Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Safi sana aiseee
 
Mimi nilifundishwa kutokupiga wanyama hata viumbe vingine visivyo na madhara kwenye mazingira yetu siui mijusi hata wadudu wengine warukao ambao hawana madhara nawafukuzia nje huko pamoja na ndugu zake Chura mpaka watoto nao hasa wa kiume tunaenda sawa maana sio waoga..
 
Mkuu; Wewe sio mgeni na suala la kumchapa viboko mtoto wa mtu. Ukijaribu tu kufanya hilo mzee, timbwili lake ni balaa hususan akija mama mzazi. Hakuna rangi utaacha kuona. Atakufedhehesha na kukudhalilisha mno hadharani kuliko maelezo.😭😭
Kwa maelezo yangu labda sikuwa detailed ni kwamba nimekuwa nikiongea nao kirafiki na kuwaelimisha madhara ya mbwa na Ubaya wa kumpiga mbwa kwani mbwa hajawachokoza. Hilo liliwahusu hata wazazi wao na shuleni.
By the way, unafahamu kwamba mbwa hutunza kisasi? Wewe kama ulimpiga mbwa kwa makusudi tuseme 2021 jua kwa uhakika siku akipata nafasi leo 2022 lazima akutie jeraha hata kama umejichanganya kwenye kundi la watu au pamepita muda mrefu. Atalipiza kisasi tu na watu wengi wanalijua hilo.
Zoezi la adhabu hufanyika kwa uangalifu.
Hata hivyo mkuu; haitatokea hata siku moja mbwa akang'ata usoni. au machoni kama ulivyotahadharisha. Mbwa mara zote hung'ata makalio, mapaja au mkono. Ni mara chache sana mgongoni na ni pale mtu anapokimbia na bahati mbaya akaanguka chini. Mtu huangukia tumbo(kifudifudi) na mbwa hung'ata mgongo.
Pamoja na hayo, labda nikuwekee tu wazi kwamba mm ni Mtaalam wa mifugo na ninafahamu ninacho kisema.
 
Kwa hiyo una ID mbili,
Moja umeleta kisa, ingine unajitetea nayo,

Wewe ni Katili hata uandike magazeti vipi na una bahati mimi sio member wa hiyo familia ya mtoto, ilikua unapewa kesi moja takatifu (kukusudia kuua mtoto) ungekaa jela hadi ujue tofauti ya Mnyama na Mtoto,

eti namuhudumia Mbwa sijui nini, aiseee! kuna watu sijui mnaishi sayari gani.
 
Kweli mmerogwa leo mnavyowatetea mbwa sasa! Ila mnavyoshabikiaga kupiga mke aloooo hadi shetani anaogopa.
 
Mkuu; kwa uhakika sina ID mbili labda unishawishi ili niwe nazo. Ni sahihi ungenipa kesi lakini ujue na Kesi huamuliwa na Mahakama sio Mlalamikaji. Kama nia yako ni ili nikae jela (kwa kunikomoa) kwanza zingatia kwamba Mtuhumiwa hawekwi jela bali huwekwa Mahabusu. Pili kumbuka kwamba mahabusu au kama wewe unavyoita ni jela huko wanakaa watu sio mbuzi. Kwa hiyo kama hoja yako eti ni kesi takatifu (kukusudia kuua mtoto), itaonekana ina mashiko basi nitakaa huko kama wanavyokaa huko watu wengine. Wewe unaogopa jela? By the way, ww ni Ke au Me? Kama ni Ke , basi hiyo comment yako inayapa uzito maneno yangu kwamba akija mama .....timbwili lake...
 
Asili ya mwafrika huwa hapendi wanyama na hili huusishwa na Imani za kishirikina mf. Paka,panya,bundi,nyoka,njiwa,mijusi, fisi na vingine vingi. Wazee wetu ndio chanzo.
Mifugo haitakiwi kudhurula mitaani, baadhi ya nchi za ulaya, kunakikosi maalumu huwa kina dili na mifugo inayo dhurula mtaani.

Mbwa wako wakimkuta mchana, hata kama yupo karibu na kwako, wanamkamata kwa kutumia sitiki maalumu, zenye kamba yenye mtego. Kisha kumchukua kwa gari maalumu na kuondoka nae.
 
