LATRA yaruhusu Mabasi ya Dar - Mtwara yapite Barabara ya Songea, Makambako, Iringa kwa dharura

Serikali kama ina nia kujenga upya njia hiyo ingepanua angalau njia mbili kila upande ili kupunguza makali ya mabonde, milima na kona kali hasa toka Njombe mpaka Madaba
 
Mabasi yana Bima inayomlinda mmiliki wa gari, abiria na mizigo yake.
Bima inatambua njia rasmi zilizoidhinishwa na LATRA.

Bima haitambui njia za kuchochora (diversion) ambazo zitamfanya dereva awahi kufika au kuchelewa kwa utashi wake.

LATRA ipo kisheria kusimamia na kutoa miongozo ya njia sahihi za kupita ili kuepuka kurundika magari mengi kwenye njia moja.

Hivyo kwa dharula kama hii ya Kilwa LATRA walitakiwa watoe mwongozo.
Bila mwongozo wa LATRA polisi watakamata magari yanayofanya mchepuko wa aina hiyo ili kumlinda abiria na mali zake.
Kila kitu kipo kisheria.
 
Kuna ongezeko la km 1000 zaidi, ni safari ndefu mno kama hauna dharura ni vizuri kusubiri tuu,
 
Kama huna ulazima wa kusafiri bora kukaa tu, kwa nini?

1. Madereva hawana uzoefu na route.
2. Ni risky.

Ikibidi sana usafiri, vunja safari mwenyewe usitumie gari moja kwenye route yote hiyo.
 

Kwa hiyo unaamini katika watu kufanya biashara bila utaratibu? Kwa sababu tu ni biashara zao?
 
Kama huna ulazima wa kusafiri bora kukaa tu, kwa nini?

1. Madereva hawana uzoefu na route.
2. Ni risky.

Ikibidi sana usafiri, vunja safari mwenyewe usitumie gari moja kwenye route yote hiyo.
Hata Mimi hofu yangu madereva kusinzia njiani.
 

1. Bima ni biashara yenye wateja na supplier.

2. Hapo #1 ni willing buyer and willing seller.

3. Bima kufungamanishwa na njia siyo kutokea mbinguni!

4. Hapo #3, kwani magari madogo ya watu yana fungamanishwa na bima ya njia ipi, wapi?

5. Si kweli kuwa mabasi bima zinafungamanishwa na njia.

6. #5, huwa mnatokea wapi na hizi sifia sifia bila facts?!

Shivji: Chimbuko la wasiokuwa na Hoja au uthubutu wa Kuhoji, linalo ligharimu Taifa (Part 1)

7. Wapi nani kasema kuchochora ni ujanja? Au kupitia iringa kwenda lindi kwako ni kuchochora?

8. Kulikoni kuwaona wengine ni wajinga ila ninyi?!

9. Bure kabisa!
 
Lipo Somanga Mkuu, madaraja jumla yaliyokatika ni matatu
Watafute sehemu kupitisha barabara ya dharula... Lakini kuzunguka songea kupitia iringa ni safari ndefu mno... Utoke Dar saa 12 asubuhi... Uingie Songea saa 4 Usiku... Kisha uanze kuitafuta mtwara..??
 
Hapo ndio namkumbuka bw Mwaibula, alianzisha kupiga mistari ya rangi tofauti, na maandishi ya Kila ruti ya daladala,
 
Nadhani ndo itakuwa route ndefu nchini!!!
 
N
Watafute sehemu kupitisha barabara ya dharula... Lakini kuzunguka songea kupitia iringa ni safari ndefu mno... Utoke Dar saa 12 asubuhi... Uingie Songea saa 4 Usiku... Kisha uanze kuitafuta mtwara..??
Hivi ndege za ATC haziwezi kupunguza nauli, na zikafanya ruti za kwenda Mtwara na kurudi kipindi hiki cha dharura?
Hizi si zimenunuliwa kwa kodi ya hawa wanyonge wanaotaabika kuzunguka Songea,
Au wakishazipokea kwa shangwe na shuhuli Yao imeisha, Zinabaki kuwa za viongozi,
 
Nimeona leo taarifa, basi zinatoka mtwara kuja Dar via Songea na nauli ni 120k, Atcl hawana route ya Dar _ Mtwara
 
Sijasoma hiyo barua ya LATRA vipi nauli ni Ile Ile au itaongezeka?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…