De Capri Don
JF-Expert Member
- Sep 13, 2023
- 481
- 947
Africa tuna hali ya hewa nzuri na Ardhi yenye rutuba,sasa kufanya kazi sana Ili iweje?Dr. John C. Maxwell ni Mwalimu mashuhuri wa uongozi duniani. Kabla ya kufika barani Afrika, aliamini yafuatayo kuhusu mafanikio, kwamba:
1. Mafanikio yanatokana na kufanya kazi kwa bidii.
2. Wamarekani wanaongoza kwa kufanya kazi kwa bidii.
Lakini baada ya kufika Afrika, alibadilisha mtazamo. Kwa mara ya kwanza maishani mwake alishuhudia watu wanaofanya kazi sana lakini bado hawana maendeleo.
Sijui "case study" yake ilikuwa nchi gani Afrika, lakini maadam ni Afrika, na Tanzania inahusika, na ni kweli kuwa kuna Watanzania wengi wanaofanya kazi kwa bidii lakini wangali wana hali ngumu kiuchumi.
Kwanini iko hivyo?
Hakuna winter Wala barafu so matumizi ya nishati kwetu ni kidogo sana na hatuhitaji kuhifadhi chakula msimu wa baridi .
Marekani lazima wafanye kazi ,marekani akizeeka anaenda kulelewa ktk majumba ya wazee na wanalipia pesa ndefu ,so kipindi Cha ujana ni kupambana Ili kesho uweze kumudu mlezi na medical care .Africa watoto kulea wazee wao ndio utamaduni wetu.
Ufeminist pia ni sababu Kwani baada ya mapinduzi ya viwanda wanaume ndio waliokuwa wafanyakazi na wanawake walezi wa familia.
Mabeberu Kwa kutaka cheap labor basi mwanamke naye akaanza kazi na mishahara ikashuka na ndo mpaka Leo.
No Harry in Africa.