Huku Tz. wanapokuwa ni wengi wanazurura mitaani, hospitali, machinjioni, kwenye majalala(Vizimba) au sokoni na ikaonekana ni kero au tishio kwa usalama wa watu, hupunguzwa kwa kupigwa risasi lakini ni kwa kuzingatia Utaratibu sio kiholela.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Pamoja na kufuga kuku ila hua si chinji kutokana na vile ninavyowalea nao pia Huwa wananipenda,Huwa sijiskii poa kabisa kuwachinja
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah, nimecheka sana
 
Hakuna siku nimeona huzuni kama siku nimeenda machinjioni (Mbalizi-Mbeya), sasa pale kweny karo la kuchinjia, ng'ombe anapelekwa mzobemzobe anavutwa mkia kutokana na zile damu kweye karo anateleza akianguka tu jamaa mmoja mbavu anakuja anamvuta mdomo yule ng'ombe shingo inajikaza, anakuja yule mchinjaji (Dingi mmoja wa kiislam) anapitisha kisu kikali mara moja tu damu zinaanza kumwagika huku ng'ombe anarusharusha miguu, Sasa kunakuwa na ng'ombe wengine ambao hawajachinjwa wako pembeni ukiwaona wanakuwa na hofu hadi wanajiharishia....na wanyama wanajua kifo na wanakiogopa sana.
 

Dah! angalau hao wengine wasione, ila huo ni ukatili kwan hamna jinsi nyingine nzuri ya kuchinja

Ila kitimoto si ndio naskia anapigwagwa shoka la kichwa kabla ya kuchinjwa mpaka anakata network, waafrika mungu atusamehe tu
 
Ni kweli na inasikitisha sana (Inhumane killing). Kiutaratibu inatakiwa mnyama wa kuchinjwa aingie eneo la kuchinjwa peke yake wengine wasione japokuwa watakuwa wameshtuka kwa harufu ya damu. Na kabla hajachinjwa anapotezwa fahamu ndipo Mchinjaji amchinje na sio hivyo kavu-kavu anajiona Live. Hupotezwa fahamu kwa kuwa stunned kwa kutumia umeme au kumgonga kwa nguvu na kitu kizito manually kichwani.
 
Dah! angalau hao wengine wasione, ila huo ni ukatili kwan hamna jinsi nyingine nzuri ya kuchinja

Ila kitimoto si ndio naskia anapigwagwa shoka la kichwa kabla ya kuchinjwa mpaka anakata network, waafrika mungu atusamehe tu
Eheeee hapo hapo nguruwe nae anauliwa kikatili sana, hatua ya kwanza lazima apigwe mipini ya kutosha kichwani na shoka la chuma, akipoteza neti ndo anapigwa beto, unaambiwa nae akikiona kisu anaweza pita na mtu na lile domo lake kama msumeno anakuua, so kumuua lazima "wamsapraizi" na shoka then ndo achinjwe
 

Hapo mbeya uliposema wanawaonea ng’ombe ambao wapole angekuwa huyo jamaa na lile pua lake angepita na sheik mchinjaji, oh sorry kumbe hamnaga sheik anaochinja ile kitu
 
Nakubaliana na wew asilimia mia moja,hawa ni viumbe ambao wameumbwa na Mungu afu sisi viumbe watu tunajiona ndo wazur zaidi kuliko wao,lakin wapo kwa ajili ya kusaidiana kwa ya kwetu,
 
-Mtu kashiba nyama, anaenda kuitupa badala ya kumpa paka mwenye njaa,
Kaka hichi ulichokiandika nikosa kubwa sana. Hawa wanyama wafungwao ni wanyama kama tulivyo sisi, kwanini yale mabaki tunayokula sisi tunawapa wao. Wale wanyama wanahitaji chakula kisafi na mahali pasafi kama sawa na mazingira tunayokula chakula chetu sisi tunaojiita wanadamu

-Mbuzi ameletwa kwajili ya sherehe, usiku umefika anaachwa ukutani badala ya kumweka hata stoo aweze kupumzika, kujikinga na baridi, mvua, n.k.
Sisi pia ni wanyama kama walivyo wao kwanini tuwaweke store na wakati unaweza hata muombea kwa jirani mwenye banda na asubuhi ukamchukua kwa shughuli yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…