#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

Mleta Maada ulikua na kamati yako na wewe ambayo umeitumia kukusanya maoni ya watanzania juu ya chanjo au ni mawazo yako tu na ukoo wenu kwamba watanzania hawakubali
 
Kwamba itakuwa huwezi kuhudumiwa mpaka uchanjwe ama.?

Ndio,unawekewa vikwazo tu ilimradi nawe ufanye upatiwe chanjo mfano :-mahujaji
Ina maana huwezi kwenda hija mpaka uwe umepatiwa chanjo.

:- ikitokea umeenda lamda hospitali hasa za serikali huwezi pewa huduma yoyote endapo kama hukupata chanjo

Itabidi upate chanjo,ndio hudum zingine ndio zitafuata

Mimi Nawaza hivyo
 
Duh [emoji849]
 
Kwani huoni hizo steps ambazo zinachukuliwa, ndio ku-fix kwenyewe huko. Au unataka mpaka Mama asema Magufuli was wrong?
Mada inazungumia watanzania kukakataa chanjo sasa ni hatua gani zilizochukuliwa kufix hili la watanzania kukataa chanjo? wote tunajua kuwa wenyewe pamoja na Magufuli kwa pamoja ndio waliyosababisha hii hali huwezi kuwatoa kwenye lawama hawa viongozi na kumtupia lawama Magufuli tu.

Sehemu anapokuwepo rais tu ndio tunaona wanavaa barakoa sasa hapo utasema wanafix nini na ndio maana hata uraiani wananchi hata hawashtuki kuona rais kuvaa barakoa wao wanaendelea kama kawaida bila barakoa.
Halafu wanakurupuka wanataka kuleta chanjo unategemea nini?
 
Mleta Maada ulikua na kamati yako na wewe ambayo umeitumia kukusanya maoni ya watanzania juu ya chanjo au ni mawazo yako tu na ukoo wenu kwamba watanzania hawakubali
Kama barakoa tu wamegoma kuvaa pamoja na kumuona rais kuvaa ndio watakubali kuchanjwa?
 
Chanjo iliyotengenezwa ndani ya mwaka mmoja, hakuna conclusive research iliyofanyika kuweza kupata final approval, hakuna data za mid- and long-term effects. Short-term effects zimeshaonekana, efficacy ipo chini lazima uchanje kila miezi 6, ni teknolojia mpya ya utengenezaji wa chanjo inayohusisha vinasaba DNA/RNA imeshaleta complications za autoimmunity kama blood clots, autoimmune thrombocytopaenia, sijui tunakimbizana kwenda wapi? au ndo presha za mabeberu hizi.....
Usibebe akili za Gwajima tu pia changanya na za kwako!
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.

Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania.

Mapendekezo yangu

1)Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa
2)Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea
3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo
4)Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
wengi ?
hiyo takwimu umeipata wapi?
 
Mleta Maada ulikua na kamati yako na wewe ambayo umeitumia kukusanya maoni ya watanzania juu ya chanjo au ni mawazo yako tu na ukoo wenu kwamba watanzania hawakubali
Mkuu kama wewe kitaa hii Malalamiko lazima ukutane nayo pia
 
Hili suala ni la kisayansi. Sayansi hiyo hiyo ndiyo imekuletea dawa za malaria, kufubaza ukimwi, kinga ya kifua kikuu, surua nk. Leo kwa kuwa tumelishwa sumu ati chanjo ya corona ni mbaya tunaitikia tu.
Kwa maoni yangu, kama ilivyo kwa madawa ya ukimwi, mtu asilazimishwe kutumia, period.
Kweli kuna watu damu inaganda (Marekani walikuwa 6 kati ya mlioni 7 waliokuwa wamechanjwa), ukipima faida na madhara unaona faida ni kubwa zaidi, Hata WHO waliliona hilo lakini waka recommend kuwa chanjo hizo ziendelee kutumika.
Je kuna dawa isiyo na madhara? Watu wamelishwa eti chanjo ya corona itazuia uzazi wanasahau kuwa hao hao ndio wanaongoza kwa kutumia dawa Za uzazi wa mpango na kufunga uzazi hadi kansa zinawamaliza! Aibu tupu!!
Kuna watu huko DRC walikataa chanjo ya ebola ( na ilikuwa bado iko kwenye majaribio), kilichowakuta.. waliitafuta kwa gharama. baadae chanjo hiyo ilkuja kuthibitishwa kuwa inafaa, Hata mlipuko wa ebola huko west africa ilikuwa hivyo hivyo.
LAKINI KILA AIPONDAE CORONA MWISHO WAKE HIYO HIYO HUM...
Canadian singer Raymond Levesque dies at 92 after contracting Covid-19
Kama nyie watu wazima hamtaki, basi tuwaokoe watoto maana nao sasa inawapata
mwisho hao wazungu tayari wanaikimbilia chanjo hadi wanashtaki kampuni inayoitengeneza kwa kuchelewesha
India wameng'ang'ania chano na hawataki kuzipa nchi nyingine hadi wao watosheke

HALAFU ETI WEWE CHANO YA CORONA NI....
 
