Kwanini wazungu na matajiri hawaangushwi na mapepo?

Kwanini wazungu na matajiri hawaangushwi na mapepo?

Mapepo yapo.

Kuna mdogo wangu upande wa mama mdogo. Ni wa kike mwaka 2023 alisema kuna jamaa anakuja kumtolea mahari - madale .
Na tar ikapangwa. Ila jamaa siku ya tukio hakutokea. Alidai washenga na baba yake mzaz amepata shida akitokea moro kwahiyo wahairishe mahar had wik 1 mbele. Ikaahirishwa.

Baada ya siku 2 yule dada ikatokea tu hawez amka kutoka kitandan mgongo unauma.
Wakambeba na kumpeleka hosp tmj. Baadae agahkan. MRI baada ya siku 2 ikaonyesha kuna pingili 2 za uti wa mgongo zimepishana.
Akaandikiwa dawa na mazoezi.

Ile ishu ya mahar ikaahirishwa tena.

Mazoez na dawa hayakusaidia hata baada ya wiki 2.
Bidada yuko kwa wheelchair.

Kwakuwa Aliita ndugu zake kutoka Moshi kuja kwenye ishu ya mahar. Na wengne wale wazee walikuwa bado hajaondoka na wakamshaur hebu tukupeleke kwa maombezi .

Wakampeleka kwa Suguye.
Siku ya maombez ya wenye shida.

Kafika na maombez yameanza . Mdada kaanguka, piga kelele sana.
Wakauliza nn shida wakaambiwa . Wakazidisha maomb. Baada ya kuzinduka. Akasimama mwenyewe.
Akawa amepona ile pingil za uti wa mgongo.
Alirud home bila wheelchair. Na had leo hakuwah rud kwa mazoez wala maumivu na lile tatizo halijajirudia.

Wazee wa kichaga baada ya kuona maombez yamefanya kazi.
Wakaonganisha na dot za mahar kutofanikiwa na kuumwa gafla.
Wakasitisha kabisa bint yao asijihusishe na yule mwanaume na wakamwambia asije maana Bint yao haolewi.

Hawakutana kupiga ramri. Ila Logic tu inakuambia kuwa jamaa atakuwa ana mwanamke wake mwingne ambaye hakutaka jamaa atoe mahar na aoe.

Kila nikifikiria hii ishu iliyotokea kwa ndugu wangu wa karibu na nimeshuhudia mwenyewe.
Nina amini Mapepo yako na Mungu yuko.
 
Hakuna Mapepo.

Hakuna Shetani.

Hakuna uchawi.

Hakuna Mungu.

Habari zozote zinazohusu mapepo, majini, Shetani, Mungu, uchawi ni hadithi za danganya toto.
Mzee uchawi upo aise! Watu Wana nguvu za kuamuru vitu vitokee na vinatokea.
 
Hakuna Mapepo.

Hakuna Shetani.

Hakuna uchawi.

Hakuna Mungu.

Habari zozote zinazohusu mapepo, majini, Shetani, Mungu, uchawi ni hadithi za danganya toto.
Kwaio mkuu we ukiamka au hata ukilala hushukuru kwa namna yoyote ile ,yani we ni chapa ilale .Na pia vipi kwenye majukumu yako unaamini vipi katika mafanikio yako bila nguvu ya Mwenyezi Mungu.
 
Sijambo laaziz, mzima wewe? 😹

Ila JF una mpenzi na mwenyewe hujui..!!
Tatizo ni ubishi wenu! Kama ilivyo Ada, nilitangaza zaidi ya wiki tatu zinazokubaliwa kisheria kuwa nakusudia kutwa Greenland ya hapa JF, kama Trump alivyojinasibu. Mwenzangu kapata upinzani usio wa kawaida. Mimi hakuna mtu hapa JF alionesha tashwishi kuwa wewe ni wake. Au anakutaka, kwa mstakbari huo, Kwanini nisisonge mbele mpaka kWa Mzee wa Upako mojawapo ya Jumapili utakapookoka kama mimi? Imeandikwa, mwanamke huwa hapendi, anapendwa. Ndo nishakupenda hivyo (in JK’s Voice)
 
Kuzaliwa Africa ni laana yani hadi leo karne ya 21 bado hujui hata wazungu wanasumbuliwa na mapepo?

Zile movies za kutisha wanazotoa kila leo tena true story zimerekodiwa na kanisa nazo hamzionagi?

CCM isitoke madarakani aisee kama vijana wenyewe ndo hawa tia mchuzi
Kuna watu wamebeba ile misimamo tu ya wazungu ila hawacuatilii ni yapi hasa yaliyopo kwenye hizo jamii za wazungu. Kuna mtu kwa sababu anajua kwamba kwa kiasi kikubwa wazungu wanaamini sana katika sayansi basi anadhani huko kwa wazungu hakuna mambo kuhusu uchawi,majini,ramli n.k
 
Mfuasi wa shetani aangushwe na Shetani?. Hivi umewahi sikia mganga amerogwa😂?.

Mfano mwengine ushawahi sikia wapi duniani mkuu wa nchi alipata pepo mbaya au alirogwa na kurogeka?.
Mganga anarogwa mbona mkuu.
 
Kwa sababu wewe umesema.
Mnahangaika sana kuongelea habari za Mungu, Shetani, Mapepo, majini.

Lakini wao wenyewe, hawajawahi kujidhihirisha wenyewe.

Mnahangaika kufosi uwepo wa viumbe wa kufikirika.
 
Kwaio mkuu we ukiamka au hata ukilala hushukuru kwa namna yoyote ile
Unashukuru nini?

Yani una hustle kwa jasho na nguvu zako mwenyewe, Halafu unashukuru Mungu wa kutungwa!

Mimi labda nijishukuru mwenyewe au nimshukuru binadamu mwenzangu. Sio Mungu wa kusadikika ambaye hayupo.
,yani we ni chapa ilale .Na pia vipi kwenye majukumu yako unaamini vipi katika mafanikio yako bila nguvu ya Mwenyezi Mungu.
Mimi ni Atheist.

Siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yoyote ile ya Mungu au miungu.

Sihitaji kuamini, nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Hakuna Mungu.

Hakuna nguvu ya Mungu kwenye kitu au jambo lolote.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.
 
Mzee uchawi upo aise! Watu Wana nguvu za kuamuru vitu vitokee na vinatokea.
Uchawi ungekuwepo kweli, mababu zetu wasingeuwawa kama kuku, enzi za utumwa na ukoloni.

Huo uchawi ungewasaidia kuwashinda wazungu.

Uchawi ungekuwepo kweli, Nchi za Afrika zingekuwa zinautumia huo uchawi kwenye michezo na mashindano makubwa ya kimataifa kama world cup.

Lakini hakuna nchi hata moja ya Afrika iliyowahi kutwaa kombe la dunia.

Hao watu wenye nguvu za kuamuru vitu vitokee, wangekuwa wanaamuru mafanikio kwa bara la Afrika katika mashindano makubwa ya kimataifa.

Lakini kiko wapi?
 
Back
Top Bottom