KERO Responded LATRA: Nauli Mwendokasi (DART) kwanini imepandishwa bila taarifa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Fanyeni kazi vijana muache kulalamika....!! Nchi inajengwa kwa pesa zetu wenyewe...yaani ongezeko la asilimia 33.3% kutoka nauli ya awali ya 750tsh ni liwafanye mlalamike?
 
Kama inavyosomeka hapo juu, jana na_scan kadi yangu pale Ubungo Maji naona 1000 imekatwa. Nauliza mhudumu inakuaje ananiambia nauli 1000.

Abiria mwingine naye ananiambia tangu usafiri umerudi ndio nauli wanayokatwa. Naambiwa hiyo haijawahi hata tangazwa.

Sasa Hawa LATRA wanafanya kazi gani!? Inakuwaje watu wanajiamulia tu kuwakata abirria nauli wanayotaka kiharamu tu!?

Naamini wanatuona wanyonge na hatuna lolote la kuweza kuwafanya. Hii sio sawa kabisa.
Kwanini usafiri wa umma uliojengwa kwa kodi zao ni gharama kubwa? Kuna mambo hayana mantiki.
 
Kwa Elfu moja sio mbaya,, muhimu huduma iwe nzuri na isije kupanda Tena nauli,maana hawakawii
Sio mbaya!? Kwa faida ya nani!? Kwa nini ipitishwe kimya kimya!? Taratibu za kuomba nauli kupandishwa zimefuatwa!? Zimejali kipato cha wananchi wanaotumia huo usafiri!? Nachokiona hapa ni kuwa "hawana cha kutufanya, wakitaka watapanda na wasipotaka watapanda" ndipo tulipofikia .
 
Kinanifurahisha mimi hata wale vichwa maji walioridhika na kumtetea huyu mwanamke atuongoze kwa sababu tu wanafanana nae dini nao wanapitia msoto ule ule wanaopitia wengine,maji hakuna wote tunalia,nauli imepanda wote tunalia,hospital dawa hakuna wote tunalia,umeme wa kusua sua wote tunalia,majuzi hapa ametuulia ndugu zetu wote tumelia siyo atheist siyo nani siyo nani.

Fact ndogo tu,hatupo Somalia hapa wala Saudia kwamba utaulizwa majina ndiyo upewe huduma spesho popote kwenye taasisi za umma kwa sababu tu mmefanana dini na raisi utapewa huduma spesho pale huyo raisi ameandaa maulid sijui hija ndiyo utaulizwa jina na dini ila mengineyo wazee,fimbo ni ile ile mpaka siku akili zitakapowakaa sawa and unfortunately hamkuumbwa hivyo so tuendelee kufurahia show.
 
ukiona huwezi gharama nunua baisikeli/boda yako au tembea kwa miguu.

Waacheni wenye pesa waendelee kufurahia huduma za usafiri wa mabasi yaendayo kasi
 
Sio mbaya!? Kwa faida ya nani!? Kwa nini ipitishwe kimya kimya!? Taratibu za kuomba nauli kupandishwa zimefuatwa!? Zimejali kipato cha wananchi wanaotumia huo usafiri!? Nachokiona hapa ni kuwa "hawana cha kutufanya, wakitaka watapanda na wasipotaka watapanda" ndipo tulipofikia .
Sasa tunafanyaje mkuu?kuna pakulalamikia?
 
Wahudumu wamechoka kuwahangaikia chenji za sh 200 na 50...

mbezi - kivukoni/Gerezani inatakiwa walipe 2000

Gaza- kivukoni/Gerezani inatakiwa 1500
Huu ni mzaha au!? Unaponunua bando kwenye simu yako kwa kutumia "simu pesa" huwa unarudishiwa chenji!?
 
Fanyeni kazi vijana muache kulalamika....!! Nchi inajengwa kwa pesa zetu wenyewe...yaani ongezeko la asilimia 33.3% kutoka nauli ya awali ya 750tsh ni liwafanye mlalamike?
Kwa hiyo tunalalamika kwa sababu hatufanyi kazi!? Je, tunapokuwa tunapanda hayo mabasi, tunakuwa tunaenda wapi!? Kuzurula!? Na nauli tunayolipa huwa tunapata wapi!? Au mwenyekiti wa ccm wa mtaa ndio huwa anatuoa nauli!?
 
Kwa Elfu moja sio mbaya,, muhimu huduma iwe nzuri na isije kupanda Tena nauli,maana hawakawii
Unasemaje mzee?kwako wewe kutoka Morocco hotel to Fire buku siyo jingi?wewe kuwa na uwezo wa kuilipa hiyo 1,000 siyo tatizo.

