wahuni na majambazi walivyochoma moto nani afidie mtumiaji?Kama inavyosomeka hapo juu, jana na_scan kadi yangu pale Ubungo Maji naona 1000 imekatwa. Nauliza mhudumu inakuaje ananiambia nauli 1000.
Abiria mwingine naye ananiambia tangu usafiri umerudi ndio nauli wanayokatwa. Naambiwa hiyo haijawahi hata tangazwa.
Sasa Hawa LATRA wanafanya kazi gani!? Inakuwaje watu wanajiamulia tu kuwakata abirria nauli wanayotaka kiharamu tu!?
Naamini wanatuona wanyonge na hatuna lolote la kuweza kuwafanya. Hii sio sawa kabisa.