heroone
Member
- Dec 15, 2011
- 24
- 3
Katika mambo ambayo binafsi huwa sielewi chanzo chake, basi mojawapo ni umasikini na lingine ni utajiri. Maneno haya hunichanganya sana hasa ninapoangalia nchi zetu za kiafrika. Huwa najiuliza hivi utajiri unapimwa na nini? Je umasikini hutambuliwa na nini? Je ni kweli umasikini upo? Na kama upo nani kauleta? Kwanini? Wapi? Na lini uliletwa?
Kwa muda mrefu sana nimejiuliza maswali haya. Kuna kipindi huwa naamanini kuwa umasikini na utajiri vyote hutengenezwa na binadamu kwa manufaa ya binadamu. Mwanafalsafa wa Ujerumani amewahi kuandika kuwa binadamu hutengeneza historia yake mwenyewe lakini nguvu kutoka nje humfanya binadamu kutengeneza historia kinyume na matwaka yake.Katika hili Karl Marx hakuiandikia jamii ya kiafrika lakini aliyoyaandika leo ndiyo yanaonekana Tanzania na Afrika kwa ujumla. Binafsi pia naamini kuwa maisha ni kutengeneza historia tusiyoitaka, historia ambayo hatujawahi kuifikiria.
Historia inaonesha kuwa kabla ya karne ya kumi na tano Afrika na Ulaya zilikuwa sawa kimaendeleo lakini baada ya karne ya kumi na tano mambo yakawa kombo kwa Afrika na kule ulaya hali ikawa shwari.Si lengo langu kufundisha historia leo lakini naamini kuwa historia ya Afrika leo inatushitaki waafrika wenyewe. Wazungu walipokuja na kututawala waafrika, walikuja na mila na desturi zao na kufanya waafrika tusahau utu wetu NA KUKUMBATIA UGENI WA WAGENI HAWA.
Hapa ndipo tulipofanya kosa kwa kumkaribisha mgeni huyu si sebuleni bali tuliamua kuonyesha ukarimu (ujinga) wetu na kuamua kumkaribisha mpaka vyumbani mwetu na tukampa wake zetu kwani huo ndio ustarabu wa MWAFRIKA!!! Matokeo yake leo ni kilio na kusaga meno, vita visivyoisha, migogoro, maandamano na migomo isiyo na kikomo. Hii yote imesababishwa na ustaarabu na ukarimu wetu wa kumuachia mgeni ale chakula chetu kizuri huku sisi tukishindia maji ya kunywa na karanga mbili tatu.
Ustaarabu wetu ndio unaotufanya tuogelee kwenye bahari ya umasikini huku tukiwa tumekaria utajiri wa kutosha. Mtaalamu mmoja wa masuala ya uchumi bwana Nurkse anadadafua kuwa
a society is poor because it is poor yaani jamii ni masikini kwasababu ni masikini au kwa maana nyingine jamii ni masikini kwa sababu ya umasikini wake.
Kimsingi Tanzania ni masikini kwasababu ya umasikini wetu. Umasikini ninaozungumzia hapa ni umasikini wa kufikiri ambao ndiyo zao la ujinga. Watanzania sio creativity na ndiyo maana tunatukuza ugeni na kuukataa uenyeji. Sisi ni watu wa kucopy na kupaste tu. Angalia vijana wa kileo huwaambii kitu kuhusu vimini, pedo, suruali zinazoonyesha maungo ya miili yao na vitopu vinavyoacha robo tatu ya mwili wazi ( kina dada) kinakaka wao ndio wameishiwa kabisa kwani wao ni walevi wa starehe, kuvaa suruali chini ya kiuno, kusuka ndicho wanachoweza, ukiuliza unaambiwa ndio kwenda na wakati. Ifahamike kuwa wakati tunahubiri kwenda na wakati akili zetu pia zinakwenda na maji matokeo yake ni ujinga unaoplelekea kuwa na mawazo ya kimasikini? Je kwa mantiki hii umasikini unatengenezwa au hautengenezwi? Kama kijana ni samadi ya taifa, taifa linaelekea wapi kwa hali hii? Nani wakuendeleza taifa? Ni hawa wanaokwenda na wakati au wengine? Wako wapi waokozi wa taifa hili JAMANI!!!?