Walikaririshwa, wakakariri sasa wanakiimba wasichokijua...
Wengi kwa sababu ya "...ulofa na..." hawatambui wanataka nini na wanadhani Tanzania ni kubwa kuliko dunia...
Sisi wengine tunaamini Mungu alishatushindia kwa maombi tuliyofanya na Magufuli ndio maana hatutaki barakoa wala social distance wala maji tiririka wala chanjo

Ila kama hiyo chanjo inatakiwa kwa wengine sio kesi ila kwa kuwa iko kwenye majaribio kwanza serikalini isiagize wasitumie Kodi zetu waachie hospital. Binafsi pili Wa kwanza kuchanjwa wawe wanasiasa na wabunge kuwa ikiwa na madhara hata ikiwaua poa tu tutachagua wengine.Kundi la pili naungana na Shehe mkuu Wa Bakwata Mufti shehe Zuberi liwe LA wale wanaoitaka hiyo chanjo watu wasilazimishwe

Watumishi Wa afya wapewe tu vifaa kinga wasichanjwe sababu ikiwa na shida tumekwisha.Wanajeshi pia wasichanjwe jeshini sio sehemu ya majaribio ya dawa
 
... siku hizi Mataga wanatambulika kama watanzania "wengi"? Be serious ndugu; labda hayajawahi kukukuta; nenda hospitalini uone wagonjwa wa Covid wanavyoteseka utatamani chanjo ije muda huu huu! Tuwaonee huruma wazee wetu na wengine wenye matatizo ya kiafya; corona ni hatari sana kwa uhai wao! Mataga achana nao hawafagi Corona wale!
Tutajie hiyo hosptali yenye wagonjwa wa corona tukawape pole.
maana mnaona fahari sana kuwa na corona.Eti nywele ngumu analilia chanjo utafikiri chanjo ndo kinga ya kifo,waliochanjwa wanakufa wengi kuliko hata waliochanjwa,ukiachana na mambo madogo ya kuganda damu.
 
Wewe ndiyo unakataa mkuu sisi wengine tunaitaka sn
Kachanje tunachokataa tusilazimishane na isiwe kwa Kodi zetu chanjo iagizwe na hospitali binafsi kanunue huko kachanje mwili Mzima hata ukitaka ila usiforce wengine ambao hatutaki kuvaa barakoa wala kuchanja woga wako Wa Corona sababu una maradhi yako unayojua mwenyewe ulikoyaokota usisumbue wengine kwa migonjwa yako ya kujitakia uliyonayo!!! Unayeona corona ikikugusa tu unageuka marehemu kachanje

Watetea chanjo wengi wanaumwa NA tena migonjwa ya kujitakia ya life style kuanzia ukimwi nk
 
Hili suala ni la kisayansi. Sayansi hiyo hiyo ndiyo imekuletea dawa za malaria, kufubaza ukimwi, kinga ya kifua kikuu, surua nk. Leo kwa kuwa tumelishwa sumu ati chanjo ya corona ni mbaya tunaitikia tu.
Kwa maoni yangu, kama ilivyo kwa madawa ya ukimwi, mtu asilazimishwe kutumia, period.
Kweli kuna watu damu inaganda (Marekani walikuwa 6 kati ya mlioni 7 waliokuwa wamechanjwa), ukipima faida na madhara unaona faida ni kubwa zaidi, Hata WHO waliliona hilo lakini waka recommend kuwa chanjo hizo ziendelee kutumika.
Je kuna dawa isiyo na madhara? Watu wamelishwa eti chanjo ya corona itazuia uzazi wanasahau kuwa hao hao ndio wanaongoza kwa kutumia dawa Za uzazi wa mpango na kufunga uzazi hadi kansa zinawamaliza! Aibu tupu!!
Kuna watu huko DRC walikataa chanjo ya ebola ( na ilikuwa bado iko kwenye majaribio), kilichowakuta.. waliitafuta kwa gharama. baadae chanjo hiyo ilkuja kuthibitishwa kuwa inafaa, Hata mlipuko wa ebola huko west africa ilikuwa hivyo hivyo.
LAKINI KILA AIPONDAE CORONA MWISHO WAKE HIYO HIYO HUM...
Canadian singer Raymond Levesque dies at 92 after contracting Covid-19
Kama nyie watu wazima hamtaki, basi tuwaokoe watoto maana nao sasa inawapata
mwisho hao wazungu tayari wanaikimbilia chanjo hadi wanashtaki kampuni inayoitengeneza kwa kuchelewesha
India wameng'ang'ania chano na hawataki kuzipa nchi nyingine hadi wao watosheke

HALAFU ETI WEWE CHANO YA CORONA NI....
Mbona huleti link ya Seychelles inayoongoza kwa kuchanja watu wake,na mlipuko uko juu tena.
unaleta utetezi wa kushobokea wazungu tu.Ni nchi gani imeondoa janga la corona baada ya kuchanjwa? Lockdown za nini? Mask za nini?
 
Utaratibu wa Zanzibar ndo mzuri mahujaji watafutiwe utaratibu tu wachanjwe si kuja na mapendekezo kana kwamba kuna mlipuko.
Mwisho wa siku mambo yakiharibika maana visa vimekuwa vikiongezeka baada ya kuchanjwa mf.majirani zetu walilazimishwa kufunga miji mitano.Likisha fika swala la lockdown hii nchi itakuwa chungu sana,maana njaa ni kitisho kuliko mafua ya wazungu.
 
Back
Top Bottom