Kwanini Watoto wa Kike wa Marehemu Mafuru hata hawalii Msibani na hawana Wasiwasi tofauti na Misiba yetu Sisi Uswahilini ambapo hulia kwa Kukufuru?

Kwanini Watoto wa Kike wa Marehemu Mafuru hata hawalii Msibani na hawana Wasiwasi tofauti na Misiba yetu Sisi Uswahilini ambapo hulia kwa Kukufuru?

Utakuta kuanzia Chekechea waliosoma Boarding

SEKONDARI Shule za maana....
Vyuo wamesoma nje...

Kila mmoja anayo account ya Dola

Wameajiriwa TPA, BOT, TRA, UN Agencies au Ubarozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa.

Kwa status hizo walilie nini sasa????
😂
 
Muda wote nawatizama sioni hata anayelia au aliye na wasiwasi na Maisha yake ya baadae baada ya Baba Kufariki.

1 The 4:13-18​

Hao watoto walilisoma hili fungu nakulielewa nafikiri.
Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
 
Mswahili amefariki kaacha deni alilokopewa kikoba na mkewe ili alipe kodi ya nyumba unadhani uchungu wa kilio utakosekana kweli?
Wakijiuliza deni linalipwa vipi? Kodi inalipwa vipi? Wanapata kilio, ukunga kwikwi....
Nakwambiajee
Unakuta umemkopea baba ako ASA mchongo unasoma afu 50000 kwa wiki we mwenywe pangu pakavu tia nchuzi unapigiwa simu baba ako kafa... Sipati picha ntalia kilio cha namna gani
 
Kwani watoto wa Mengi au Ali mufuruki uliona wanalia?
Au watoto wa tajiri yeyote uliwahi ona wanagaragara chini?
Hapana mkuu, anakuwa na miwani nyeusi na kakitambaa, utasikia tu Its ok, Its Ok, Our beloved dad hatunaye, amepumzika.

Huku kwengine, Ukunga mkubwa, woooooooooooooooi woi woi. Ameeendaaaaa jamani ameeenda,

Ntaweka wapi sura yangu mie, Babaaaaa rudi unichukue na mimi, umendaaaaa. Huku ana kwikwi, kamasi n.k
 
Na muda si muda anatupa waombolezaji kazi ya kumbeba baada ya kuzimia.
 
Back
Top Bottom