Kwanini watu wengi tunaendelea kunywa pombe licha ya kuona madhara yake kwa wengine?

Watu wanakunywa pombe miaka na miaka na bado wanadunda tu .

Huna babu huko kijijini ambaye anakunywa pombe?
 
Tuache kila mtu apambane kuishi kwa namna yake. Tusihukumu sana. Binafsi sinywi kwa ajili ya kutunza utimamu wa akili tu. Nataka kila ninalopitia maishani nipitie nikiwa timamu. Nataka "full experience" yaani.
Vipi ikitokea unasumbuliwa na jino na linatakiwa kung'olewa???

Upo tayari kupitia maumivu ukiwa timamu bila ganzi?
 
Vipi ikitokea unasumbuliwa na jino na linatakiwa kung'olewa???

Upo tayari kupitia maumivu ukiwa timamu bila ganzi?
Dah, hongera sana mkuu umeuliza swali zuri sana ambalo sikuwahi kabisa kufikiria.

Nimeegemea zaidi kwenye mapito ya kihisia na kiakili mfano huzuni, shauku, woga nk.

Haya ya kimwili hayana mbabe aiseeπŸ˜…
Kuna viwango huwezi kujikaza.
 
Mm iko normal.

sitetei pombe. Ila pombe sio kisababishi kikubwa cha Figo kama watu wanavyodhani.

BP unaweza pata pia hata kama haunywi bia.

Figo inaweza kudhurika pia na sumu au kemikali. (Madawa bila mpangilio au kuzidsha dose).
 
Bruh adjee
 
Pombe si Tatizo, Tatizo ni Wanywaji.

Pombe nzuri ni ile Fermented, Sio hizo sanitizers (Spirits).

Alaf hapa unachanganya na Mo energy au Azam energy. Ukitoka hapo unaenda sarandia Mwanamke.

moyo unakimbia Hamilton anasubiri πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Alaf hapa unachanganya na Mo energy au Azam energy. Ukitoka hapo unaenda sarandia Mwanamke.

moyo unakimbia Hamilton anasubiri πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Noma mzee.

Alafu lawama anarushiwa Pombe badala ya Sanitizers.
 
Wanaoongoza BP sio wanywaji pombe zingatia ilo.
 
Addiction mkuu. It is all we think is making us free at moments of frustration.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…