia siku nyingi na siku hizi tumewazidi kete, wanatuona kero kweli kweli. Kuikasikilia TANZANIA kunatokana na msimamo wetu huo wa kukataa shotgun wedding ya Federation vile vile na kutokubali ku-sign an open ended clauses zilizo wekwa kimaksudi kula kwetu.

Nilisha sema siku nyingi tu kwamba TANZANIA ni nchi huru - nyie fanyeni mambo yenu huko kwenu na wala sidhani kama kuna Mtanzania yeyote in his/her right mind anayeweza kuwa-bothered na mambo mnayo yafanya HUKO kwenu; mkitaka tubadilishane mawazo kwa heshima tutawasikiliza lakini mkileta mambo ya ukoloni ya kufikilia Watanzania ni shambaboy tutawapa wakati mgumu kweli kweli. Mkituomba msaada kwa kuheshimiana tutawapa, mifano tunayo:

* CHAKULA wakati wa baa la njaa nchini mwenu mwaka jana - hiyo ndio maana alisi ya ujirani mwema, siyo ujirani wa hila.

* Rais Jakaya Kikwete alipo tumia busara zake kuwasuluhisha wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe - je kama ingekuwa Tanzania mgetoa usuluhishi wowote kweli?

Back to the point, Mkuu we soma post yake No6 para No.2 ndiyo utagunduwa lengo lake lilikuwa ni nini hasa, kumbuka kahanzia mbali kwa ku-quote gazeti fulani; baadae kabisa ndiyo ka andika ya kwake-mambo mengine aliyo andika yalikuwa ni kupoteza lengo tu, madhumuni yake hasa hasa ni hayo aliyo andika paragraph No.2 post No.6-jamaa huyu yuko hell bent kuikandia Tanzanai-and 4what reason one may ask?

East Africa kuna nchi zaidi ya TANO na nyingine zinataka kujiunga, chukulia mfano wa nchi kama Uganda, Rwanda, Burundi na wale wengine ambao wanataka kujiunga na Africa Mashariki, katika nchi hizi zote tajwa hakuna nchi yoyote ambayo ina some kind of deluded axe-to-grind with TANZANIA zaidi ya baadhi ya raia wa Kenya - nimesema baadhi (some) sio wote, yaani chuki za baadhi yao mtu unaweza kufikili TANZANIA iliwahi kupigana vita na Kenya!

Mwisho, labda nisema mimi nimepata bahati ya kutembela nchi yenu na kuona kila kitu, leo hii nikimuona MKenya yeyote anaicheka/kubeza TANZANIA kuhusu umasikini ntamshangaa sana, nyiyi mna kitu gani cha kujivunia kuhusu kujali raia wenu masiki wa kutupwa; mimi nafikili ulipitiwa kidogo you didn't mean IT, kwa sababu tukianza kuchambua nulicho kiona huko kwenu KENYA hapa patakua hapakaliki nimeamua kumezea tu.

Leteni mambo ya kujenga kwenye FORUM hii na sio ridiculous rhetoric ambazo hazisadii chochote Tanzania, Kenya au wana JF, mimi binafsi sipendi mambo ya kutuniana misuri kama wendawazimu.
 
Inawezekana huyu bwana ana nia na uchungu, wasiwasi wangu ni kama kweli ana uwezo wa kuyakabila anayoyazungumza na kuwaza. Nafikiri hana! Na nia peke yake bila uwezo haiwezi kusaidia kumaliza umaskini, utasikitika sana lakini at the end of the day watu hatutampima kwa kiasi gani aliamia na umaskini wetu bali aliweza kupambana nao!
Namuunga mkono Dr. Kitira Mkumbo kwamba inawezekana ni kweli mkuu wa nchi (JK) anakosa usingizi kutokana na ugumu wa maisha ya watu wake lakini tatizo hakuna strategies nzuri zinazotekelezeka kuweza kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha.
 
Watanzania wenzangu imefikia wakati wa kuacha kulalamika kuhusu nchi yetu kuwa masikini na kufanya mabadiliko. Matatizo yote ya Tanzania yanajulikana na jinsi ya kuyatatua matatizo hayo inajulikana pia. Hivyo Kama Watanzania kwa nia yao wakichagua Viongozi ambao ni walarushwa na ambao hawawezi kutatua matatizo yao wasije wakalalamika. Imefikia wakati wa Watanzania kuelewa kwamba kuna Watanzania wenye uwezo na vilevile kuna Watanzania wala rushwa na wanajulikana vizuri. Watanzania wakichagua walarushwa basi tusije tukapoteza muda miaka michache ijayo na kujiuliza mbinu za kutatua matatizo wakati tunaelewa fika sababu ya matatizo.
 
Back
Top Bottom