Nikirudi kwa ndugu zangu wasomi aaahaaa!! Uozo mtupu!!! Hawa ndiyo kabisa wameathirika na utandawazi hadi vichwa vyao vimekuwa wazi. Utandawazi umeharibu kabisa malengo chanya ya elimu ambayo baba wa taifa aliyaainisha katika kitabu chake cha ujamaa ambapo anaeleza Elimu katika nchi yoyote duniani ni kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine maarifa na mila za taifa na kuwaandaa vijana wawe tayari kuchukua nafasi zao katika kulitumikia na kuliendeleza taifa. (ujamaa uk , 43) Je! Elimu ya Tanzania ina malengo yapi? Je! Elimu yetu inarithisha maarifa na mila za taifa kwa maendeleo na manufaa ya taifa? Au ndiyo kwanza inatufanya tuwe mabingwa wa kwenda na wakati? Au ndio chanzo cha mafisadi papa na mafisadi nyangumiiii? Kimsingi elimu ambayo haina shabaha ya kuendeleza taifa si elimu bali ni ujinga unaopelekea umasikini wa jamii na taifa kwa ujumla. Je kwa mantiki hii tutapata wapi wasomi watakao likomboa taifa hili?
Tanzania yenye neema ipo, tena ipo mikononi mwetu, akilini mwetu na majumbani mwetu. Ili kuipata Tanzania hiyo, hatuna budi kubadili mfumo mzima wa elimu hasa serikalini kwani mwanafalsafa mmoja aliwahi kuandika kuwa the government tend not to solve problems but only rearrange them Yaani serikali haina tabia ya kutatua matatizo bali kuyapanga upya ( tafsiri ni yangu) hivyo hatuna budi kuishinikiza serikali sasa ijipangie utaratibu wa kutatua matatizo na siyo kuyapanga upya. Hili linawezekana ikiwa tu tutaweza kuwapata viongozi wasomi wenye shabaha ya kweli ya elimu siyo hawa wasasa wasiotaka mabadiliko
Tatizo sugu lililopo kwa viongozi ni kutokubali ukweli. Viongozi hawa ndiyo zao la elimu yetu ya Tanzania na kupitia viongozi ndipo tunaweza kujua kama shabaha ya elimu ya Tanzania ni sawa na ile aliyoizungumza baba wa taifa. Viongozi hawa ambao ndiyo wasomi wa leo ndiyo walioko mstari wa mbele kukumbatia wageni, ndiyo wanaoongoza kwa kashfa zisizo na idadi, ndiyo wanaongoza kusaini mikataba kama ya kina chifu Mangungo na Karl Peters. Leo hii viongozi hawa ndiyo wakwanza kuchekelea pale wanapomuona mwananchi wa kawaida anapohangaika katika umasikini. Nikiangalia wayafanyayo viongozi hawa huwa nashindwa kuamini kama kweli hawa wamerisishwa maarifa na mila za taifa ili kuliendeleza taifa.
Kimsingi viongozi wetu hawapo nasisi tena, badala ya kujenga daraja wao wametumia kura zeu kama mtaji wa kujenga ukuta ili kuwa mbali na sisi, wameamua kujenga ukuta ili kuficha yale mabaya wafanyayo. Kwa mujibu wa nadharia ya Plato anaeleza kuwa kiongozi mzuri ni yule aliyesoma, kiongozi ni yule anayetumia elimu kutatua matatizo ya wananchi, kiongozi ni yule anayetumia elimu kuweza kutambua wananchi wake wanataka nini? Kwa wakati gani? Na kwa namna ipi?
Plato hakuishia hapo anaendelea kuelezea kuwa kiongozi mwenye elimu ni yule aliye tayari kufuata utawala wa sheria, aliyetayari kusikiliza wananchi wanataka nini, Plato anamalizia kwa kueleza kuwa kiongozi mwenye elimu yuko tayari kufanya kazi kwa namna yoyote ile kwa maslahi ya taifa na siyo kwa maslahi yake binafsi. Katika hili Plato anatuonya juu ya viongozi wanafanya mambo kwa maslahi yao binafsi. Je! Viongozi wetu wapo katika msimamo upi wa Plato? Je ni kweli wanafata yale yayotakiwa kufanywa na kiongozi kama yalivyoainishwa na Plato? Kama hawafanyi je elimu wakiyopewa na watanzania ina shabaha gain kwao?
