LATRA yapiga Stop usafirishaji kwa kutumia magari madogo kuepuka ajali za kila siku

Ni lini watazuia na bodaboda sasa?

Kwa hayo maelezo ya Afisa mfawidhi wa LATRA-Simiyu Bwana Sekulu,shida siyo michomoko bali ni wasimamia sheria wenyewe.

Je ile michomoko inayotoa hudumu kwa kuzingatia sheria wao wanazuiwa kwa misingi ipi?
 
Kwa jicho la kibiashara kupeleka coaster njia ya bugando ni kujitafutia hasara tu. Abiria wengi huwepo mida ya kuona wagonjwa. Baada ya hapo abiria wa kutafuta sana. Dar tu daladala nyingi mbovu sana . Bongo tupo nyuma kwenye kila kitu
Route plan ndugu yangu, kule unaweza kutokea usagara kwenda mpaka Bugarika, Maina, machinjioni, kakebe ni mipango tu.
 
Hizi gari ni shida yaani mtu anapakia abiria hadi mwenyew dereva anakaa upande upande na zipigwe marufuku tu
 
Huyu ni kichaa, kila aina ya gari inaweza kupata ajari, kwa vile bunduki zinaua huwezi kusema watu wasimiriki bunduki, Chanzo Cha ajari si aina ya gari, huwezi kusema kwavile bodaboda zinaua, basi huo usafiri upigwe marufuku, chanzo sio bodaboda kama chombo Cha usafiri,ni utumiaji ndio unaleta shida.

Sasa huyu analipwa mshahara, anategemea wananchi wengine wapate wapi mapato ya kuendesha maisha!
 
Tatizo watu wanafanya maamuzi wakiwa wamekaa kwenye ofisi kwenye makochi hawaelewi huko nje kuna nini

Michomoko ndio msaada mkubwa wa usafiri maeneo mengi tu yenye changamoto za usafiri
 
Hizi gari ni shida yaani mtu anapakia abiria hadi mwenyew dereva anakaa upande upande na zipigwe marufuku tu
Unadhani kwa akili yako abiria wanapenda hiyo hali au wanalazimika tu kupanda sababu mbadala haipo

Pili unadhani matajiri wa mabasi hawaoni hiyo fursa waweke mabasi yao au kuongeza idadi ? Ukiona hivyo ujue kuna changamoto eneo hilo ambazo unatakiwa ushughulikie kwanza

Sio tu kukurupuka tu usingizini na kusema kuanzia leo michomoko marufuku
 
Huu ndo ukweli ila tatizo ni kupakia abiria kama ndizi wengine wanakaliana, siti ya dereva anakaa yeye na abiria mmoja, halafu speed yake ni ya hatari.
 
Yaani kiongozi ndo akurekebishie maisha?
 
Kigoma wapunguze speed Tu maana michomoko ya Kasulu- Mvugwe au daladala za Kasulu-Kibondo zinakimbia utadhani dreva ameitwa na shetani.
 
Hujasoma vizuri walishapewa onyo kuzidisha abiria na Bado wanaendelea kwaiyo kma changamoto ni hiyo ndo uende kinyume na utaratibu kwaiyo vifo ni Bora kuliko kufata Sheria iliyowekwa ili kupunguza ajali
 
Sasa nijichange ninunue probox ya kwenda nayo shambani naamin ztashuka bei
 
Kigoma wapunguze speed Tu maana michomoko ya Kasulu- Mvugwe au daladala za Kasulu-Kibondo zinakimbia utadhani dreva ameitwa na shetani.
Na bahati nzuri barabara ya kibondo -kasulu muda wote huwa ni mkeka kwa kweli wale wajinga wanatembea hatari
 
Hujasoma vizuri walishapewa onyo kuzidisha abiria na Bado wanaendelea kwaiyo kma changamoto ni hiyo ndo uende kinyume na utaratibu kwaiyo vifo ni Bora kuliko kufata Sheria iliyowekwa ili kupunguza ajali
Kwa hiyo michomoko yote nchi nzima imegongana uso kwa uso hadi ipigwe marufuku nchi nzima? Huo ni ujinga
Sheria zipo dereva akisababisha ajali hata Kuua unashughulika na huyo dereva sio mwenye gari ndio maana ninaita uamuzi wa kijinga

Gari ikijaza kupitiliza traffic wako kibao mibarabarani kusimamia hiyo mionyo ya ohh usijaze kupitiliza!! Bila kujali eneo hilo usafiri ukoje!! Maeneo mfano Dar es salaam route za mbagala na gombolamboto asubuhi na jioni ukisema dalasala wasijaze kupitiliza Kesho abiria wa hizo route wataandamana kupinga hadi ikulu hilo Tatizo kutokana na shida kubwa ya usafiri maeneo hayo.Hapo Dar mikoani huko mawilayani hali mbaya zaidi

Hayo maamuzi yaliyotolewa sio sahihi ni usumbufu na kuleta Kero kwa wananchi wamiliki na wafanyakazi wa michomoko ambao maisha yao tegemeo lao liko kwenye michomoko

Waziri husika atengue huo uamuzi kabla halijapata sintofahamu kwa wananchi
 
Kigoma wapunguze speed Tu maana michomoko ya Kasulu- Mvugwe au daladala za Kasulu-Kibondo zinakimbia utadhani dreva ameitwa na shetani.
Panda trekta kama huna haraka sio lazima upande michomoko achia wengine wenye haraka zao wapande michomoko
 
Hizo daladala dereva anakosa pa kukaa??kiasi akae upande unajua upande dereva kwenye mchomoko wanakaa watu wanne hiyo ni sawa dereva anaendeshaje pale
 
Mbadala wake nini baada ya kupiga marufuku? Je upo kwa sasa huo.mbadala?
Hata kama mbadala haujapatikana, maamuzi aliyochua Kafulila ni sahihi ili kuokoa maisha ya wananchi.
Kiongozi hawezi kukaa kimya akishuhudia watu anaowaongoza wakiteketea(ndani ya siku 12tu vifo 10!).

Kusema kosa ni la dereva ni sawa ila aina ya vyombo husika na mazingira vinaweza kuwa chanzo pia.
Ninakumbukuka kipindi cha nyuma huko kaskazini njia ya Arusha - Moshi kulikuwa na ajali nyingi sana ambazo chanzo kikuu ilikuwa mabasi madogo 'Hiece'. Serikali iliamua kuyapiga marufuku na zile ajali zikakoma.
 
Hizo daladala dereva anakosa pa kukaa??kiasi akae upande unajua upande dereva kwenye mchomoko wanakaa watu wanne hiyo ni sawa dereva anaendeshaje pale
Shida ya usafiri ndio inakuwa hivyo abiria wanataka hivyo kutokana na shida ya usafiri na dreva hana shida anasaidia wenye shida wenzie na wameshazoea hizo shida wanajua dereva ataendesha kwa shida lakini watafika kila moja akiomba Mungu wafike salama waendako maana usafiri mgumu hakuna namna.Dereva anavumilia mkao wa abiria na dereva anavumilia mkoa wa abiria sababu kuendesha mkao huo kwahitaji dereva mvumilivu pia

Unadhani usafiri ungekuwa mzuri nani angekubali kubanana hivyo?

Hayo maamuzi wametoa ni ya kukurupuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…