Kwanini Watanzania wengi hawafanikiwi kutokana na kazi zao?

Africa tuna hali ya hewa nzuri na Ardhi yenye rutuba,sasa kufanya kazi sana Ili iweje?
Hakuna winter Wala barafu so matumizi ya nishati kwetu ni kidogo sana na hatuhitaji kuhifadhi chakula msimu wa baridi .
Marekani lazima wafanye kazi ,marekani akizeeka anaenda kulelewa ktk majumba ya wazee na wanalipia pesa ndefu ,so kipindi Cha ujana ni kupambana Ili kesho uweze kumudu mlezi na medical care .Africa watoto kulea wazee wao ndio utamaduni wetu.
Ufeminist pia ni sababu Kwani baada ya mapinduzi ya viwanda wanaume ndio waliokuwa wafanyakazi na wanawake walezi wa familia.
Mabeberu Kwa kutaka cheap labor basi mwanamke naye akaanza kazi na mishahara ikashuka na ndo mpaka Leo.
No Harry in Africa.
 
Yaani mtu unasimangwa ndani ya nchi yako iliyo huru!

Very painful!
 
Kama hiyo ni sababu, kwa nini nchi za Kiafrika ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa "uwizi?"

Ukiona mtu anaiba, anachukua rushwa n.k. ujue anatafuta mafanikio kwa njia haramu.
 
Siasa ndio kazi pekee Afrika inayoweza kukuletea mafanikio kwa haraka
Nasita kukubali hilo mkuu! Wengi wa wanaoonekana wamepata mafanikio ya kifedha baada ya kuingia kwenye Siasa ni "wezi".

Labda ungesema "ujambazi" wa kisasa" ni mrahisi zaidi barani Afrika.

Lakini simaanishi wanasiasa wote ni "majambazi", wapo walio "wazuri".
 
Inategemea aina ya kazi unayofanya na jinsi unavyofanya. Hiyo bidii unaweka katika kitu gani.

Ukiwa na watu wengi ambao wanafanya kazi za mkokoteni, bodaboda, bajaji, uchuuzi, udalali, ukuli n.k kwa bidii bado ni vigumu sana kuendelea kwa sababu ni kazi zisizotumia akili nyingi.

Ukiwa na jamii kubwa ya watu wanaofanya kazi za kitaaluma kama ufundi,assembly viwandani, udaktari, ukufunzi, uongozi, Kilimo, ufugaji na nyinginezo kwa bidii ndipo maendeleo yanaweza kupatikana katika nchi.
 
Kutumikisha wengine ni sawa, ni mojawapo ya smart work, ila hayo mengine uliyoandika kabla hayana uhusiano
Hilo neno "kutumiskisha" kama lina kaukakasi mkuu. Mimi nafikiri kazi nzuri ni ya "win win" baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Kama inayokusaidia ni ya kwako hata kama inamilikiwa na mtu mwingine.

Mfanyakazi na mwjiri wake ni "partners" wa maendeleo ya kila mmoja.
 
Pia ni vigumu kufanikiwa kibinafsi kama sehemu kubwa ya jamii inayokuzunguka haijafanikiwa.
Kuna kitu kinaitwa vicious circle of poverty, hiyo chain kama umezungukwa nayo katika jamii yako na haijavunika hata kwa bahati wakati fulani ni vigumu mno kufanikiwa hata ukifanya kazi kwa bidii vipi.
 
Toa maoni Kwa maana unayoijua wewe kuhusu kuchapa kazi
Kwa mtazamo wangu, ni kufanya kazi kwa kujitoa sana kulikotanguliwa na maarifa sahihi.

Ndiyo kusema, kama mtu kapewa masaa manane ya kukata mti, anaweza kutumia masaa zaidi ya manne kunoa shoka ili atumie muda mfupi sana kuuangusha huo mti badala ya kupambana nao kwa masaa nane yote aliyopewa.
 
Mbona kuna Wahindi walikuja Tanzania wakiwa na hali duni kiuchumi, wakapanga vyumba vya kawaida Uswahilini, lakini baada ya muda wakawa mabilionea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…