Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KWELI KUNA WANACHADEMA HAMNAZO. UTAWEZAJE KUPIGANIA HAKI BILA KUWA NA KIONGOZI MWANAHARAKATI?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kwa kweli Wanachadema wamenishangaza Sana. Uchaguzi huu umeniongezea uelewa kuhusu CHADEMA inawatu wa aina gani.
Hivi mtu anawezaje kupambania HAKI, ukombozi pasipo kuwa mwanaharakati?
Huwezi tenganisha ukombozi na uanaharakati never ever.
Kama kweli CHADEMA ni chama cha ukombozi kwa wananchi, kupigania HAKI na mabadiliko ya taifa letu haiwezekaniki kuepuka uanaharakati.
Upinzani ambao kimsingi unalenga kupigania ukombozi wa haki za watu kama HAKI za kisiasa, HAKI za kujieleza, Katiba mpya, kukomesha mifumo kandamizi; hauwezi kuitwa chama cha maendeleo bila kuwa chama cha uanaharakati.
Huwezi kuipata Demokrasia bila harakati. Huwezi.
Baada ya ukombozi chama ndio hugeuka kuwa chama cha siasa. Kwa sababu kunakuwa na uwanja sawa, HAKI sawa katika nchi.
Lakini CHADEMA hakitaki kiongozi mwanaharakati alafu wakati huohuo ati wanaitisha maandamano ya kudai Katiba, hivi mmelogwa ninyi au?
CHADEMA hakihitaji kiongozi mwanaharakati lakini kila siku kinaimba kinataka tume Huru ya uchaguzi. Hivi ninyi ni nyumbu?
CHADEMA hakihitaji kiongozi mwanaharakati lakini kila siku kinahangaika kupigania HAKI ya kufanya mikutano ya siasa kwa Uhuru kama wafanyavyo ndugu zao ccm. Hivi ninyi ni kenge Maji?
CHADEMA kila mara wanawekwa korokoroni, wanatekwa, na wengine wameuawa, wanapigania HAKI uchunguzi wa Haki ufanyike lakini hayohyo majitu yanakuambia hayataki kiongozi mwanaharakati! Hivi wanafikiri kwa kutumia makamasi au kitu gani?
Unapopigania Jambo lolote ambalo ni HAKI yako wewe tayari ni mwanaharakati.
Ikiwa upo kwenye chama ambacho kinapigania HAKI Fulani lakini hutaki kiongozi mpigania(mwanaharakati). Ujue wewe unaitwa Nyumbu.
Yaani hujielewi, huelewi nini unafanya, huelewi upo wapi.
Naachia maiki. Nawatakia maandalizi Mema ya sikukuu ya Christmas
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam