Bunda-Lamadi, Bariadi-Lamadi, Mwigumbi-Maswa-Bariadi, huu ndio usafiri wa muda wowote kwa hayo maeneo naona hiki ni kilio kwa madereva na watu waliojiajiri kupitia hayo magari ya michomoko.
Kabla watu wa serikali hawajatoa hili tamko nadhani walikuwa hawakufanya upembuzi yakinifu, uwepo wa hizi gari umefanya kutanuka ama kukua kwa sekta ya ajira isiyo rasmi kwa hayo maeneo, kwa maana unapozuia michomoko isifanye biashara ya kubeba abiria hapo hujamuumiza mwenye gari na dereva tu, uamuzi waliouchukua unaenda kuwaumiza watu wengi sana ktk hayo maeneo, hapo petro station zitakuwa zimepunguza mauzo, watu wa spea za hizo gari watakuwa wamepoteza ama kupungukiwa na wateja, mafundi wa hizo gari pia, waosha magari vilevile kwa wale jamaa zetu wanaowahi minadani zile siku za gulio hizo ndio gari zao za kuwafikisha huko nadhani kwa hiki kabla ya serikali hawajatoa tamko ilitakiwa wakae mezani wajadiliane kwanza, huu uamuzi unakwenda kuwaumiza watu wengi sana, na pengine kuchangia kwa kushuka kwa shughuli za kiuchumi kwa hayo maeneo, tukumbuke nchi yetu bado inachangamoto ya usafiri kutokana na miundombinu ya barabara, kingine sio kila sehemu unaweza kupeleka min bus au basi kubwa kuna sehemu zinapaswa kufanya kazi gari ndogo tu kutokana uchache wa watu, cha msingi wangeweka mpango mkakati kwa madereva na wamiliki ili kuweza kupunguza au kuondokana na hili janga la ajali barabarani kwa sababu hiyo sio ajali ya kwanza kutokea Simiyu, ajali huwa zipo zitakuwepo na zitaendelea kuwepo cha msingi ni kuangalia namna ya kuzipunguza.