Em muwazie mmama mjane anayetakiwa akafungashe dagaa mchele pale ferry aje nao mtaani kuunga unga,aende kwa elfu arudi kwa elfu wakati uwezekano wa kuwaruhusu watu waweke gari zao wafanye nauli Tsh 600 upo ila wanabanwa ili wote mpeleke hela mwendokasi,siyo rahisi kihivyo.
 
ukienda ktk majiji kama Amsterdam utakuta wazungu wengi sana wanatumia usafiri wa baisikeli...nashangaa Tz kwanini raia wanakuwa wavivu kuendesha baiskeli. Eneo fupi la kunyonga pedeli kwa dk 5 tu mtu anataka kutoa 1000-2000..

Baiskeli ndio usafiri mzuri kwa afya zenu.

BMT kupitia chama cha waendesha baiskeli Tanzania (CHABATA) wahamasishe watanzania wazidishe matumizi ya kuendesha baiskeli kwa ajili ya kuboresha afya zao
 
Angalia nilishasemaje kwenye mijadala yangu kuhusu mambo kama haya. Kwa ufupi ni matokeo ya uharibifu. Kama mtu alidhani anaikomoa mamlaka amechelewa. Wacha tufaidike na machumo yetu. Huu ni mwanzo tu. Wacha tule mtori, nyama tutaikuta chini. Mchuma janga hula na wa kwao.
 
Unasemaje mzee?kwako wewe kutoka Morocco hotel to Fire buku siyo jingi?wewe kuwa na uwezo wa kuilipa hiyo 1,000 siyo tatizo.

Em muwazie mmama mjane anayetakiwa akafungashe dagaa mchele pale ferry aje nao mtaani kuunga unga,aende kwa elfu arudi kwa elfu wakati uwezekano wa kuwaruhusu watu waweke gari zao wafanye nauli Tsh 600 upo ila wanabanwa ili wote mpeleke hela mwendokasi,siyo rahisi kihivyo.
Sasa tunafanyaje mkuu,unataka tutekwe
 
Kwa hiyo tunalalamika kwa sababu hatufanyi kazi!? Je, tunapokuwa tunapanda hayo mabasi, tunakuwa tunaenda wapi!? Kuzurula!? Na nauli tunayolipa huwa tunapata wapi!? Au mwenyekiti wa ccm wa mtaa ndio huwa anatuoa nauli!?
yaani sh 250 tu ndio ije kukutoa povu mitandaoni.

250 si pesa ya pipi tu.
 
Kama inavyosomeka hapo juu, jana na_scan kadi yangu pale Ubungo Maji naona 1000 imekatwa. Nauliza mhudumu inakuaje ananiambia nauli 1000.

Abiria mwingine naye ananiambia tangu usafiri umerudi ndio nauli wanayokatwa. Naambiwa hiyo haijawahi hata tangazwa.

Sasa Hawa LATRA wanafanya kazi gani!? Inakuwaje watu wanajiamulia tu kuwakata abirria nauli wanayotaka kiharamu tu!?

Naamini wanatuona wanyonge na hatuna lolote la kuweza kuwafanya. Hii sio sawa kabisa.
Kuna mtu ATAKUJA kakwambia TAFUTA Heraaa/pesa/ helaa (money) MWANAUME hawatiagi HURUMA...
 
Huu ni mzaha au!? Unaponunua bando kwenye simu yako kwa kutumia "simu pesa" huwa unarudishiwa chenji!?
mlivyochoma vituo vya mwendokasi mlitegemea serikali itoe wapi pesa za dharura kufanya ukarabati ndani ya wiki 2 tu kurudisha huduma?
 
ukiona huwezi gharama nunua baisikeli/boda yako au tembea kwa miguu.

Waacheni wenye pesa waendelee kufurahia huduma za usafiri wa mabasi yaendayo kasi
Wenye pesa siku hizi nao wanatumia mwendokasi!? Nikajua wana teleza na bodaboda , bajaji na magari yao binafsi!? Kwa kuwa wewe mfanyakazi wa mwendokasi huna wasi. Wewe si unapanda bure hayo magari, unaingilia mlango wa mbele. Hongera.
 
Unasemaje mzee?kwako wewe kutoka Morocco hotel to Fire buku siyo jingi?wewe kuwa na uwezo wa kuilipa hiyo 1,000 siyo tatizo.

Em muwazie mmama mjane anayetakiwa akafungashe dagaa mchele pale ferry aje nao mtaani kuunga unga,aende kwa elfu arudi kwa elfu wakati uwezekano wa kuwaruhusu watu waweke gari zao wafanye nauli Tsh 600 upo ila wanabanwa ili wote mpeleke hela mwendokasi,siyo rahisi kihivyo.
Sasa tunafanyaje mkuu,unataka tutekwe
 
Ukiona huwezi kuongezea sh 250 kwenye 750

-NUNUA BAISKELI
- NUNUA PIKIPIKI
-NUNUA GARI
- TEMBEA KWA MIGUU

Napongeza matumizi ya kadi katika kulipa nauli za mwendokasi
maana wabongo wagumu kuacha chenji hata ya sh 50....anakomalia arudishiwe 50 katika rush hours pale Gaza au Gerezani.
 
Back
Top Bottom