Hii ni game ya kikubwa, Iran wamefyata mkia kuona kumbe walikuwa wanacheza michezo ya hatari wanasingizia hali mbaya ya hewa.
Wakubwa wameuchuna kiimya kama siyo wao.
TOKA MAKTABA:
Hutasikia Mossad kitengo cha ujasusi wa nje, wala Aman kitengo cha utambuzi / military intelligence (MI) au Shin Bet usalama wa ndani wa Israel wakisema lolote lililotokea leo (jana) katika msafara wa helicopter 3 zilizokuwa katika msafara wa Rais Raisi wa Iran.
Hata wachokozwe vipi si Benjamin almaaruf (Bibi) Netanyahu wala hizo idara tatu muhimu za usalama Israel zikitia neno. Ni siri kubwa isiyotakiwa kufahamika na yoyote idarani wala wanasiasa waliotoa idhini, operesheni itabaki katika makabrasha yaliyofungiwa kwa fungua pacha, kufuli na Code kwa miaka kibao kwa ajili ya kuficha taarifa hizo muhimu kwa usalama wa Israel.
Hata Iran ikingamua kuna mkono wa nje unahusika nao watajifanya ni ajali kwa kuwa michezo hii ya kijasusi haihitaji hasira wala mihemuko bali kujifunza wapi wamejikwaa au kufanikiwa, kimya kimya bila kupiga kelele za kuumia huku wakijikakamua kuwa siyo mkono wa maadui bali kazi ya Mungu huku lakini wanaugulia maumivu na kuwajibishana kwa siri