Swali lako nimeishalijibu katika maelezo ya uzi wangu, ila naona hujaelewa.
Sikiliza ndugu. Katika Mathayo 1:23 tunaona unabii wa Isaya 7:14 ukitimizwa kuwa Yesu ataitwa Emanueli, yaani "Mungu pamoja nasi"
Jina Emanueli linaonyesha kuwa Yesu hakuwa mtu wa kawaida bali ni Mungu aliyekuja kuishi kati ya wanadamu. Andiko hilo linaendana na Yohana 1:14, inayoeleza kuwa "Neno(Mungu) alifanyika mwili, akakaa kwetu."
Hiyo ndiyo sababu nimekuambia Yesu alipokuwa duniani alivaa ubinadamu.
Nakutajia hapa aya nyingine zinazothibitisha kuwa Yesu ni Mungu aliyekuja katika mwili:
1. Yesu alisema katika Yohana 10:30 – "Mimi na Baba tu umoja."
2. Yesu alijitambulisha kwa jina la Mungu: ‘Mimi Niko’ (Ego Eimi)
Yohana 8:58 – "Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Kabla ya Ibrahimu kuwako, Mimi niko."
Mimi Niko ni jina ambalo Mungu alilitumia alipomwambia Musa: "Mimi Niko ambaye Niko" (Kutoka 3:14).
3. Yesu alisamehe dhambi – jambo linalofanywa na Mungu pekee
Marko 2:5-7 – Yesu alipomsamehe mtu aliyepooza dhambi zake, waandishi wa sheria walishangaa na kusema: "Kwa nini huyu anasema hivi? Anatukana! Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?"
4. Tomaso alimwita Yesu Mungu
Yohana 20:28 – "Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!"
Yesu hakukataa kuitwa Mungu, badala yake akasema "heri aaminiye pasipo kuona"
5. Yesu alisema Yeye ni Alfa na Omega
Ufunuo 22:13 – "Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho..."
Hiyo ni sifa ya Mungu pekee (Isaya 44:6).
Uungu wa Yesu ndio uliomuwezesha kutenda miujiza mikubwa ambayo mwanadamu wa kawaida hawezi kuitenda.
Hebu tuangalie Yohana 10:30 "Mimi (Yesu) na Baba tu Umoja."
Mstari huu haueleweki kabisa na umetolewa nje ya muktadha, kwa sababu kuanzia mstari wa Yohana 10:23 tunasoma (katika muktadha wa 10:30) kuhusu Yesu akizungumza na Wayahudi.
Katika mstari wa Yohana 10:28-30, akizungumza juu ya wafuasi wake kuwa kondoo wake, yeye asema:
“...Wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wala hakuna awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
Mistari hii inathibitisha tu kwamba Yesu na Baba ni wamoja kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuwanyakua kondoo kutoka mkononi mwa wawili hao.
Haisemi kabisa kwamba Yesu ni sawa na Mungu katika kila jambo.
Kwa hakika maneno ya Yesu, “Baba yangu, aliyenipa wao ni mkuu kuliko WOTE...,” katika Yohana 10:29 yanakanusha kabisa dai hili, la sivyo tunabaki na mkanganyiko tu sentensi tofauti.
Yote inajumuisha kila mtu hata Yesu .
Pia tuangalie mstari wa Yohana 17:20-22 " WOTE WAWE MMOJA. Kama wewe Baba ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, wawe UMOJA ndani yetu.wao, wao ndani yangu, wapate kuwa wakamilifu katika MMOJA".
Katika mstari huu, neno lile lile alilotumia MMOJA, la Kiyunani, HEN limetumika, sio tu kumwelezea Yesu na Baba bali kumwelezea Yesu, Baba na wanafunzi kumi na mmoja wa wale kumi na wawili wa Yesu . Kwa hivyo hapa ikiwa hiyo inaashiria usawa wa kipekee wa 1, tunayo kisa cha kipekee cha 1.
Kuhusu mstari unaozungumziwa, “Mimi na Baba tu Umoja” katika (Yohana 10:30), tunahitaji pia kuzingatia mistari inayofuata mstari wa 30 katika kifungu hicho.
Katika mistari hiyo, Wayahudi wanamshtaki Yesu kwa uwongo kwa kudai kuwa yeye ni Mungu kwa maneno haya.
Hata hivyo anajibu, akithibitisha shitaka lao kuwa si sahihi kwa andiko lao wenyewe:
“Wayahudi wakamjibu, wakisema, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi mawe, bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe kuwa Mungu” (Yohana 10:33).
Yesu anajibu shtaka hili akisema:
"Yesu akawajibu, 'Je, haikuandikwa katika Sheria yenu, Nilisema ninyi ni miungu. Ikiwa anaweza kuwaita miungu, ambao neno la Mungu liliwajia, ninyi mwasema yeye ambaye Baba alimtakasa na kumtuma ulimwenguni, “Unakufuru, kwa sababu nilisema mimi ni Mwana wa Mungu?’” ( Yohana 10:34-36 ) .
Hebu tuangalie Matendo 2:22
“Enyi Waisraeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, MTU aliyethibitishwa na Mungu kwenu...”
Petro katika kitabu cha Matendo anashuhudia juu ya Yesu. Hivyo Yesu hata kwa wanafunzi wake, kama kwa Wakristo wa mapema, bila kutiwa sumu na fundisho la Paulo, alikuwa mwanadamu, si Mungu.