Mwanahabari wa Taifa
JF-Expert Member
- May 27, 2020
- 1,588
- 956
- Thread starter
- #21
Amejitahidi ila apunguze kulipa waandishi wa habari ili a-tren
Kwani anatrend Kafulila au kazi za Kafulila?Kwani anatrend Kafulila au kazi za Kafulila?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amejitahidi ila apunguze kulipa waandishi wa habari ili a-tren
Kwani anatrend Kafulila au kazi za Kafulila?Kwani anatrend Kafulila au kazi za Kafulila?
Route plan ndugu yangu, kule unaweza kutokea usagara kwenda mpaka Bugarika, Maina, machinjioni, kakebe ni mipango tu.Kwa jicho la kibiashara kupeleka coaster njia ya bugando ni kujitafutia hasara tu. Abiria wengi huwepo mida ya kuona wagonjwa. Baada ya hapo abiria wa kutafuta sana. Dar tu daladala nyingi mbovu sana . Bongo tupo nyuma kwenye kila kitu
View attachment 2292276
RC Kafulila apiga marufuku ‘michomoko’ kusafirisha abiria Mkoa wa Simiyu
![]()
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC) nchini Tanzania, David Kafulila amepiga marufuku magari madogo maarufu michomoko kusafirisha abiria mkoani humo.
Ni baada ya kuhusika kwenye matukio ya ajali yaliyosababisha vifo vya watu 10 na majeruhi 17 ndani ya siku 12 zilizopita.
Amri ya Kafulila imetolewa leo Jumatano Julai 13, 2022 ikiwa ni siku moja baada ya ajali iliyotokea eneo la Magereza nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu usiku wa kuamkia jana ikihusisha "michomoko" na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 11.
Wakati majina ya marehemu watano waliofariki kwenye ajali ya Simiyu bado hayajawekwa wazi na waliojeruhiwa ni Elizabeth Nestory (26), Yohana Mwita (22), Sumai Mabula (43), Joseph Masanja (32) na Neema Samson (20).
Wengine ni, Felister Maganda (54), Happy Manyama (23), Oscar Nsolo (47), Stephano Stephene (22) na Joyce Manyama (27) huku majeruhi mmoja ambaye yuko kwenye hali mbaya hajafahamika.
soma pia hii
Ajali hiyo litokea baada ya magari madogo mawili madogo aina ya Toyota pro box na Toyota wish yanayosafirisha abiria kati ya miji wa Bariadi Wilaya ya Bariadi na Lamadi wilayani Busega kugongana uso kwa uso.
Tukio hilo limetokea siku 12 pekee baada ya ajali nyingine iliyohusisha “mchomoko” aina Toyota wish iliyotokea eneo la Luguru Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi watano.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi yaliko makao makuu ya Mkoa wa Simiyu, Kafulila amesema magari hayo madogo yanafanya shughuli ya kusafirisha abiria kinyume cha sheria na maelekezo ya Serikali kupitia Mamlaka ya Usafirishaji wa ardhini (Latra).
"Wamiliki na waendeshaji wa nigari haya ya michomoko wamepewa maelekezo ya kufuata ili kuwaruhusu waendelee kufanya kazi ya kusafirisha abiria, lakini ni zaidi ya miezi sita sasa hawajatekeleza,” amesema Kafulila
Mkuu huyo wa mkoa amesema kutokatana na ukaidi wa wamiliki hao huku watu wakiendelea kupoteza maisha na kujeruhiwa katika ajali zinazohusisha magari hayo, Serikali inasitisha shughuli za magari hayo ya kusafirisha abiria kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Usafirishaji inayoipa mamlaka ya kufanya hivyo.
Ametumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji katika sekta ya usafirishaji wa abiria kwenda mkoani Simiyu kuwekeza katika usafirishaji salama kwa mujibu wa sheria.
Naye ofisa mfawidhi wa Latra mkoa wa Simiyu, Amaniel Sekulu amesema kwa mujibu wa leseni, magari madogo yanayofahamika kwa jina maarufu ya ‘mchomoko’ yanayosafirisha abiria katika miji mbalimbali mkoani humo yamesajiliwa kama Taxi, akini badala yake, wamiliki wamebadilisha shughuli kwa kusafirisha abiria kinyume cha sheria.
“Magari haya yanatakiwa kusajiliwa, kupakwa rangi, kuandikwa namba za utambulisho ubavuni na kubandika vibao maalum vinavyoonyesha kuwa ni Taxi na zinatakiwa kupakia abiria kwa idadi inayoruhusiwa kisheria,” amesema Sekulu
======================
WAKATI HUOHUO LATRA YAPIGILIA MSUMALI AGIZO LA KAFULILA, MICHOMOKO YOTE KUONDOLEWA BARABARANI NCHI NZIMA!
Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini( LATRA) limetoa tamko kali kuunga mkono maamuzi magumu aliyochukua Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Kafulila ya kupiga marufuku gari ndogo zinazotumika kusafirisha abiria maarufu kama michomomoko kuanzia Julai13, 2022.
Kafulila alipiga marufuku gari hizo kuendelea kutumika kutokana na kuwa sababu kuu ya ajali mkoani Simiyu kufuatia gari hizo kutimika kubeba abiria wengi na kukaidi agizo lake la muds mrefu kutaka zitumike kama taxi badala ya kujigeuza daladala kwa kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo. " Kwakua kutokana na mwenendo usioridhisha gari hizi zimekuwa chanzo kikubwa cha ajali, na kwakuwa gari hizi zimekaidi maelekezo ya serikali kutaka zifuate taratibu za kujiendesha kama taxi kwa kisingizio kuwa mfumo huo haulipi kibiashara, basi kuanzia leo Julai13, 2022, nasitisha usafiri wa MICHOMOKO mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo" alisisitiza RC Kafulila.
Katika tamko Lao, LATRA wamesisitiza mikoa wakuu wa mikoa mingine kufuata mfano huo kukabili tatizo la ajali nchini kwani gari hizo sio salama , nihatari kwa usalama wa wananchi kwani zimekuwa chanzo cha ajali maeneo mengi nchini na kuahidi kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo jeshi la polisi kuhakikisha inafanyika opareshen nchi nzima
View attachment 2292287View attachment 2292289
RC Kafulila anatumia kifungu cha 25 cha kwenye sheria ya Land Transport Reguratory Act
View attachment 2292293
Nae kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani ACP Wilbroad Mtafungwa amekandamizia kuwa sasa Tanzania michomoko basi kwa usalama wa Watanzania na mali zao, msikilize mpaka mwisho huyu Mwamba,
Tatizo watu wanafanya maamuzi wakiwa wamekaa kwenye ofisi kwenye makochi hawaelewi huko nje kuna niniKwa mkoa km kigoma kupiga marufuku michomoko ni kuwataka waha watembee kwa miguu michomoko ndo mkombozi wa huku hakuna mabasi njia mbovu hakuna tajiri anayeweza kurisk Basi lake kulileta kwenye njia za mbavu za mbwa km kigoma cha muhimu wazuiwe kujaza kupita kiasi traffic barabarani walisimamie hilo
Unadhani kwa akili yako abiria wanapenda hiyo hali au wanalazimika tu kupanda sababu mbadala haipoHizi gari ni shida yaani mtu anapakia abiria hadi mwenyew dereva anakaa upande upande na zipigwe marufuku tu
Huu ndo ukweli ila tatizo ni kupakia abiria kama ndizi wengine wanakaliana, siti ya dereva anakaa yeye na abiria mmoja, halafu speed yake ni ya hatari.Hujafika maeneo ya wilayani yenye shida za usafiri wewe
Haya mambo ya ku.copy na ku paste sheria za wazungu na kuzifanya za Latra bila kuangalia mazingira yetu na hali ya uchumi wa watu wetu ni ujinga
Maeneo mengi mabasi hamna hasa mawilayani na yakiwepo.machache kuna route njia mbaya wenye basi hawapendi au hawataki sababu ya gharama za.mafuta wanaona hailipi.Mchomoko unatumia mafuta kidogo na waweza enda route zenye watu wachache ambako mabasi machache au hayapo au route mbaya
Yaani kiongozi ndo akurekebishie maisha?Haya ndio mambo anayoyaweza Kafulila ila kukuza elimu, uchumi na ku-improve maisha ya wananchi wanyonge kwa ujumla wake ni sifuri...
Anyways, ni uamuzi utakaopunguza kidogo kasi ya ukuaji uchumi kwa kupunguza ajira na kuongeza shida ya usafiri lakini utakaopunguza ajali na kuokoa uhai na kupunguza vilema.
I think it's worth it.
