LATRA yaruhusu Mabasi ya Dar - Mtwara yapite Barabara ya Songea, Makambako, Iringa kwa dharura

Waruhusu wapite njia ya masasi, liwale hadi ifakara/mahenge japo sio rasmi lakini ni fupi kuliko huo mzunguko na kupunguza gharama ya nauli kwa abiria
Mji wa ifakara umezingirwa na maji ya mto lumemo kutokana na mto kufurika
 
"ikiwa ni dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua mikoa ya Nyanda za Juu Kusini"! Sifa isiyostahili, mikoa ya nyanda za juu kusini ilifunguka tangu wakati wa ukoloni kutokana kuwa na mazao mengi ya kila aina.
 
Nchi kubwa hivi acheni uchoyo,wamegeeni wenzenu kidogo
 
Dar / Moro 8h:15mins! Hapo sijaelewa naomba nieleweshwe.
No. Ni Iringa. Angalia kidude chekundu ndio destination.

Niliiforce Google Map inipitishe Iringa Songea Mtwara.

Maana ukiandika Dar to Mtwara inakupitisha Mkuranga huku.
 
Na haya mafuriko nadhani hiyo option itakuwa sio feasible

Liwale pia madaraja yamebebwa
 

Na. 4. Sasa unataka kila mtu ajiamulie njia ya kupita? Pengine nyie ni vijana wadogo, miaka ya nyuma kulikuwa hakuna utaratibu wa njia au route katika jiji la Dar. Daladala hazikuwa na rangi. Walitumia vibao kutambulisha route. Ilikuwa ni shidaa. Maana daladala zilikuwa zikienda route ambayo ina abiria wengi. Na kila daladala ilikuwa na rundo la vibao chini ya kiti cha dereva. Yeye alichokuwa akifanya ni kuangalia abiria wengi wanaelekea wapi. Kisha kuweka kibao hicho. Yaani ilikuwa ni shida na vurugu kubwa.
kupanga route ni jambo lisilo kwepeka ili kulinda haki za mlaji.
 
Zamani tulikuwa tunaenda mtwara na meli hasa kipindi cha masika.
Kwanini serikali wasilete meli kubwa kama Ile SANTORINI nakumbuka miaka Ile ya 1995-1999 kulikuwa na meli nyingi Sana zinaenda mtwara
 
MOJA YA MIKOA AMBAYO NAHISI SIO TANZANIA BASI NI MTWARA KWA NAMNA ULIVYO NA MIUNDO MBINU MIBOVU.!!! KUNA VIDARAJA UCHWARA SANA.! NJIA YA HOVYO HOVYO KABISA KUWAI KUTOKEA

KWA HIYO NJIA BORA UPANDE NDEGE TU
 
MOJA YA MIKOA AMBAYO NAHISI SIO TANZANIA BASI NI MTWARA KWA NAMNA ULIVYO NA MIUNDO MBINU MIBOVU.!!! KUNA VIDARAJA UCHWARA SANA.! NJIA YA HOVYO HOVYO KABISA KUWAI KUTOKEA

KWA HIYO NJIA BORA UPANDE NDEGE TU
 
Hiyo bajeti iliyotengwa si dhani kama itakidhi hiyo plan inayofanyika hapo. Pia namashaka sana na uwezo wa mkandarasi aliyepewa hiyo kazi.
 

1. Umeelewa tofauti ya ulichoandika na nilichoandika hapo #4?

2. Kwamba kujua unakoelekea hata kama njia si salama mpaka wenye akili ya kulijua hilo wakwamulie.

3. Angalia tena hoja yako, Kulikoni kulazimisha mabasi kwenda kusiko na abiria au njia isiyokuwapo?

4. Hapo #3, wadhani Kuna njia yenye abiria na kupitika itakosa abiria?

5. Kulikoni kulazimisha mtakayo kwenye biashara za watu? Myatakayo nyie si mpeleke ya kwenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…