Mkuu, hapo kwenye umbali wa Singida to Dom umetupiga [emoji28]
 
Serikali naona hawataki kutuona tunarud mikoani kwetu kusalimia wazee. Sasa kwenda bk nauli ya kwenda tu almost laki 1 kutoka dsm hapo bado kula njiani na nauli za kunifikisha stendi... Maisha yanazidi kuwa magumu sasa.

Na hakuna dalili ya gharama kushuka. Sijui nani atatusaidia.
 
Unalipa nauli pesa nyingi afu kuchimba dawa unaambiwa dakika 10,Bora tujitafutie hata IST cha kusafiria hata kama itachukua siku 2 na mafuta ya laki na nusu
Unakuwa free na unaenjoy safari,tukifika shelui tunashuka na kuwa salimia wananchi,
 
Hayo si maamuzi ya mtu mmoja ni jopo kikubwa LATRA siyo muamuzi wa mwisho , Kwa upande wa Kutafuta Kiki Kwa CCM. uenda pia lisemwalo lipo au lajongea.

Msimu wa kusifia huu imebaki kuwaabudu Tu.
 
Wakuu nimeona kitu cha kushangaza kidogo kuna nauli hapo na umbali umenistaajabisha Dom kwenda Dsm kupitia chalinze nauli ni buku tano na umbali ni 80 km hii nauli ya basi au latra wameamua kuutambua rasmi usafiri wa ungo wanaupangia hadi bei?

Au mimi ndiyo sielewi
 

Serikali imeelemewa na wafanyabiashara. Wafanyabiashara wameiteka.
 
Makonda c alipanda punda. Alionyesha majinga tutakavyoishi. Na kumsindikiza. Alivyoona wamemkubali. Ndo nauli imepandishwa

Kweli mkuu. Halafu kesho akianza ziara wananchi wanaanza kumwambia awasaidie kuhusu nauli imepanda Sana. Halafu Makonda atampigia simu Waziri husika na kumpa wiki moja nauli ishushwe. Halafu wananchi watapiga makofi itaishia hapo.
 
Hakika bado tuna safari ndefu. Aliyekaa na kutoa taarifa hii mpaka muda huu hapaswi kuwepo ofisini Hivi kutoka Dodoma hadi Dar ni umbali wa Kilometa 80? Dodoma hadi Morogoro kilometa 1,140!!? Pole sana watanzania na mimi nikiwemo. Chart tu ya Dodoma kwenda maeneo mengine imejaa madudu ya namna hii, vipi kuhusu maeneo mengine na yale ambayo hayako wazi kwa wananchi?
 

Attachments

  • IMG_20231127_200313.jpg
    109.1 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…