Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
CV unayosoma ni ya kupindapishapindisha. Aliteuliwa na Mkapa kama Waziri mdogo mwaka 1995 akiwa ama bado mwanafunzi au la; hiyo ya kufanya kazi Muhimbili au Kairuki ni vitu vya pembeni labda katika nia ya kupika CV lakini jamaa amekuwa Waziri tangu 1995; aliteuliwa kipindi kimoja na Magufuli.Kuna jambo halipo sawa kuhusu watoto wa Mwalimu manake hata wale waliowahi kupata kuwatumikia wananchi hawakuonesha consistence yoyote. Na kuhusu Hussein Mwinyi, CV yake inasema tofauti na unachosema wewe. Kwa bahati mbaya sifahamu taaluma ya afya inavyoendeshwa endeshwa lakini CV ya Hussein inaonesha badala ya kumaliza MD, amefanya kazi Muhimbili kama Registral na MD, Kaiuruki kama Specialist na Lecturer. CV yake inaonesha amepata nafasi ya kwanza ya uteuzi miaka 7 baada ya kuwa ameshachukua MD (awamu ya Mkapa).
Nisichofahamu ni kuona muda huo ambao ni takribani miaka 9 pia alikuwa anasoma Masters na PhD UK. Sasa kama udaktari na wenyewe unaweza kusoma bila coursework, hapo ndo sina uhakika. Sasa kama unaweza kusoma bila kuingia darasani (hususani masters) sioni kubebwa kwa Hussein kunaingiaje ingiaje hapo hasa ukizingatia wakati anachukua uteuzi kwa mara kwanza, alishakuwa mbunge. CV inaonesha amemaliza MD 1991, wakati ubunge na uteuzi ni mwaka 2000.