LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
Kufuatia latra kutangaza bei mpya za nauli za vyombo vya usafirishaji nchini, baadhi ya wananchi wamehoji iweje nauli kutoka singida to dodoma Kwa basi la daraja la kati iwe shilingi 86,000? Huku umbali wake ni takribani kilometer 1,208 hivi.

Ukiendelea kuichambua takwimu hizo Kuna makosa mengi ambayo inaonesha lATRA hawakuipitia takwimu hizo baada ya kuandaliwa labda na wanafunzi wa Field works.
Mkuu, hapo kwenye umbali wa Singida to Dom umetupiga [emoji28]
 
Serikali naona hawataki kutuona tunarud mikoani kwetu kusalimia wazee. Sasa kwenda bk nauli ya kwenda tu almost laki 1 kutoka dsm hapo bado kula njiani na nauli za kunifikisha stendi... Maisha yanazidi kuwa magumu sasa.

Na hakuna dalili ya gharama kushuka. Sijui nani atatusaidia.
 
Hayo si maamuzi ya mtu mmoja ni jopo kikubwa LATRA siyo muamuzi wa mwisho , Kwa upande wa Kutafuta Kiki Kwa CCM. uenda pia lisemwalo lipo au lajongea.

Msimu wa kusifia huu imebaki kuwaabudu Tu.
 
Wakuu nimeona kitu cha kushangaza kidogo kuna nauli hapo na umbali umenistaajabisha Dom kwenda Dsm kupitia chalinze nauli ni buku tano na umbali ni 80 km hii nauli ya basi au latra wameamua kuutambua rasmi usafiri wa ungo wanaupangia hadi bei?

Au mimi ndiyo sielewi
 
Serikali nayo iache upuuzi bhana.. hivi treni ya mwendokasi imeishia wapi?. Nauli imepandishwa mwaka jana mwezi aprili, leo tena nauli mnapandisha
. Hivi mnajua athari zake kiuchumi kweli?. Mama Samia usicheke na wafanyabiashara watakuharibia. Namkumbuka sana Magufuli kwa kweli.

Serikali imeelemewa na wafanyabiashara. Wafanyabiashara wameiteka.
 
Makonda c alipanda punda. Alionyesha majinga tutakavyoishi. Na kumsindikiza. Alivyoona wamemkubali. Ndo nauli imepandishwa

Kweli mkuu. Halafu kesho akianza ziara wananchi wanaanza kumwambia awasaidie kuhusu nauli imepanda Sana. Halafu Makonda atampigia simu Waziri husika na kumpa wiki moja nauli ishushwe. Halafu wananchi watapiga makofi itaishia hapo.
 

Attachments

  • IMG-20231127-WA0015.jpg
    IMG-20231127-WA0015.jpg
    140.9 KB · Views: 5
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600. Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700.

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900. Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300 na kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400.

Aidha nauli za wanafunzi zitaendelea kusalia 200 kwa safari za masafa mafupi.

Nauli za mabasi zimeorodheshwa kwenye jedwali hapa chini.

View attachment 2826735View attachment 2826734View attachment 2826733View attachment 2826732
Hakika bado tuna safari ndefu. Aliyekaa na kutoa taarifa hii mpaka muda huu hapaswi kuwepo ofisini Hivi kutoka Dodoma hadi Dar ni umbali wa Kilometa 80? Dodoma hadi Morogoro kilometa 1,140!!? Pole sana watanzania na mimi nikiwemo. Chart tu ya Dodoma kwenda maeneo mengine imejaa madudu ya namna hii, vipi kuhusu maeneo mengine na yale ambayo hayako wazi kwa wananchi?
 

Attachments

  • IMG_20231127_200313.jpg
    IMG_20231127_200313.jpg
    109.1 KB · Views: 5
Back
Top Bottom