Ukistaajabu ya MUSA kweli hutayoona ya FIRAUNI, wasomi wetu wa leo ndiyo hawa waliotayari kupiga marufuku maandamano ya wanafunzi na walimu kwa kile wanachodai kuwa wanamadai yasiyo ya msingi, wasomi wetu ambao ndiyo viongozi wetu wako tayari kufungia vyombo vya habari kwa kile wanachodai kuwa vinapotosha umma, wasomi wetu ambao ndiyo viongozi wetu wako tayari kusaini mikataba ya madini inayoliingizia taifa hasara zaidi ya dola milioni 20 kila mwaka. Wasomi hawa hawa ambao ndiyo viongozi wetu wanamuona mtu yeyote kuwa adui pale tu anapoamua kusema ukweli. Je! Kwa hali hii ni wasomi gani watakaolikomboa taifa? Ni wasomi gani wenye uwezo wa kutambua nini wananchi wanataka?
Kuna haja kubwa sana ya kubadili sekta hii ya elimu kwani kimsingi sekta hii imekufa na kuoza. Malalamiko yote yaliyopo yanayoelekezwa kwenye sekta ya elimu na mambo yote yanayofanywa na viongozi ambao ndiyo matokea ya sekta hii ni ishara tosha kuwa sasa mabadiliko yanahitajika kama kweli tunataka kulikomboa taifa na hii haihitaji shahada wala stashahada kulielewa.
Ifahamike kuwa mabadiliko katika sekta hii ambayo binafsi naiona ni muhimu kuliko sekta zote ikifuatiwa kwa ukaribu sana na sekta ya afya kutaleta na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa wananchi na kufyeka kama siyo kuondoa kabisa bahari ya ujinga nchini mwetu. Maendeleo ya taifa lolote huletwa na wasomi, je kama tusipowekeza katika elimu tutapata maendeleo kweli? Au ndiyo tutakuwa wasindikizaji katika mbio ndefu za kusaka maendeleo huku tukiwa tumelalia vitega uchumi vingi kuliko nchi yoyote duniani.
Badala ya kuwekeza katika elimu yenye shabaha ya kuliendeleza taifa, tunaamua kuwekeza kwenye malumbano ambayo kimsingi yahana kichwa wala miguu. Tuko tayari kupigana na mtu anayetaka kupunguza ulaji wetu badala ya kupigana na ufisadi ambao ni chanzo cha umasikini unalitufuna taifa hili bila huruma. Haiingii akilini kungangania Tsh. 200,000 kwa siku wakati mama yako anayefundisha shule ya msingi anapewa Tsh.250,000 kwa mwezi, baba yako askari analipwa si zaidi ya Tsh. 300,000 kwa mwezi, wakati huo huo dada yako anashindwa kumlipia mwanae anayesoma sekondari Tsh. 20,000 kwa mwaka na mtoto wako aliyeko chuo kikuu anapewa Tsh. 7,000 kwa siku bila kuangalia gharama za maisha zilivyopanda Je! Huu ndiyo ukarimu na ustaarabu tulionao watanzania? Tumewapa viongozi kura zetu wakatusemee au wajinufaishe?
Tubadilike, tuijenge nchi. Tuwe na roho ya huruma kama kweli sisi ni ndugu, tuwe na upendo kama kweli tunataka amani, tuwe wastaarabu kama kweli tunataka heshima, tuwe na mshikamano kama kweli tunataka umoja na mwisho tuwekeze katika elimu, tuingie darasani, tusikilize mawazo ya wengine kusaka maarifa mapya kama kweli tunataka maendeleo na kuipata Tanzania yenye neema. TANZANIA YENYE NEEMA IPO.
Waheshimiwa wananchi naomba kuwasilisha.