Kwanini wazungu na matajiri hawaangushwi na mapepo?

Kutoa madai ya moja kwa moja kwamba Mungu yupo bila uthibitisho pia ni UONGO.

Na huyo Mungu unayedai yupo bila uthibitisho hayupo.

Ukibisha Mungu hayupo, thibitisha Mungu yupo.
 
Kutoa madai ya moja kwa moja kwamba Mungu yupo bila uthibitisho pia ni UONGO.

Na huyo Mungu unayedai yupo bila uthibitisho hayupo.

Ukibisha Mungu hayupo, thibitisha Mungu yupo.
Ingekuwa hivyo basi Agnostic nao wangekuwa wanadai hakuna Mungu maana nao hawaamini Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho ila kutokuwepo kwa huo uthibitisho hakujafanya waweze kujua kuwa hakuna Mungu.

Nimeeleza kwamba kuna wengine wanakubali uwepo wa Mungu ila wanapinga vile huyo Mungu anavyoelezwa na dini, ila wewe mwenzetu ndio unajua tena kwa uhakika kuwa hakuna Mungu.
 
Niliwahi pata rafiki wa kimarekani, mtu mzima hivi alikuja kutafiti mambo ya madini. Kuna siku tulipanga tuonane ilikuwa jumapili, basi nilipokutana nae nikamwambia nimetoka kanisani!

Akaniambia muda uliotumia kwenda kanisani umeupoteza bila sababu ha msingi. Nikamwambia nilikwenda kusali, akaniambia wewe ni mpoteza muda. Nahisi aliniheshimu sana angeweza kuniambia kwa namna kali, wenda hakutaka niwe Offended.
 
Ushahidi upo?. Kama kweli basi shetani wake alikuwa junior kakutana na mashetani ya senior huyo
Mimi nazungumzia kuhusu mganga kuweza kurogwa ila wewe unazungumzia mashetani, hao mashetani wenyewe tu wanarogwa vile vile na mashetani wenzao au binaadamu.

Au wewe mkuu unafikiri shetani ndio uchawi wenyewe kwamba ukiwa na shetani haiwezekani ikatokea kurogwa au kwamba shetani hawezi kurogeka?
 
Hivi mtu anawezaje kumwambia mtu mwengine anapoteza muda kwa kufanya mambo yaliyo katika ratiba zake? Kuna watu wa ajabu sana.
 
Wakati JK anaangushwa alikuwa masikini!!??
 
Mkuu mimi najua shetani ndio uchawi wenyewe, Nipe elimu kidogo kama utakuwa na wakati wa kunipatia hii elimu hapa.
 
Mfuasi wa shetani aangushwe na Shetani?. Hivi umewahi sikia mganga amerogwa😂?.

Mfano mwengine ushawahi sikia wapi duniani mkuu wa nchi alipata pepo mbaya au alirogwa na kurogeka?.
Kama inakuja hivi
 
Mkuu mimi najua shetani ndio uchawi wenyewe, Nipe elimu kidogo kama utakuwa na wakati wa kunipatia hii elimu hapa.
Uchawi ni uchawi na shetani ni shetani, wapo baadhi ya mashetani wana ujuzi wa huo uchawi na hufundisha watu uchawi na baadhi yao hutumika katika uchawi.

Na ndio maana kuna matatizo mengine yanaweza yasiwe uchawi ikawa ni mashetani tu ndio yanasumbua au kusababisha madhara, sasa ingekuwa mashetani ndio uchawi wenyewe basi kusingekuwa na kutofautisha kati ya matatizo ya kichawi na ya kishetani ingekuwa hata wale wanaotolewa mapepo (mashetani) tungesema wanatolewa uchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…