Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Kero ya paka ni kwamba huwa anaajiona yeye ndio anakumiliki wewe, vile anavyoona unamlisha, unamshika shika, n.k anaona yeye ndie bosi wako, yani inafikia kipindi kama siku mnapika samaki na yeye mmempa dagaa, hatakula hizo dagaa 😂 atasubiria samaki hao mnaowaunga ama kuwakaanga. 😂😂😂 ubaya wa paka mwengine ni kwamba mda wowote anaweza kuondoka hapo kwenu anarudi baada ya miezi ana mimba 😂😂

Kwa mbwa tayari huwa anajua wewe ndie master / mmiliki wake, inakuwa rahisi hata kufundishika, ila sasa wabongo wengi wanatesa mbwa wao.
 
Kama hili ni tukio kweli umelifanya kwa mtoto,hakika ulivuka mipaka...ila naona ni kama tu umeamua kuchangia mada kwa chai.
 
Ni mazoea mabaya tu.

Tunapaswa kuwahurumia, na kutowatesa.
 
Ni hali ya umaskini tu wa hali na mali akili na nafsi zetu ni maskini sana, ndio maana roho mbaya zinatutawala
 
Na pia paka wanaringa na dharau ila nawapenda wanavyodeka tu nadhan ndio wameumbwa hivyo
Sijawah kuishi na mbwa ila najua ni wazuri
 
Yes, sichezi na wajinga kwani huyu mtoto na wenzake huu ulikuwa mchezo wao.....kila nikawakataza walifanya kama mchezo. Wakitoka shule na madrasat wanapitia nyumbani na kurushia mbwa mawe ili awabwakie tu. Mtoto akicheza na moto au wembe -----------!
Akili yako haipo sawa, yaan mtoto anafanana na mbwa?? Hao wazazi labda ni masikini sana ila ingekua mm show ungeipata vzur
 
Wasukuma wana tabia ya kutesa sana punda.Nenda uone wamasai wanavyotunza punda wao
 
Yaani ni ukweli mtupu..!! Tunawabutuaga vibaya sana yaani..!! Enzi zetu tukikuta mbwa wamenasiana yaani tunabiga haswaa.. Hata sijui ilikuwa kwa sababu gani.. MUNGU ATUSAMEHE KWA KWELI
 
Si unaona hapa dogydogy wangu anaitwa wisky anaingia ndani

Na chill naye .....kwanza wakati mwingine naonaga bora mnyama kuliko binadam,maana mwanadam
Hata umfanyie nini hana shkran
Minafki tu
Nje yuko simba,simba mtata zaidi hanaga kujuana na watu
Hawa ndiyo rafiki zang wa unwell

Ova
 
Asili ya mwafrika huwa hapendi wanyama na hili huusishwa na Imani za kishirikina mf. Paka,panya,bundi,nyoka,njiwa,mijusi, fisi na vingine vingi. Wazee wetu ndio chanzo.
 
Kuna wale paka wanaofugwa na kurandaranda kwenye pub au migahawa ya uswahilini. Kila wakiona mteja kapewa huduma ya chakula nao usogea miguni wakivizia wadondoshewe chakula. Uwa najiuliza kama hao paka ni wa wamiliki wa hizo pub au migahawa ambao wapo pale kwa lengo la kukubiliana na panya kwa nini wasiwe wanawaandalia hata makombo ya chakula kilichobakizwa na wateja kwa kuwawekea sehemu yao maalumu ili wasiwe wanawabugudhi wateja kwa kuwazongazonga miguuni? Maana mteja kula chakula huku kamkaushia paka anaemzongazonga huku akilia nako kunamletea aibu mbele ya wateja wengine na akisema ampe sehemu ya chakula alichohudumiwa kama ni kidogo basi yeye anaweza asishibe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…