Kigoma wapunguze speed Tu maana michomoko ya Kasulu- Mvugwe au daladala za Kasulu-Kibondo zinakimbia utadhani dreva ameitwa na shetani.Kwa mkoa km kigoma kupiga marufuku michomoko ni kuwataka waha watembee kwa miguu michomoko ndo mkombozi wa huku hakuna mabasi njia mbovu hakuna tajiri anayeweza kurisk Basi lake kulileta kwenye njia za mbavu za mbwa km kigoma cha muhimu wazuiwe kujaza kupita kiasi traffic barabarani walisimamie hilo
Hujasoma vizuri walishapewa onyo kuzidisha abiria na Bado wanaendelea kwaiyo kma changamoto ni hiyo ndo uende kinyume na utaratibu kwaiyo vifo ni Bora kuliko kufata Sheria iliyowekwa ili kupunguza ajaliUnadhani kwa akili yako abiria wanapenda hiyo hali au wanalazimika tu kupanda sababu mbadala haipo
Pili unadhani matajiri wa mabasi hawaoni hiyo fursa waweke mabasi yao au kuongeza idadi ? Ukiona hivyo ujue kuna changamoto eneo hilo ambazo unatakiwa ushughulikie kwanza
Sio tu kukurupuka tu usingizini na kusema kuanzia leo michomoko marufuku
Na bahati nzuri barabara ya kibondo -kasulu muda wote huwa ni mkeka kwa kweli wale wajinga wanatembea hatariKigoma wapunguze speed Tu maana michomoko ya Kasulu- Mvugwe au daladala za Kasulu-Kibondo zinakimbia utadhani dreva ameitwa na shetani.
Kwanini hazipaswi? Je ukifanikiwa kuzitoa kwenye biashara ya abiria, utazikataza na matumizi binafsi ,kama misiba ,sherehe na kupeleka vijana mashambani?Hizo gari na Noah hazipaswi tumika safirisha abiria
Kwa hiyo michomoko yote nchi nzima imegongana uso kwa uso hadi ipigwe marufuku nchi nzima? Huo ni ujingaHujasoma vizuri walishapewa onyo kuzidisha abiria na Bado wanaendelea kwaiyo kma changamoto ni hiyo ndo uende kinyume na utaratibu kwaiyo vifo ni Bora kuliko kufata Sheria iliyowekwa ili kupunguza ajali
Panda trekta kama huna haraka sio lazima upande michomoko achia wengine wenye haraka zao wapande michomokoKigoma wapunguze speed Tu maana michomoko ya Kasulu- Mvugwe au daladala za Kasulu-Kibondo zinakimbia utadhani dreva ameitwa na shetani.
Hizo daladala dereva anakosa pa kukaa??kiasi akae upande unajua upande dereva kwenye mchomoko wanakaa watu wanne hiyo ni sawa dereva anaendeshaje paleKwa hiyo michomoko yote nchi nzima imegongana uso kwa uso hadi ipigwe marufuku nchi nzima? Huo ni ujinga
Sheria zipo dereva akisababisha ajali hata Kuua unashughulika na huyo dereva sio mwenye gari ndio maana ninaita uamuzi wa kijinga
Gari ikijaza kupitiliza traffic wako kibao mibarabarani kusimamia hiyo mionyo ya ohh usijaze kupitiliza!! Bila kujali eneo hilo usafiri ukoje!! Maeneo mfano Dar es salaam route za mbagala na gombolamboto asubuhi na jioni ukisema dalasala wasijaze kupitiliza Kesho abiria wa hizo route wataandamana kupinga hadi ikulu hilo Tatizo kutokana na shida kubwa ya usafiri maeneo hayo.Hapo Dar mikoani huko mawilayani hali mbaya zaidi
Hayo maamuzi yaliyotolewa sio sahihi ni usumbufu na kuleta Kero kwa wananchi wamiliki na wafanyakazi wa michomoko ambao maisha yao tegemeo lao liko kwenye michomoko
Waziri husika atengue huo uamuzi kabla halijapata sintofahamu kwa wananchi
Hata kama mbadala haujapatikana, maamuzi aliyochua Kafulila ni sahihi ili kuokoa maisha ya wananchi.Mbadala wake nini baada ya kupiga marufuku? Je upo kwa sasa huo.mbadala?
Shida ya usafiri ndio inakuwa hivyo abiria wanataka hivyo kutokana na shida ya usafiri na dreva hana shida anasaidia wenye shida wenzie na wameshazoea hizo shida wanajua dereva ataendesha kwa shida lakini watafika kila moja akiomba Mungu wafike salama waendako maana usafiri mgumu hakuna namna.Dereva anavumilia mkao wa abiria na dereva anavumilia mkoa wa abiria sababu kuendesha mkao huo kwahitaji dereva mvumilivu piaHizo daladala dereva anakosa pa kukaa??kiasi akae upande unajua upande dereva kwenye mchomoko wanakaa watu wanne hiyo ni sawa dereva anaendeshaje pale