Umeshaelewa.Kila linalofanyika popote,hata kama hukumuona mfanyaji ukiwa na utajua yupo aliyefnya hivi,ukiona unyao wa simba hata kama hayupo,utasema hapa kapita simba.Hutasema huu unyao umejifanya wenyewe.Utaanza kuchukuwa tahadhari,kuwa eneo hili lina simba.
Ukiingia darasani,!!ukiona ubao umeandikwa,utajua wazi yupo aliyeandika,hata kama hukumuona.
Iweje upate usingizi na uone watu wanakufa,halafu useme havina mfanyaji.Tumia akili,!!japo akili huioni,lakini utaambiwa huyu ana akili sana,ni kutokana unayofanya ya ki akili.
Ngoja nikupe kisa kimoja.
Almasi ni aina ya madini yanayopatikana zaidi sehem moja inaitwa Mwadui_kishapu _Shinyanga.
Kuna migodi kadhaa, ukiwemo mmoja maarufu unaenda na jina la kampuni ya Williamson Diamonds limited.
Hapo awali kabla ya uhuru, almasi ilikuwa inapatikana juu tu kama mawe na wazee wa pale mwadui walikuwa wakichezea bao kama mawe.
Hivyo almasi ilikuwa ya kuokota.
Mpaka alivyokuja mzungu (Williamson) kuzichukua hadi kuanza kufanya uchimbaji.
Kwasasa almasi haipatikani juu tena, ni uchimbaji wa mashimo marefu sana.
Kupitia historia hii
Ukamkuta mzee aliyekuwa amepoteza fahamu kipindi wanachezea almasi kwenye bao amezinduka leo, na katika kuzinduka huko akaja na almasi zake alizokuwa ameziacha kwenye chumba chake.
Na akakwambia kuwa aliziokota, utakataa umlazimishe kuwa ni lazima ziwe zimechimbwa kisa wewe unadhani kuwa ni lazima ziwe zimechimbwa kwasababu umelazimishwa na mawazo yako kuamini ni lazima kama unavyoona muda huo?
Nnachokwambia wewe ni kwamba, unataka kulazimisha Uende kama mawazo yako yalivyo.
Cha kukuongezea ni kwamba:
Hata zamani ilikuwa ni inajulikana kuwa jua ndo linazunguka dunia na dunia ndiyo center ya universe.
Hapo usingeweza kumwambia mtu kitu akakuelewa kama ulivyo wewe na imani kuwa ni lazima kuwepo na kilichotengeneza ulimwengu.
Ni mawazo hayo hayo watu walitumia kulazimisha kuwa dunia ni flat, na ilichukua muda mpaka watu wakafanya proof kujua kuwa dunia sio flat, bali ni umbo tufe.
Hapo pia usingeweza kumwambia mtu tofauti akakuelewa kama ulivyo wewe na imani kuwa ni lazima kuwepo na kilichotengeneza ulimwengu.
Kwasababu hapo watu walikuwa na anthropic bias katika kutafsiri na kulazimisha mambo yawe ni lazima kama wanavyoona muda huo.
Sasa hiyo anthropic bias ndio hii hii unayoilazimisha wewe hapa uitumie.
Ukiambiwa uthibitishe uwepo wa Mungu huwezi na umeshindwa umebaki na mawazo haya haya ya kulazimisha kadri wewe unavyoweza kuona.
Nijibu hapa.
Kama kila tukionacho kina aliyetengeneza, huyo Mungu yeyee alitengenezwa na nani?